Huenda huu ukawa ndio mwisho wa Kagame Regime in Rwanda.
 
Baada ya kuondoa vichwa kama Nyerere na Magufuli na kuongozwa na wanaofikiri kwa matummy na mabutty, unategemea nini? Zama za mchonga mdudu kama Kagame wala asingetingisha mkia wake kabla ya kushikishwa adabu.
Magufuri alikuwa na ukichwa gani?
Chini ya utawala wake si ndo aliridhalilisha jeshi kwa kuli bebesha makorosho?
Chini ya utawala wake mpaka akina Sabaya na akina Makonda walikuwa wana uwezo wa kuamrisha jeshi cha kufanya?
Si ndo kipindi kagame alikuwa anauwa wanajeshi wetu huko kongo na Magufuri alikuwa ana ufyata?
 
Waafrica wapumbavu sana. Mpaka leo bado wanafarakanishwa na ushawishi wa wazungu. Sikumbuki ni lini niliona mabeberu wao kwa wao wanabishana hadharani. Ila hii minyau sasa.🤣🤣🤣
 
PK anajua hulka ya viongozi wengi wa kiafrika hivyo hana shida Wala wasiwasi juu ya matendo na kauli yake,kwa sababu mwafrika ni kiumbe mnafiki.

Huo mgogoro wa Congo niwa muda mrefu sana na njia ya kupata suluhu ni kupitia majadiliano Kati ya waasi na serikali.
 
Kagame anatakiwa kupigwa au kuvamiwa nchini kwake. Siyo tu kuwapigia nchini Congo. Hapo atawasumbua sana.
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame amemuonya Rais Cyril Ramaphosa akisema Kiongozi huyo wa Afrika Kusini amepotosha mazungumzo yao ya Faragha waliofanya na kusema kama Afrika Kusini inataka makabiliano basi Rwanda iko tayari kujibu.

Katika waraka wake mzito alioandika kwenye Mtandao wake wa X, Rais Kagame amesema alifanya mazungumzo mawili wiki hii na mapema jana na Rais Ramaphosa kuhusu hali ya Mashariki mwa DRC, akisema kuwa kile kilichosemwa na maafisa wa Afrika Kusini na Rais Ramaphosa mwenyewe kuhusu mazungumzo yao kwenye vyombo vya habari kimejaa upotoshaji mwingi.

Rais Kagame amesema ikiwa maneno yanaweza kubadilika kiasi hicho kutoka kwenye mazungumzo hadi kwenye tamko la umma, inasema mengi kuhusu jinsi masuala haya muhimu yanavyoshughulikiwa.

Rais Kagame amesema ikiwa Afrika Kusini inataka kuchangia suluhisho la amani huko Mashariki mwa DRC hilo ni jambo jema, lakini haina nafasi ya kuchukua jukumu la mpatanishi au msuluhishi. Na iwapo Afrika Kusini itataka makabiliano, Rwanda iko tayari kujibu hilo.

#KitengeUpdates

 
Last tym TATA MADIBHA MANDELA warned mr PK...., "ukiigusa CONGO utakiona cha mtena kuni"......

Tunataka kiongozi kama MANDELA, jemedari wa vita kama MUNANGAGWA na RT.LT GEN MWAKIBORWA saa 4 asubuhi tutakuwa kigali tunakunywa KAHAWA
 

Majeshi ya Rwanda hayana uwezo wa kuyashinda Majeshi ya Afrika ya Kusini katika medani za kivita ubavu huo Rwanda haina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…