Mtoa mada kumbuka Kristo ni yule yule Jana leo na hata Milele! Makanisa ya Kimwendo kasi na matapeli wa dini huibuka kama uyoga na hufa hivyo hivyo....walikuwepo wengi na wataendelea kuja wengi, lakin kanisa ni moja, takatifu lenye mizizi ndani ya Kristo wa Ukwel halitajufa mpaka atakapoamua.Huu ni msimu wake huyo Mwamposa, acha aendelee kula vichwa! Walivuma sana hawa leo wako wapi?Kakobe, Mwingira,Ngurumo za upako, marehemu mama Rwakatare,Mzee wa upako makuhani na manabii wa uchawi kila kona!
Neno la kweli ni Kristu na neno litasimama milele mambo yote yatapita....Wewe vuta pumzi mpe muda, kama anachofanya ni kazi ya Mungu haitakufa itatimiza ilichotumwa kwa Kristu hamna mashindano.
Tumsifu Yesu Kristo.