Kafulila: Lissu acha kuzipaka matope Mahakama za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa?

Kafulila: Lissu acha kuzipaka matope Mahakama za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa?

Huyu Bwana amekuwa Mtetezi wa CCM ?

Hata kama CCM wapo sawa na kila kitu ni Sawia kwamba wamekosa watetezi kiasi hiki hadi huyu afanye hio Kazi ?

Kwanini asiwaachie wengine wafanye utetezi yeye atafute hata baya moja aliongelee..., au yote ni mazuri ?

Kama kuna anayemjua muombe azungumzie na haya:-
  1. Tuhuma za Ndugai
  2. Mikopo kama hatuna akili nzuri na allocation za mikopo
  3. Bunge kuwa zaidi ya Rubber Stamp
  4. Mfumuko wa Bei na Maisha kuendelea kuwa ndivyo sivyo
  5. Mgao wa Umeme
  6. Adui Mpya anayelitafuna Taifa (Uchawa)
  7. Ukosefu wa kazi zenye ujira (Time Bomb) tunalolilea
  8. Kutokuwepo na Sera zinazoeleweka
  9. Tabia ya kuwa ombaomba na kila kitu kuwapa wadau ndio wafanye...
 
Nadhani mjibuni hoja yake achaneni na hoja kwamba anatafuta UTEUZI
hoja gani huyo kafulila ndio anapotosha mwambie aweke clip ya lissu tuisikilize neno kwa neno ndio ueleww alichosema Lissu na kama hujui lissu alichosema ni kwamba mara nyingi serikali hutumia ubabe ndio maana inalazimika njia ya utatuz wa migogoro kwenda kwenye arbitration for determination of the matter in dispute na akarejea for the case at hand serikali kama ya tanzania ni serikali ya hovyo inayofikir inaweza kutumia ubabe kwenye mambo ya uwekezaji wa kigeni.

Na kama huna taarifa mamayenu juz kule Arusha kwenye kongamano la East African Lawyers Association alisema nin?

Alisema kwamba nyie tumien sheria za nje na mim nitatumia zangu za ndan sasa hapo kuna akili nan alikua anamtisha mwambien atumie hizo za ndan sasa tuone halafu huyu kafulila anafikir watu wote ni hamnazo kama wajinga wenzie kule ccm.
 
kwa Tanzania ukiwa msema kweli unaonekana mamluki wa mabeberu
Tatizo la Tanzania sio kusema ukweli bali wanatizama ni nani anasema, kuna watu hata wakisema ukweli watu wataishia kumjadili yeye badala ya hoja yake na wengine hata wakipitosha watasikilizwa kwa sababu aliyesema ni fulani.
 
Wasalaam wana wa Mungu.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Kafulila, amekosoa kauli ya Makam Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu hoja ya kesi kukamatwa ndege...
Ila kiukwel kbs bila kupepesa macho hii nchi yetu watu wangekua wanatoa maoni yao aku kusema ukwel bila kutegemea kupata chochote kitu iwe pesa au madaraka, sidhan kama tawala hizi zingepata sapoti!!
 
Wasalaam wana wa Mungu.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Kafulila, amekosoa kauli ya Makam Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu hoja ya kesi kukamatwa ndege na zingine mashauli yake kushughulikiwa kwenye mabaraza la usuluhishi ya kibiashara kama ICSID- international Center For Settlement of Investment Disputes.

====

Akikosoa kauli hiyo, Kafulila amenukuliwa kwenye mtandao wa tweeter akisema kuwa " Sitaki kujadili suala la kesi, naomba nijadili suala moja tu la uelewa kuhusu ICSID na uanachama wake kwani Lissu amepotosha katika hilo na anawezafanya wasiojua kuamini kwamba Tanzania ni mwanachama wa ICSID Sababu ya udhaifu wa Mahakama na Serikali katika kusimamia uhuru wa Mahakama

TunduLissu alinukuliwa kupitia ClubHouse akieleza kuwa " Lazma ieleweke kuwa sababu ya mashauri haya ya mikataba baina yetu na kampuni za nje kushughulikiwa kwenye mabaraza haya ya usuluhishi wa migogoro ya biashara na uwekezaji kama ICSID inatokana na tabia ya Serikali yetu ikiwa chini ya JPM na hata Samia kuingilia mambo ya mahakama na hivyo mahakama kukosa uhuru. Hivyo mahakama zetu haziaminiki, serikali yetu haiaminiki, hatuaminiki kwasababu ya rushwa za majaji na kuingiliwa na Ikulu. ndio sababu mashauri haya yanamuliwa ICSID "

Tundu A. Lissu ambae ni M/kiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa JMT aliyepata kura kiduchu sana katika Uchaguzi Mkuu uliyopita wa 2020, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Siasa pekee ambaye familia yake yote ni Raia wa Marekani ameonekana mara zote kuwa upande wa mataifa ya nje kuliko taifa lake.

David Zacharia Kafulila anatoa mfano wa nchi kubwa kama Marekani na Uchina zikiwa nchi wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania pamoja na nchi nyingine zaidi ya 166 kumuuliza Tundu A. Lissu kuwa nchi zote hizi Mahakama zao zinaingiliwa kama ilivyo kwa Tanzania ama ni utaratibu tu wa hiari wa kiusuluhishi uliowekwa Duniani katika kuoneaha imani kwa wawekezaji hasa wa nje?

Hoja ya David Zacharia Kafulila kwa Tundu A. Lissu ni kwamba kama Tanzania Mahakama zake siyo huru ndiyo sababu kesi za migogogro ya kibiashara zinafanyikia nje kwenye tume hii ya ICSID. Je, Marekani na Uchina ambazo nazo kesi zao za migogogro ya kibiashara zinafanyikia huko huko ICSID tulikopelekwa sisi kwa hoja ya hiyo ya Lissu anataka tuamini pia kuwa Mahakama za mataifa haya pia haziko huru?

" Lissu acha kuzipaka matope Mahakamani za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa ?"

View attachment 2433362View attachment 2433363
Kafulila wa hoja , kafulia Hoja !
 
Tatizo la Ndg yetu Lissu ni Chuki

Hata vitabu vya Mungu vinatuasa kusameheana

Mungu amsaidie moyo wa kusameheana
Umerukia kuandika "Mungu amsaidie moyo wa kusameheana"!Kwani kuna mtu alimuudhi?Alimuudhi kwa nini?Kusamehe ni hiyari au lazima?Unaweza kumchagulia mtu uamuzi?
 
Back
Top Bottom