Kalynda imefunga ofisi zake hapa nchini, viongozi wake hawajulikani walipo

Hatari sana mkuu. Sijui CEO wa ITV kwa sasa ni nani, ili yule mama Mhavile alikuwa anajitahidi sana. Sidhani kama bado yupo pale.
 
Mimi nilimuuliza muhamasishaji mmoja wa huu utapeli kwanini naweka pesa yangu kama malipo yatatokana na mimi kurate hizo bidhaa zao feki!

Sikupewa jibu na muhamasishaji akaninunia baada ya kukataa kujiunga.
 
Kuna jamaa aliweka milion 10 toka mwezi wa 6 akawa anasubiria mwezi huu achukue mpunga wa kutosha akamalizie nyumba yake mara ghafla bin vuu anaona watu waleeee wanatokomea kusikojulikana[emoji38][emoji38][emoji38]
Duh kweli nimeamini kuna watu ni wapumbavu,yaani mtu ana milioni 10 mkononi anashindwa kuizalishia anakwenda kuwapa matapeli
 
Ukivilaumu vyombo vya habari unakosea ndugu,wewe ni mtu mzima mwenye akili timamu unapaswa kuchanganua mambo na kujua baya na zuri.
Vyombo vya habari kazi yao ni kupokea matangazo na kuyatangaza bila ubaguzi,ukipeleka tangazo la pombe watalitangaza,tangazo la sigara watalitangaza wao si kazi yao usiwe mlevi,ukilewa ukaharibikiwa huwezi kwenda kuwalaumu kwa nini mmetangaza pombe halafu mimi nikawa mlevi hiyo ni wewe na akili yako.
Angalau kidogo ungelaumu vyombo vya usalama ingekuwa na mantiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…