kwa uislamu hakuna amani,ukifuatilia uislamu zaidi unakuwa jihad,alafu nimekuuliza Uislamu Kama dini ilianza lini??na ikaletwa na Nani???na Allah anakaaje kisura????
Mbona hata kwenye ukristo kuna Crusade ??
Islam means peace , ni Amani. ilianza lini ni tokea kuumbwa ulimwengu. Amani ililetwa na Mungu mwenyewe.
SIFA ZA MUNGU
(a) Kutoka 33:17-20- Mungu haonekani:
“Bwana akamwambia Mussa nitafanya na neno hili ulilolinena kwa maana umepata neema mbele zangu nami na kujua jina lako, akasema nakusihi unioneshe utukufu wako . Akasema nitapitisha wema wangu wote mbele yako nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili ,nitamrehemu yeye nitakayemrehemu . Kisha akasema , Huwezi kuniona uso wangu , maana mwanadamu hataniona akaishi .
(b) Timotheo (1) 6:16 – Mungu haonekani wala hafi :
“Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribia , Wala hakuna mwanadamu aliyemuona , Heshima na uwezo una yeye hata milele Amina.
(c) Yohana 5:37- Sauti ya Mungu haijasikika:
Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote ,wala sura yake hamkuiona .
(d) Yakobo 1:17- Mungu habadiliki:
“Kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika wala kivuli cha kugeuka geuka”
YESU ALIVYOPACHIKWA UUNGU
(a) Warumi 9:5
“Ambao mababu ni wao ,katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili . Ndiye aliye juu ya mambo yote . Mungu mwenye kuhimidiwa milele Amina.”
(b) Timotheo 3:16
“Na bila shaka siri ya utawa ni kuu, Mungu alidhihirishwa katika mwili , akajulikana kuwa na haki katika roho , Akaonekana na malaika akahubiriwa katika mataifa akaaminiwa katika ulimwengu , Akachukuliwa juu katika utukufu”
(c) Tito 2:13
Tukilitazamia tumaini lenye Baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na mwokozi wetu.
YESU ALIVYOUKANA UUNGU
(a) Luka 18:18
“Tena mtu mkubwa mmoja alimuuliza akasema , mwalimu mwema nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja , naye ndiye Mungu”
(b) Yohana 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma”
(c) Yohana 14:28
“Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia naenda zangu tena naja kwenu kama mngalinipenda mngalifurahi kwasababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni Mkuu kuliko mimi”
UDHAIFU WA YESU KATIKA UUNGU
(a) Matayo 8:22-24 – Yesu alilala usingizi:
“Lakini Yesu akaniambia nifuate wache wafu wazike wafu wao akapanda chomboni ,wanafunzi wake wakamfuata kukawa msuko suko mkuu baharini , hata chombo kikafunikizwa na mawimbi naye alikuwa amelala usingizi “
Rejea Zaburi 121:1-4 Mungu halali
(b) Yesu alikuwa akionekana Rejea Kutoka 33:17 …….Timotheo
(1) 6:16 Mungu haonekani .
(c) Matayo 27:46 Wakristo wanaamini kuwa Yesu anamlilia Mungu
“Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. Na kama saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema Eloi , Eloi lama sabakthani? Yaani Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha”?
(d) Matayo 20:20-23
“Ufalme wako , Yesu akajibu akasema , Hamjui mnaloliomba Je mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi?
Wakamwambia twaweza. Akawaambia mtakinywea kikombe changu, laikini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto sina amri kuwapa , bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.