Kadri siku zinavyoenda kanisa katoliki linapotea slowly kwa sababu watu hawataki kusali kimprinsiple preiple.

Kadri siku zinavyoenda kanisa katoliki linapotea slowly kwa sababu watu hawataki kusali kimprinsiple preiple.

Leo nimeona nyomi ile ya watu aliowakusanya Mwamposa kule Arusha hakika nimelisikitia kanisa langu. Kadri maaskofu na mapadre wanavyompinga mwamposa ndo anazidi kuchanja mbuga.

Imekuwaje kanisa katoliki likakosa mvuto hivyo ghafla jamani.
" kimprinsiple preiple."
Misa ya kilatini mnaanza saa ngapi?
 
Jambo usilo lifahamu ni kwamba RC ni Kanisa na taasisi kongwe kabisa duniani, huku likiwa limeanza miaka mingi iliyopita. Mwamposa ni kiumbe mdogo sana ukimlinganidha na Kanisa Katoliki! Atapita kama upepo, na Kanisa litabakia palepale.

Imagine alikuwepo Mzee wa upako! Yuko wapi kwa sasa?
Moses Kulola,Egon Falk,Reinhard Bhonke nk.Mtoto huyo hajui lolote.
 
Tofauti ni Nini?
Tofauti ipo. Kanisa Katoliki liligawanyika mara mbili zaidi ya miaka 1,000 iliyopita. Kuna Kanisa Katoliki la Mashariki (Eastern Catholic Church) almaarufu kama The Orthodox Church na The Western Catholic Church almaarufu kama The Roman Catholic Church. Ndo maana katika jamii ya mchanganyiko lazima ujitambulishe Kwa ufasaha kwamba wewe ni Muumini wa Catholic Church ipi. Roman Catholic au the Eastern Catholic Church
 
Unachekesha kumfananisha Mwamposa na Roman Catholic Church.
Na wasiwasi na uwezo wako wa kuelewa na kupambanua mambo
 
Kwa hiyo kanisa katoliki haliamini kabisa kwamba Maonbi yanaondoa shida za mtu. Sasa mnaenda kanisani kufanya nini, kutoa sadaka
Duh! Yani wewe unaenda kanisani au unasali ili kuomba shida zako tu ziondoke? Vipi, zisipoondoka huendi tena kanisani? Unamfuata Yesu simply kwa sababu ulishiba mikate 5 na samaki 2 na kusaza vikapu 12? (Marko 6:41 na Yohane 6:26.)
Nyie ni wasaka miujiza.
 
Kwa hiyo kanisa katoliki haliamini kabisa kwamba Maonbi yanaondoa shida za mtu. Sasa mnaenda kanisani kufanya nini, kutoa sadaka
Linaamini, lakini si kwa mkumbo mkumbo hivyo au ukomedi komedi. Si huyo mkuu wa Kanisa alisema amefunga na ifikapo mwezi wa 8 mtandao wa Twitta utakuwa umefutwa. Yaani Mungu anaweza kufanyiwa mzaha hivyo?
 
Unachekesha kumfananisha Mwamposa na Roman Catholic Church.
Na wasiwasi na uwezo wako wa kuelewa na kupambanua mambo
Mwamposa ni mtu a person anaweza kufa wakati wowote lakini RC ni Kanisa (Taasisi) milango ya kuzimu haitalishinda i.e Hakuna kufa.
 
Pale miafrika inavyo tetea dini za mabepari kwa kutumia jina la Shetani,Yesu na Mungu.
 
Tatizo unajiona ww ni mkatoliki zaidi. Pengine hapa unaongea na Paroko!
Paroko sio mtu bali ni Ofisi; ni mamlaka. Mtu mwenye kuikalia hiyo Ofisi au Msemaji mkuu katika Ofisi hiyo anaweza kubadilishwa wakati wowote lakini Ofisi itabaki palepale na kuendelea kutoa Huduma.
 
Binadamu toka afanye maasi pale edeni maisha yake yamekuwa ni yakutafta majibu ya changamoto zake. Na hii ndio inawapa manabii, nitumie, mashekhe, waganga nk nguvu ya kupata wafuasi.
Hapo sio kwamba wote waumini wake wengne wapo Hapo ili kupata majibu ya changamoto zao ambazo zimekoswa ufumbuji walipotoka. Ndio maana kwa asilimia kubwa sio kwamba wanamuamini mungu bali wanamuamini mwamposa
 
Watu kama kina Mwamposa wanaibuka na kutoweka, wamekuwepo pia watu kama kina Luther lakini Catholic Church ina miaka 2024 and still counting. Zinakuja nyakati ambapo madhehebu yote ya KiKristo yatarudi Roman Catholic Church sababu RC ndilo msingi, nembo na hitimisho la Ukristo.
 
Watu hawachoki kuzungumzia RC? Tangu nikiwa mtoto RC imesemwa sana, lakini sioni ikitetereka.

Yote haya ni kwa sababu misingi ya imani ya kikatoliki imejengwa katika elimu, tena elimu kubwa, kuanzia Falsafa, theolojia, sayansi na saikolojia.
RC haina individuals kama Mwamposa, RC ina mifumo imara tangu enzi na enzi.

RC kinachofanya kazi si individuals bali ni Sytem.

Never compete with system, you will never win.

They will come, they will go but RC remains.

Extra Ecclesiam Nulla Salus!
 
Back
Top Bottom