Kaliba ya Ualimu lazima iheshimiwe

Mkuu hawa wanasema ukweli kwamba ualimu ulikua ni wito zamani sio sasa hivi kwa sababu maisha yamebadilika.
mwalimu athaminiwe kwa kulipwa vizuri ili maisha yake yawe mazuri nafikiri mwl akiwa na maisha mazuri ni rahisi sana kuwa inspire watoto wetu huko mashuleni
Ujue ukiwaambia wanafunzi elimu ni ufunguo wa maisha inabidi watoto wakuone hata wewe unaewaambia upo vizuri sio shati, suruali zimepauka.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Dah! Hapo mwishoni nimefarijika sana uliposema Mungu ibariki Tanganyika. Am proud to be Mtanganyika, from Tanga.
 
Kaza hapo hapo, huwezi kubaki kazini Hadi saa 11 tena bila kwenda lunch, halafu bila motisha yoyote....muda wa serikali ukiisha sepa....muhimu umetimiza majukumu yako ya siku.
Kwa mshahara gani hasa wa kujitafutia vidonda vya tumbo? Unajitoa Kwa watoto ambao wao na wazazi wao wanakudharau.....huu ni uzwazwa.
 
Mkuu unamawazo mazuri sana ila anza ukiwa kazini yakitiki kopa wekeza mifugo yako na mashamba then timua. Kuna watu wanamake hela mashambani na hata hawa habari na ajira ila sema mtu ukiajiriwa unahofia kupoteza ajira.
 
Hiyo Iko wazi viongozi wa juu wanaweka vikao Kila siku posho kibaoo wanajibebea, kada zingine akiongeza muda ambao hupo kisheria ana demand malipo na analipwa, kuja kwetu sisi mkuu anataka akutumie to the maximum mfukoni hakuna kitu, Mwalimu aliyenifundisha Niko secondary mpaka Leo Nimekua Mwalimu maisha yake mpaka Leo yako vilevile, kwa kifupi walimu ni daraja la watu kwenda sehemu nyingine wakati huko palepale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…