Kafulila: Lissu acha kuzipaka matope Mahakama za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa?

Kafulila: Lissu acha kuzipaka matope Mahakama za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa?

Mbona mmetaka ziwafukuza akina Halima mmegonga Mwamba?

Eti Mnataka Rais atoe maelekezo mahakamani hili halipo,

Mahakama zetu ni huru sana
Mkuu acha Tania za kujipendekeza hata huyo Rais mwenyewe anajua kulingana na mifumo yetu Mahakama zetu sio guru sasa wewe umekazana kuubadili uongo kuwa ukweli.Unaweza kuonekana kituko mbele ya watu-kuunga mkono Serikali au viongozi fulani haimanishi kula wakati ni kusema ndio na kusifia bali na kuona penye mapungufu na kuyaonyesha.
 
Rais juzi akiongea na mawakili wa Afrika mashariki alusemaje?
Kwamba nyie tumieni sheria zenu za nje mie nita tumia sheria zangu kuhakikisha......
Huu ndio ushahidi kwamba mahakama zetu ziko mikononi mwa dola. Na haziko huru...
Nje kwa hio wamefanya yao kwa ndani Mahakama zipo chini ya Serikali inaweza kuamua lolote na isiulizwe chochote?

Noma sana Cc: monde arabe
 
Wasalaam wana wa Mungu.

Kwenye ukurasa wake wa tweeter David Zacharia Kafulila amemnyooshea kidole Tundu A. Lissu kwa kila alichokiita ni "Uongo na upotoshaji wa Lissu dhidi ya Mahakama huru za Tanzania "

Tundu A. Lissu ambae ni M/kiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa JMT aliyepata kura kiduchu sana katika Uchaguzi Mkuu uliyopita wa 2020, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Siasa pekee ambaye familia yake yote ni Raia wa Marekani ameonekana mara zote kuwa upande wa mataifa ya nje kuliko taifa lake.

David Zacharia Kafulila anatoa mfano wa nchi kubwa kama Marekani na Uchina zikiwa nchi wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania pamoja na nchi nyingine zaidi ya 166 kumuuliza Tundu A. Lissu kuwa nchi zote hizi Mahakama zao zinaingiliwa kama ilivyo kwa Tanzania ama ni utaratibu tu wa hiari wa kiusuluhishi uliowekwa Duniani katika kuoneaha imani kwa wawekezaji hasa wa nje?

Hoja ya David Zacharia Kafulila kwa Tundu A. Lissu ni kwamba kama Tanzania Mahakama zake siyo huru ndiyo sababu kesi za migogogro ya kibiashara zinafanyikia nje kwenye tume hii ya ICSID. Je, Marekani na Uchina ambazo nazo kesi zao za migogogro ya kibiashara zinafanyikia huko huko ICSID tulikopelekwa sisi kwa hoja ya hiyo ya Lissu anataka tuamini pia kuwa Mahakama za mataifa haya pia haziko huru?

" Lissu acha kuzipaka matope Mahakamani za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa ?"

View attachment 2433362View attachment 2433363

Huyu naye tangu kutumbuliwa anajifanya mtetzi wa serikali.
 
Lissu sio mtu mzuri,

Kwanza yeye watoto wake sio Watanzania,

Hata Kama atatupiganisha tukauana yeye na familia yake atabaki kuwa salama,

Tumwogope kabisa Huyu mtu kwa usalama wa Taifa letu

Asante Mzalendo Kafulila

Akupiganishe na naani. Punguza unafiki ndugu yangu.
 
Tatizo la Ndg yetu Lissu ni Chuki,
Hata vitabu vya Mungu vinatuasa kusameheana,
Mungu amsaidie moyo wa kusameheana

Yeye ndio asamehe?. Mbona serikali haikumsamee , Tena siku ya kesi yake ya ubunge serikali ilileta wanasheria karibia ishirini.
 
Mkuu acha Tania za kujipendekeza hata huyo Rais mwenyewe anajua kulingana na mifumo yetu Mahakama zetu sio guru sasa wewe umekazana kuubadili uongo kuwa ukweli.Unaweza kuonekana kituko mbele ya watu-kuunga mkono Serikali au viongozi fulani haimanishi kula wakati ni kusema ndio na kusifia bali na kuona penye mapungufu na kuyaonyesha.
Tatizo liko wapi kumtetea Rais wa nchi na Serikali yake?
 
Lissu sio mtu mzuri,

Kwanza yeye watoto wake sio Watanzania,

Hata Kama atatupiganisha tukauana yeye na familia yake atabaki kuwa salama,

Tumwogope kabisa Huyu mtu kwa usalama wa Taifa letu

Asante Mzalendo Kafulila

Sio lissu tu, kuna viongozi waandamizi wa chama tawala sito wataja, wana watoto nie tena wajukuu.
Hili suala lilianza enzi za mkapa, na umekuwa utamaduni wa viongozi wengi
 
Sio lissu tu, kuna viongozi waandamizi wa chama tawala sito wataja, wana watoto nie tena wajukuu.
Hili suala lilianza enzi za mkapa, na umekuwa utamaduni wa viongozi wengi
Nadhani watajwe tu sio jambo la kizalendo hata kidogo
 
Back
Top Bottom