Kagame anataka DRC iwatambue waasi wa M23 lakini yeye hataki kuwatambua waasi wa kihutu!

Kagame anataka DRC iwatambue waasi wa M23 lakini yeye hataki kuwatambua waasi wa kihutu!

Hio ndio Demokrasia wajameni

Amerika ukiwa kwa waasi/ Militias unatambulika, ukiwa kwa BLM hutambuliki. Inafaa M23 watambulike na wapige kura kuchagua vile wanataka ndio kukomaa Kidemokrasia huko.

"KUNA KUSHINDA NA KUSHINDWA"
HAO M23 Wananuimwa nini na serikali ya Congo hadi wapigane badala ya kupeleka malalamiko un
 
HAO M23 Wananuimwa nini na Congo hadi wapigane badala ya kupeleka malalamiko un
Respectfully, sijaelewa hiyo wananuimwa. Na siezi jichanganya nikakuharibia ulichotaka kusema. Naomba urudie swali lako🙏
 
Kasome kuhusu The Coalition for the Defence of the Republic(CDR) na Radio Télévision Libre des Mille Collines (RTLM) utaelewa kwa kifupi nini kilikuwa kinaendelea Rwanda wakati Genocide inakaribia. Hiyo Genocide iliandaliwa kwa muda mrefu sana, isingekuwa rahisi kwa mauaji ya watu karibia laki nane wauliwe kwa miezi minne tu bila maandalizi ya kupanga ya hali ya juu ya muda mrefu.
Nilishasoma hayo yote. Kwani ni wakati hayo mambo ya cut the 'Tall trees' or 'Kill the cocroaches' yalikuwa yakihimizwa?
 
Moja ya utetezi aliokuja nao Rais Kagame kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na EAC kuhusu kutatua mgogoro wa DRC ni kutaka serikali ya DRC iwatambue kwanza waasi wa M23 ambao wanajumuisha jamii ya walowezi wa kitutsi iliyopo DRC (Banyamlenge), lakini hapo hapo Kagame hataki kabisa kutaka kusikia suala la waasi wa kihutu waliokimbilia DRC nao kutambuliwa kama sehemu ya jamii ya Rwanda yenye haki ya kuongoza na kutawala Rwanda.

Kweli mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
Yeye aliambiwa aongee na waasi kipindi cha JK akaanza kuharabdunia nzima. Dawa ni nchi zinazokizunguka kile kimkoa ziungane zikichape halafu tugawane vipande na kasiwepo tena kama kanchi duniani. Kamtu kanaongoza eneo saw na kata moja huku bongo ila kanajiona kanaongoza Uchina yote 🚮🚮🚮
 
Uganda iko pamoja na Rwanda
 
Kama Marafiki wa karibu zaidi wa kufa na kuzikana, wa kusaidiana kwenye shida na raha.
Vivuruge wa nchi za maziwa makuu ila mmoja kazeeka sasa, mwingine bado ni kichomi tu.

Regime change ikitokea Kigali, Drc mashariki itapumua.
 
Yeye aliambiwa aongee na waasi kipindi cha JK akaanza kuharabdunia nzima. Dawa ni nchi zinazokizunguka kile kimkoa ziungane zikichape halafu tugawane vipande na kasiwepo tena kama kanchi duniani. Kamtu kanaongoza eneo saw na kata moja huku bongo ila kanajiona kanaongoza Uchina yote 🚮🚮🚮
If wishes were horses
 
Waasi wa M23 hawana itikadi za genocide kama walivyo waasi wa FDLR
Wameua zaidi ya watu 3000 ndani ya mwezi mmoja halafu unasema hawana itikadi za genocide. Wewe kwako genocide ni nini?
 
Una hoja mkuu....

Ila.....

Serikali ya DRC inafanya kosa kubwa sana kusema BANYARWANDA-BANYAMULENGE ni raia wa RWANDA na wanatakiwa kurudi kwao....this is a gravious misdemeanor"...

Watu waliohamia kwenu kabla hata ya kupata uhuru wenu na wakakubali kuwa WAKONGOMANI leo unadai warudi kwao ?!!! Khaaaa upuuzi mkubwa huu

#Tanzania kwanza!
Soma vizuri, Hao banyamulenge ni Warwanda waliokimbia vita vya kimbari. Na kufika Congo wakaungana na watusi wenye asili ya Congo. Kumbuka watusi wa Congo, Rwanda na Burundi walikua ni jamii moja ambayo ilikuja kutenganishwa na mipaka tu.So wale watusi waliopo Congo kuna wacongo na warwanda. Sawa na wamasai wa Tz wakimbilie Kenya then Kenya iwachanganye wote wamasai wa Kenya na Tz kama wahamiaji haramu.
 
Back
Top Bottom