Uchaguzi 2020 Kachero Mbobevu Bernard Membe atua nchini, adai ukata umepelekea kusuasua kwa Kampeni za Vyama vya Upinzani nchini

Uchaguzi 2020 Kachero Mbobevu Bernard Membe atua nchini, adai ukata umepelekea kusuasua kwa Kampeni za Vyama vya Upinzani nchini

BERNARD Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, mazingira magumu ya Siasa kwa sasa, yamesababisha marafiki na wafanyabiashara kushindwa kuwasaidia. Na kwamba, kusuasua kwa kampeni hasa vyama vya upinzani nchini, kunatokana na ukweli kwamba, wagombea wengi wana ukata kwani hawana msaada tofauti na chaguzi zilizopita....
Wafanya biashara ya Korosho na Manji wameshindwa kumsaidia ??
 
"Mgombea wa nafasi ya u Raisi kupitia chama cha Act wazalendo Benard Membe amedai vyama vya upinzani zina ukata wa fedha za kampeni haijawahi kutokea."

Una maoni yapi ya kuishauri Serikali iruhusu vyama vya upinzani kupata pesa kutoka kwa marafiki na wakereketwa?
 
Sijawahi kumuelewa hyu mwamba tangu akiwa waziri mpk leo, mwenzangu ebu nitajie ata jema lake moja tu ambalo tunaweza tukajivunia.
Zaidi ya miaka 60 ccm haina lolote ililo wafanyia watanzania zaidi ya kuwatia umasikini tu
 
Ila kampeni za mwaka huu za chadema ni bora na zinatoa mwanga kwa watanzania kuliko miaka mingine..

Pesa ni hila tuu za serikali wakati ccm wanatumia kodi za wananchi kuendesha kampeni.
 
Mie nafkiri tena ingekuwa vizuri sana ukata huo ukazidi mara dufu ili uharakishe ukombozi wa taifa hili! Siku zote binadamu huwa na uwezo mkubwa wa kufikiri kwa haraka na kutumia mbinu na maarifa stahiki pale anapokuwa taabuni!
 
Hilo hata halihitaji phd kuligundua,angalia tu hata

matangazo stcker,bunner,mabango ya upinzani huko

barabarani unapishana nayo mangapi compare na baba lao CCM.
 
Sema mimi mwenyewe nikijuaga hili game sishindi

mkeka naweka vihela vidogo vidogo tuu,hata vikiliwa poa tu lakini

sio kwamba nakua sina hela ila ni kwasababu nishajua huu mkeka kuungua n dk 0 tu.
 
Back
Top Bottom