Maneno yenu ya kuzua zua mnayodanganya kanisani usiyalete hapa hapa lete maandiko
Toa hilo andiko linalosema Yesu alizaliwa usiku kwenya hori la ng'ombe
Luka 2:8
Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.
Luka 2:9
Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
Luka 2:10
Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
Luka 2:11
maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.
Luka 2:12
Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.
Luka 2:13
Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,
Luka 2:14
Atukuzwe Mungu juu mbinguni, <br>Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.
Luka 2:15
Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.
Luka 2:16
Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.
Luka 2:17
Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto.
Luka 2:18
Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.
Luka 2:20
Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.