Niliwahi kusema RDF ni jeshi Bora ukanda huu wa Afrika ila watu wasio jua mambo ya medani wakakaza makomwe na mapovu na kunitukana.

Sawa hata kaka m23 wanapewa nguvu hii ya kupigana na majeshi zaidi ya 10 na kuteka maeneo mikononi kwa maadui zake ni dhahiri kuwa hawa RDF ni hatari kuliko hadithi za vijiweni.


Rdf/m23 kwa wakati mmoja anapigana na Fardc,Burundi,Sadc,Wazalendo,Wegner, Monusco na makundi mengine zaidi ya 6 lakini wote wanachezea kichapo.


Sadc tayari keshapigwa, huko drc na waasi kuiteka Goma .
 
Hao Sadc si walikuwepo Goma na walikua kwenye izo operation..!! Ilikuaje wakachezea kichapo na kuruhusu M23 kuchukua Mji mzima?
Mwanzo walikua wanalinda AMANI sasa wanaenda KUPIGANA
 
Unajua umbali wa kutoka Goma mpaka Kinshasa..!?
 

..Kagame naye kawazunguka SADC.

..unakumbuka kikosi cha askari wa Rwanda wanaolinda mradi wa LNG wa Msumbiji usishambuliwe na magaidi?

..jiulize kwanini Msumbiji ambaye ni mwanachama wa SADC alikwenda kuomba msaada wa Kijeshi Rwanda badala ya kulindwa na ndugu zake wa SADC.
 
Miaka yote hii wanazurula humo humo DRC wanapishana nao leo hii wanajipya gani?
Ndiyo maana Trump anawashangaa waafrika tujui tunatembeaga vichwa chini miguu juu hata sielewi!
 
Mwanzo walikua wanalinda AMANI sasa wanaenda KUPIGANA
Sasa iyo aman wanayolinda iko wapi? Mbona wanajeshi wameuliwa na wananchi wanakufa? Ni aman gan iyo wanayolinda?

Tukubali tu uyu Kagame jeshi lake limejipanga na kuzoea vita kuliko majeshi yetu haya
 
Usiku wa leo BM zimenyeesha mvua ya rasha rasha hadi mpakani mwa GISSENYI.
Nataka kujua updates za maazimio ya viongozi wa SADC.
Comred MUNANGAGWA na MWAKIBORWA natamani warudi msituni sasa
 
Kuna mdau ameanzisha uzi na kuweka details kuwa kuna wanajeshi wameasi huko Congo na kuwa pamoja na M23.

Ni yale yale kama ya Syria.
 
Aliingia huko South na akamuua adui yake na wauaji wakatoka salama.. Anajiamini anammudu Ramaphosa. Kapandikiza watu wake wa kutosha sana
Nakubaliana na wewe chief. Kagame hatumpendi lakini ana akili sana ya kupigana vita kuliko mtu yeyote Japa Afrika.
Haipendezi kusema ila ukweli uko wazi kwamba jeshi la Rwanda Lina ubora wa hali ya juu kwa kuangalia tu mission wanazoshiriki.

Kwa mgogoro na Rwanda namuona SANDF akidhalilika kwa RDF.

Pale DRC moto anaopeleka Rwanda kwa muungano wa adio zake ni balaa.
Kheri kujenga amani na Rwanda kuliko vita . Hawa jama hawaongei wala kujisifia ila ukiingia anga zao utawajua.
Waulize waganda wanamjua kagame.
Waulize waasi pale Msumbiji wanawaelewa wanyarwanda
 
Nakuunga mkono asilimia 1000 kwani madaraka kupita kiasi hulevya kupita kiasi. Kagame akumbushe kilichompata nduli Idi Amin alipoichokoza na kuichokonoa Tanzania. Awaulize wareno kilichowapata Angola na Msumbiji.
Kumbuka JW wako kule ,kwa muziki huu wa m23 iliyoboreshwa wametumia busara kuwa watazamaji
 
Kinacho nishangaza kuhusu huyu mtwana ni kwamba Yeye anasema hawaungi mkono M23, Ila ananuna akiona nchi jirani wanaisaidia Serikali ya congo.

The only way ya kudeal na huyu mtu, ni huko huko msituni Congo mpaka paeleweke
 
Vita ni teknologia, Rwanda hana ubavu wa kupambana na South Africa. Rwanda hana Air defensive yeyote, ukirusha ata jiwe linaingia na kupiga popote pale. Ni mkwara mbuzi tu
Sidhani kama una uhakika na hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…