Kalynda imefunga ofisi zake hapa nchini, viongozi wake hawajulikani walipo

Kalynda imefunga ofisi zake hapa nchini, viongozi wake hawajulikani walipo

View attachment 2383637

Niliambiwa mimi na huyu mwamba one b kwamba usiingie huko, serikali ina mkono wake huko itawapiga isepe

Nikanyuti sikuingia mara paaaa chali watu washaliwa, sasa ndio nmeamini kabla ya kufanya Jambo tafuta washauri wazuri usikurupuke
Tozo nyingine zimekusanywa na serikali kiana....[emoji4][emoji4][emoji4]
 
Ukivilaumu vyombo vya habari unakosea ndugu,wewe ni mtu mzima mwenye akili timamu unapaswa kuchanganua mambo na kujua baya na zuri.
Vyombo vya habari kazi yao ni kupokea matangazo na kuyatangaza bila ubaguzi,ukipeleka tangazo la pombe watalitangaza,tangazo la sigara watalitangaza wao si kazi yao usiwe mlevi,ukilewa ukaharibikiwa huwezi kwenda kuwalaumu kwa nini mmetangaza pombe halafu mimi nikawa mlevi hiyo ni wewe na akili yako.
Angalau kidogo ungelaumu vyombo vya usalama ingekuwa na mantiki.
ITV hili linawahusu kwa asilimia 100 ni kama yale ya Kigwangala na Qnet. Kuna haja ya watu influential au taasisi influential kua na uwezo wa kufanya due diligence kabla ya kuendorse kitu kwa general public wasiishie tu katika kupokea bahasha.
 
Kwan mkuu ITV walikushikia panga ukaweke pesa zako umo, watu wamekuja na vibali vyote wanataka warushe tangazo lao na wakalipia sasa wao wahasukaje apo na wao wanafanya biashara?
 
Kuna jamaa aliweka milion 10 toka mwezi wa 6 akawa anasubiria mwezi huu achukue mpunga wa kutosha akamalizie nyumba yake mara ghafla bin vuu anaona watu waleeee wanatokomea kusikojulikana[emoji38][emoji38][emoji38]
Huyo ndio kapigwa vizuri sana, aendelee kusubiri atamaliziq tu nyumbani
 
Kwan mkuu ITV walikushikia panga ukaweke pesa zako umo, watu wamekuja na vibali vyote wanataka warushe tangazo lao na wakalipia sasa wao wahasukaje apo na wao wanafanya biashara?
Hawakushika panga ila unajua kwa nini wanahusika sababu ya reputation yao. Unadhani hili Tangazo lingekua Carrymastory linakua na weight kama ya ITV? Jibu ni hapana. Jamii ina imani kubwa sana na ITV na ndio maana hata habari ITV ina aminika zaidi.
 
Nyie viongozi wa KALYNDA popote mlipo,,

Nawaambieni ,,
MUNGU ATAAMUA UGOMVI

Jasho letu haliwezi kwenda bure.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
ITV hili linawahusu kwa asilimia 100 ni kama yale ya Kigwangala na Qnet. Kuna haja ya watu influential au taasisi influential kua na uwezo wa kufanya due diligence kabla ya kuendorse kitu kwa general public wasiishie tu katika kupokea bahasha.
ITV hawana liability yoyote hapo kisheria.

Failure kubwa hapa ni taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yao hasa vyombo vya ulinzi na usalama.

Swali la msingi la wao kujiuliza, ni kwann matatizo haya yamekuwa yakojirudia mara kwa mara?

Anayeathirika pakubwa ni mteja kwa kutokufanya due diligence ya kutosha.

Sasa nikipeleka tangazo langu la msiba ITV, inabd ITV wakafanye due diligence kupata uhakika marehemu kafa?

ITV most likely watafanya due diligence kwenye mambo ambaye yatawaweka kwenye legal ramifications wao kama taasisi.

ITV watafanya nn unadhan pale taasisi inapokuja na genuine documents kutoka relevant authorities? Kuzi-despute?
 
Ndio kitu gani hio[emoji1787][emoji1787]

Another DECI

mtapigwa kwa ponzi schemes hadi lini

1. DECI

2. RIFARO

3. FOREVER LIVING

4. QNET

5. KALYNDA

6.....

Nyingine nyingi zitakuja sababu wapumbavu ni wengi sana .
IMG-20221011-WA0191.jpg
 
Serikali iwajibike. Haiwezekani waruhusiwe kufanya biashara ya pesa bila dhamana.

Wananchi wataelewa serikali ndiyo imewatapeli.

Walisajiriwa brella wakalipa kodi.

Huku mtaani ni vilio tu mpaka huruma.

Nashukuru Mungu sikufanya ujinga huu
mambo mengine mtakuwa mnaipa seriakali kazi ambazo ni za kijinga,iwaze kuwatafutiw madawa na maji safi wananchi wake,ikae inahangaika na watu wenye kukimbilia utajiri bila kufikiria vizuri,bali ni tamaa tu!!Mala ngapi zimeshatolewa tahadhari kwa hizi mambo?!!Acha tu watapeliwe,labda cha kuilaumu serikali ni kuwafanya wananchi wake wawe masikini,kwani ndio wahanga wengi wa michezo hii.
 
ITV hawana liability yoyote hapo kisheria.

Failure kubwa hapa ni taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yao hasa vyombo vya ulinzi na usalama.

Swali la msingi la wao kujiuliza, ni kwann matatizo haya yamekuwa yakojirudia mara kwa mara?

Anayeathirika pakubwa ni mteja kwa kutokufanya due diligence ya kutosha.

Sasa nikipeleka tangazo langu la msiba ITV, inabd ITV wakafanye due diligence kupata uhakika marehemu kafa?

ITV most likely watafanya due diligence kwenye mambo ambaye yatawaweka kwenye legal ramifications wao kama taasisi.

ITV watafanya nn unadhan pale taasisi inapokuja na genuine documents kutoka relevant authorities? Kuzi-despute?
Reputation damage ndio inawahusu hapa.
 
Back
Top Bottom