Kaka yangu amechomwa Moto kwa kudhaniwa ni mwizi


Endelea tu na huo utaratibu wako usio rasmi wa kujichukulia sheria mkononi. Siku ikifika, utajuta kuzaliwa. Maana kesi za mauaji, kwa sheria za Nchi yetu; huwa hazina dhamana.

Kupitia hayo maelezo yako, makosa ni ya polisi! Na siyo kila anaye tuhumiwa/kuitiwa mwizi, ni mwizi kweli. Fuata sheria za Nchi aisee. Uhai wa mtu haulinganishwi na kitu chochote kile.
 
Ndo maana nikasema mtoa mada achukulie Kama Ni ajali.

Haina haja kuwalaumu waliomshughulikia maana ndugu yake uyu wkt anakamtwa hakutembea na Cheti na kuwaonyesha kua Ni mgonjwa wa akili washambuliaji wakakikataa .

Hapo lawama ziende kwa waangalizi, pia ichukuliwe Ni bahat mbaya TU[emoji26]
 

Umeshaambiwa huyo ndugu yake alikuwa ana matatizo ya akili! Unategemea atajieleza kama ulivyo wewe? Jaribu kuuvaa uhusika wa mtoa mada.

Siku ndugu yako afanyiwe ukatili kama huo, utajisikiaje kuona baadhi ya watu wana kukejeli?
 
Kwani hao wezi na majambazi,
uhai wa mtu, hao wahalifu huwa wanaulinganishaje wanapokwenda kufanya uhalifu kwa nguvu.

Wanagapi umeskia wameuwawa/kujeruhiwa na wezi, vibaka na majambazi wkt wakitekeleza uhalifu wao?
Au na wao hawana ndugu wenye uchungu?

Ifike mahali tukatae huo UNYONGE,
Ifike mahali tuwe Kama Russia,

huwezi kuahatarisha usalama wangu kwa kujifanya kibaraka na kumkumbatia adui yangu afu ulete visingizio eti UN, unhcr, n.k watanifikiriaje nikimfanyia Hivi jirani yangu[emoji3525].
 
Mzee naona umeandika kwa uchungu wa kuibiwa dukani kwako sio...
Mwaka Jana TU nmepigwa matukio 2 ya uhalifu (moja dukani na jingine goddown), la dukani mlinzi wangu kapigwa Shaba kauwawa palepale.

Mwaka 2008,
Kijana wangu mmoja akipeleka pesa nbc alitekwa na majambazi wakamnyanganya pesa na kwenda kumtelekeza Chamazi

Mwaka 2005,
nmewai fatwa hotel na majambazi, nikajeruhiwa mguu wa kushoto na jambazi na wakachukua pesa wakaondoka .

2000,
Nmefatwa nyumbani na majambazi wakanikosa na kuijeruhi familia yangu wakiilazimisha iseme nilipo.
Alhamdullillah nilishapata tip kwa bodaboda mmoja nikaenda kulala gesti badala ya nyumban usiku ule.

Naanzaje kwamfano kuwaonea huruma wezi[emoji3525]
 
Ngoja yakukute ndugu zako wataleta uzi kama huu. Subiri uingie 18 za raia
Kuna mshikaji wangu aliuwawa kisa kwenda kudai pesa yake, mwenye nyumba akamwitia mwizi na aliuliwa kikatili.
 
We jamaa unatumia nn kufikiri?
Ukitanguliza gadhabu mbele hauwezi tatua lolote,
Ina maana ww unaharalisha kitendo cha walinda amani mtaani mida ya usiku kujichukulia sheria mkononi?
Unaharalisha uhalifu hadharani masta...
Ungekua Ni uhalifu nna imani hata polisi wangelikua Pamoja na mtoa mada,

Sasa Kama polisi walinda usalama wa raia na mali zao wamempuuza mtoa mada unadhani Mimi Ni Nani mpk nimuonee huruma[emoji3525]

Mtoa mada anyooshe maelezo vizur, Hamna huruma ya bure bure nowdays.

Watu tushaumizwa Sana na Hawa wanaojiita vibaka, wezi na majambazi[emoji3525]
 
Hivi unawajua sungusungu wewe? Naona unaongea tu bila facts.
 
Reactions: amu
Kenge huwa hasikii hadi atoke damu masikioni.
Sahii kabisa,
Hizi janja janja za kujifanya Ni mgonjwa wa akili zinatumika Sana skuhizi.

Maana mateja na waathirika wa bangi nao Skuhzi wanaitwa wagonjwa wa akili[emoji3525]
 
Na inawezekana watu walimtumia kufanya uhalifu( hao waliokuwa nae tangu apotee) all in all sababu hayuko sawa, walitakiwa wasimpige kabisa,.
Hapo unalosema linawezekana,
Akatumiwa na Vibaka Kama chambo afu Hali ikishakua mbaya wanaingia mitini wanamuachia msala.

Hujawai sikia zile kesi watoto wa miaka 9-12 wanatumika kuvunja nyumba za watu madirishani, afu wez wanaingia na kufagia?
 
NB:hata Mimi nilikuwa nafurahia mwizi akipokea kipondo na wewe siku ndugu yako akipigwa moto na unajua fika sio mwizi ndio utajua kwanini serikali inakataza raia kujichukulia sheria mkononi
Kwakweli Mimi hata awe Ni mwanangu wa kumzaa.
Kama Ni mwizi wauwe TU, sifugi wezi Mimi.

Hata watoto wangu wanalijua hilo[emoji3525]
 
Loh poleni sana sana.

Down-syndrome ni maradhi ambao wengi wanayo na jamii haijaelimishwa kuhusu hiyo issue.

Nasikitika sana hii tabia ya wananchi kujimilika hasira kali kinyume na sheria. Mtu anaitiwa mwivii watu wanatola mbio kwenda kuua badala hata ya kuhoji nani kaibiwa nini na kidhibiti kipo wapi.

Poleni sana mkuu. Inauma
 
Pole sana mkuu
 
Ha ha ha....
Hzo kesi na wahalifu wangu tuziweke pembeni chief[emoji4]
 
Mkuu umeteleza hapo, mwaka 2000 kwa bodaboda!!!? [emoji848]
 
Mkuu umeteleza hapo, mwaka 2000 kwa bodaboda!!!? [emoji848]
Bodaboda zilikuepo mkuu mbona, kulikua zile pikpik za kukodi zinaitwa CD 125
Sijui Kama unazikumbuka chief, au uljua bado mdg bwashee[emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…