Kalynda imeondoka na kijiji, Viongozi hawajulikani walipo

Mrejesho huu hapa ameniambia niache unafiki [emoji23]
View attachment 2383167
Kuna mmama mmoja ni mwalimu alikua mwenyekiti wa jumuia yangu naye alinishawishi sana kuingia huko mpaka akaitisha mkutano na mtu alomuingiza kunishawishi jamaa alipoanza kusema ananiunganisha na mimi niwaunge watu watano nikasema hii ni Network Marketing nikaishia kusema sawa mkuu tutawasiliana. Kwa sababu ya heshima niliyonayo kwake niliishia kukaa kimya.

Baada ya kama wiki tatu akanambia ameweka 1M kila siku anapokea 54k nikamwambia hongera. Sasa toka juzi sijaonana naye nasubiri Jmos tutakutana kwenye jumuia nimuulize kama miamala bado inasoma?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 2383171
Jamaa kajianika vizuri mno. Huyu akichukiliwa maelezo ataeleza hao jamaa wapo wapi na pesa zinarudi.

Nimepitia tena akaunt ya Kalynda naona wanafuta posts zao kuondoa ushahidi

I guess unajua hii account haina uhusiano wowote na serikali.

Mshauri wa serikali ni nani exactly (mwenye hiyo acc) maana watendaji wote wa serikali ni washauri wa serikali ikiwemo mawaziri na wabunge.
 
Kwanza green card ni bure. Pili GC ni worldwide. Tatu Kuna watu kadhaa wameshinda GC na wapo USA rn na wengine wapo humu humu JF. Changamoto ya GC ni kwamba ni bahati nasibu Kuna 50,000 slots only kwa waombaji wote worldwide so you can see ambavyo ni mbinde kushinda.
 
Mjini mipango
 
Nusu ya Watanzania ni chini ya Miaka 18

Hesabu inayobakia 35,000,000
Kati yao asilimia 20 ni Wastaafu
Hivyo twabaki na Milioni 28

Kati ya hao Milioni 28 wanaojitambua ni 100,000
Hivyo misukure ni Milioni 27.9
 
Na hata ukishinda kama Bongo huna michongo ya maana na unatoka familia maskini bado consular anaweza kukunyowa Ndio ninapoona hata Wamarekani nao wanazinguwa vile vile na green card rotary yao.
 
Umekosea, ulipaswa kumjuza n kumpa mifano ya dhahiri, huenda angeelewa akaepuka hili.
Una hatia kwenye hili mzee. So hapo unasubiri muonane umcheke ama umpe pole ya kinafiki, ulichukua hatua gani kumsaidia?
 
Haha ukikutana naye mzuge kuwa umeshatafakari vya kutosha unataka kujiunga.
 
Na hata ukishinda kama Bongo huna michongo ya maana na unatoka familia maskini bado consular anaweza kukunyowa Ndio ninapoona hata Wamarekani nao wanazinguwa vile vile na green card rotary yao.

Inabidi uwe kilaza grade A Hadi consular akutolee nje wakati umeshinda. Sijawahi kusikia hiyo ila nawajua watu walioshinda wakiwa vyuoni bongo au kwenye mishe zao tu mtaani wameshinda na Sasa wapo hapa. Sijawahi kusikia mtu kakataliwa baada ya kushinda.
 
Niliwahi kushauri, Tanzania tuwe na mfumo wetu, kura za kuchaguwa Rais zisipigwe kwa kigezo cha Uraia au kutimiza miaka 18, inabidi na sisi tutengeze mfumo wetu wa college vote kama za Marekani ili Rais achaguliwe na wachache na mikoa yenye watu wajinga kama Morogoro na Tabora ipewe nafasi chache zaidi za kura za Urais.
 
Huu ndiyo ukweli...

" DECI, Mr.Kuku......Kylanda...ni mipango ya serikali kukusanya fedha kutoka kwa raia vilaza, wapenda slope.

Hakuna muhusika wa hizo business ambaye atafungwa.

Walio liwa nawashauri wahamie kule kwenye VANILLA...[emoji16][emoji16][emoji16].

1M unapata 1B after 1year...hiyo ndiyo vannila.
 
Umekosea, ulipaswa kumjuza n kumpa mifano ya dhahiri, huenda angeelewa akaepuka hili.
Una hatia kwenye hili mzee. So hapo unasubiri muonane umcheke ama umpe pole ya kinafiki, ulichukua hatua gani kumsaidia?
Mkuu ilikua ni ngumu kufanya hivyo kwa sababu yeye aliniita ili nionane na mtu aliyemhamasisha na huyo mtu ni mdogo wake ambaye kwetu ni kama uncle. Huyo jamaa alikua tayari keshawapa semina walimu kibao na wengi wakiendelea kujiunga. Hivi unamuelemishaje kwa situation kama hiyo? Mimi nilimjibu ngoja niendelee kujipanga tutawasiliana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio mana nasema wajinga ni wengi. Tena kwenye dini ndio kabisa sijui kwann tumekosa maarifa, leo hii you can imagine Masanja na Mc pilipili nao ni mabishop eti wana wafuasi kibao🤣🤣🤣
hapa kwenye dini tuache tu, ila matatizo ya ki afya, kukata tamaa, fedha huwafanya watu wajaribu bahati zao kwenye dini

na badala ya kutatua tatizo wanaongeza tatizo
 
hapa kwenye dini tuache tu, ila matatizo ya ki afya, kukata tamaa, fedha huwafanya watu wajaribu bahati zao kwenye dini

na badala ya kutatua tatizo wanaongeza tatizo
Hivi hata kama kukata tamaa ndio uambiwe kuna nyumba za kudownload? Au kuna pesa za kudownload? Au eti unaweza kudownload gari? Jamani jamani tutumie hata hizi akili ndogo tulizonazo.
 
Na hata ukishinda kama Bongo huna michongo ya maana na unatoka familia maskini bado consular anaweza kukunyowa Ndio ninapoona hata Wamarekani nao wanazinguwa vile vile na green card rotary yao.
Mkuu una changamoto ya kifikra?

Mwanzo ulisema huo ni utapeli, baada ya kuelezewa kidogo imebadili gia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…