Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Maisha ndivyo yalivyo kwa waafrika kubishana DINI. Na ndivyo yalivyo kwa wenzetu kuzidi kututawala kifikra kwa hizo hizo Dini..watu kazi hawafanyi ni kukesha makanisani na misikitini kuomba miujiza itokee waki ukemea Umaskini "Umaskini tokaaa".

The issue is, We cannot use prayers to replace our laziness.
Na watu hao hao wanalisha na kusomesha familia zao na si kwamba ni wale ombaomba wa barabarani, sababu za umasikini wa afrika huwa kila mtu anaongea lake mara utasikia waafrika ni masikini kwa sababu ya kupenda sana ngono(japo hatuwazidi wazungu) mwengine atakwambia ni kutokana na watu kwenda kanisani au misikitini, sasa najiuliza waarabu mbona wanaenda msikitini na wameshika sana dini ila mbona wametuzidi kimaisha? Ni kwamba wazungu wameanza kuwa matajiri baada ya kuacha kwenda kanisani?
 
Mpaka Sasa umeshindwa kuthibitisha
Kwa kuweka original na iliyotiwa mikono
Kwa hiyo madai Yako tunayatupa Kwenye dustbin

Sasa Rudi ujibu hoja za mada
Iliyotiwa mikono si hayo maandiko yaliyo kwenye hicho kitabu cha biblia au unataka tuanze kuonesha jinsi biblia ilivyotiwa mikono?
 
kwa uislamu hakuna amani,ukifuatilia uislamu zaidi unakuwa jihad,alafu nimekuuliza Uislamu Kama dini ilianza lini??na ikaletwa na Nani???na Allah anakaaje kisura????

Mbona hata kwenye ukristo kuna Crusade ??

Islam means peace , ni Amani. ilianza lini ni tokea kuumbwa ulimwengu. Amani ililetwa na Mungu mwenyewe.

SIFA ZA MUNGU

(a) Kutoka 33:17-20- Mungu haonekani:

“Bwana akamwambia Mussa nitafanya na neno hili ulilolinena kwa maana umepata neema mbele zangu nami na kujua jina lako, akasema nakusihi unioneshe utukufu wako . Akasema nitapitisha wema wangu wote mbele yako nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili ,nitamrehemu yeye nitakayemrehemu . Kisha akasema , Huwezi kuniona uso wangu , maana mwanadamu hataniona akaishi .

(b) Timotheo (1) 6:16 – Mungu haonekani wala hafi :

“Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribia , Wala hakuna mwanadamu aliyemuona , Heshima na uwezo una yeye hata milele Amina.

(c) Yohana 5:37- Sauti ya Mungu haijasikika:

Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote ,wala sura yake hamkuiona .
(d) Yakobo 1:17- Mungu habadiliki:

“Kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika wala kivuli cha kugeuka geuka”

YESU ALIVYOPACHIKWA UUNGU

(a) Warumi 9:5
“Ambao mababu ni wao ,katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili . Ndiye aliye juu ya mambo yote . Mungu mwenye kuhimidiwa milele Amina.”

(b) Timotheo 3:16
“Na bila shaka siri ya utawa ni kuu, Mungu alidhihirishwa katika mwili , akajulikana kuwa na haki katika roho , Akaonekana na malaika akahubiriwa katika mataifa akaaminiwa katika ulimwengu , Akachukuliwa juu katika utukufu”

(c) Tito 2:13
Tukilitazamia tumaini lenye Baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na mwokozi wetu.
YESU ALIVYOUKANA UUNGU

(a) Luka 18:18
“Tena mtu mkubwa mmoja alimuuliza akasema , mwalimu mwema nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja , naye ndiye Mungu”

(b) Yohana 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma”

(c) Yohana 14:28
“Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia naenda zangu tena naja kwenu kama mngalinipenda mngalifurahi kwasababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni Mkuu kuliko mimi”

UDHAIFU WA YESU KATIKA UUNGU

(a) Matayo 8:22-24 – Yesu alilala usingizi:

“Lakini Yesu akaniambia nifuate wache wafu wazike wafu wao akapanda chomboni ,wanafunzi wake wakamfuata kukawa msuko suko mkuu baharini , hata chombo kikafunikizwa na mawimbi naye alikuwa amelala usingizi “

Rejea Zaburi 121:1-4 Mungu halali

(b) Yesu alikuwa akionekana Rejea Kutoka 33:17 …….Timotheo

(1) 6:16 Mungu haonekani .

(c) Matayo 27:46 Wakristo wanaamini kuwa Yesu anamlilia Mungu

“Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. Na kama saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema Eloi , Eloi lama sabakthani? Yaani Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha”?
(d) Matayo 20:20-23

“Ufalme wako , Yesu akajibu akasema , Hamjui mnaloliomba Je mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi?
Wakamwambia twaweza. Akawaambia mtakinywea kikombe changu, laikini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto sina amri kuwapa , bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.
 
Kutoka 20:11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Surah Al-A'araf Ayah 54

إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُغۡشِي ٱلَّيۡلَ ٱلنَّهَارَ يَطۡلُبُهُۥ حَثِيثٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ وَٱلنُّجُومَ مُسَخَّرَٰتِۢ بِأَمۡرِهِۦٓۗ أَلَا لَهُ ٱلۡخَلۡقُ وَٱلۡأَمۡرُۗ تَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.

Mungu wako anayestarehe weekend mbona hayumo ??
 
Mahakamani hoja zilizowasilishwa unazikumbuka lakini?

Moja ya hoja ni hizi;
1. Quran Kwa sehemu kubwa imejawa na hearsay kuliko Biblia
2. Quran imefanya Plagiarism na Forgery kutoka kwenye Biblia.
3. Quran haina mpangilio wa maana na wenye kueleweka unaoelezea matukio ya tawala za kidunia wakati Biblia ijayo.

4. Quran imeandikwa na Mtu mmoja ambaye anaelezea matukio ambayo hakuwepo na mazingira asiyoyajua.
Wakati Biblia inamaandiko yaliyoandikwa na manabii na mitume wengi katika matukio wanauoyajua na walioyashuhudia na Maeneo yalipotokea waliishi.

Kati ya hizo hoja kuna yoyote humu Kati yenu mawakili WA Quran mmepangua hoja hata Moja?
1)Yote yaliyokwenye Qur'an ni kwamba yamezungumzwa na Mungu mwenyewe kupitia kwa Muhammad na si kwamba Muhammad alikuwa akisimulia mambo aliyoyasikia kwa watu au kueleza kile anachokijua yeye, hivyo Qur'an ni maneno ya Mungu moja kwa moja kupitia kwa mtume wake Muhammad.
 
Kwa hiyo hata wakina Mwamposa tukubali wanaongea na Mungu si ndio?
 
Mahakamani hoja zilizowasilishwa unazikumbuka lakini?

Moja ya hoja ni hizi;
1. Quran Kwa sehemu kubwa imejawa na hearsay kuliko Biblia
2. Quran imefanya Plagiarism na Forgery kutoka kwenye Biblia.
3. Quran haina mpangilio wa maana na wenye kueleweka unaoelezea matukio ya tawala za kidunia wakati Biblia ijayo.

4. Quran imeandikwa na Mtu mmoja ambaye anaelezea matukio ambayo hakuwepo na mazingira asiyoyajua.
Wakati Biblia inamaandiko yaliyoandikwa na manabii na mitume wengi katika matukio wanauoyajua na walioyashuhudia na Maeneo yalipotokea waliishi.

Kati ya hizo hoja kuna yoyote humu Kati yenu mawakili WA Quran mmepangua hoja hata Moja?
2) Hayo madai unayathibitisha vp? Kwa sababu Qur'an inajieleza kwamba kila kilichomo humo kwenye Qur'an ni maneno ya Mungu mwenyewe na ndio Mungu wa vitabu vya Torat,Zaburi,Injili pamoja na kitabu cha mwisho cha Qur'an.
Sasa biblia ni kitabu ambacho watu walikaa na kuamua kukusanya maandiko mbalimbali wakachagua yapi yawekwe na yapi yasiwekwe wakaongeza na maandishi ya watu wengine kama barua za Paulo, hicho ndio kitabu cha biblia ni tofauti na Qur'an.
 
Mimi nikiandika kitabu nikakiita maneno ya Mungu utakubali?
Maneno ya Mungu yanabeba detail zote za muhimu historical na yanayokuja/kinabii.

Sasa Kwa upande wa Historical Quran ndio imeshindwa vibaya, ni akheri ingesema wazi kuwa inanukuu Kwa ajili ya Waarabu Kwa sababu visa vya Wayahudi havikuwa vinasomwa na jamii zingine za watu.
Kila jamii ilikuwa na Dini zake
 
Kwa hiyo hata wakina Mwamposa tukubali wanaongea na Mungu si ndio?
Ni wewe sasa kuamua kukubali jambo hilo au usikubali, maana hata kwenye hiyo biblia kunaelezwa kwamba Musa aliongea na Mungu hivyo ni imani yako kuamua kukubali kwamba ni kweli Musa aliongea na Mungu ama si kweli, Musa alipewa kweli amri kumi na Mungu au si kweli ni imani yako.
 
Kwa hiyo Kwa Uelewa wako kila alichoandika Musa aliambiwa na Mungu?

Hapa tunajadili mambo Kwa kutumia Akili.
Yapo mambo Musa ambayo aliandika Kwa kufuata Oral tradition stories kutoka Kwa wazazi wake na kutoka Kwa jamii yake.
Na yapo aliyoambiwa na Mungu.

Kwa mfano kisa cha Adamu na Hawa, hiyo simulizi aliikuta na sio kwamba alisimuliwa na mungu.

Ndio maana nikakuambia, Biblia pia inahearsay ingawaje sio nyingi kama za kwenye Quran.

Usidhani nipo hapa kuikandamiza Quran na kuipaisha Biblia.
Hivyo vyote vitabu ninavisoma,

Hapa ninachojadili ni ukweli
 
Na watu hao hao wanalisha na kusomesha familia zao na si kwamba ni wale ombaomba wa barabarani, sababu za umasikini wa afrika huwa kila mtu anaongea lake mara utasikia waafrika ni masikini kwa sababu ya kupenda sana ngono(japo hatuwazidi wazungu) mwengine atakwambia ni kutokana na watu kwenda kanisani au misikitini, sasa najiuliza waarabu mbona wanaenda msikitini na wameshika sana dini ila mbona wametuzidi kimaisha? Ni kwamba wazungu wameanza kuwa matajiri baada ya kuacha kwenda kanisani?
Kasome vizuri historia dini zililetwa kipumbaza watu!!!!
 
Mimi nikiandika kitabu nikakiita maneno ya Mungu utakubali?
Maneno ya Mungu yanabeba detail zote za muhimu historical na yanayokuja/kinabii.

Sasa Kwa upande wa Historical Quran ndio imeshindwa vibaya, ni akheri ingesema wazi kuwa inanukuu Kwa ajili ya Waarabu Kwa sababu visa vya Wayahudi havikuwa vinasomwa na jamii zingine za watu.
Kila jamii ilikuwa na Dini zake
Kwanza siku zote Qur'an huwa inatoa nafasi kuichallange kama unaona yaliyomo si maneno ya Mungu bali ya watu na unaweza kuonesha makosa humo au kuweza kujaribu kubuni aya kama za Qur'an, na Qur'an ina mambo yake yenye kuthibitisha kuwa ni kweli ni maneno ya Mungu na si vinginevyo.

Sasa biblia ni mkusanyiko wa maandiko ndio maana nilisema biblia kama biblia haikufaa kulinganishwa na Qur'an.
 
Biblia na Quraan zingefikishwa Mahakamani na Hakimu angekuwa Kiranga wa jf

Ningehudhuria kikao hicho😆
 
Kwanza siku zote Qur'an huwa inatoa nafasi kuichallange kama unaona yaliyomo si maneno ya Mungu bali ya watu na unaweza kuonesha makosa humo au kuweza kujaribu kubuni aya kama za Qur'an, na Qur'an ina mambo yake yenye kuthibitisha kuwa ni kweli ni maneno ya Mungu na si vinginevyo.

Sasa biblia ni mkusanyiko wa maandiko ndio maana nilisema biblia kama biblia haikufaa kulinganishwa na Qur'an.

Nani kasema Quran sio Maneno ya Mungu?
Quran imenukuu maneno ya Biblia na kuyafanyia plagiarism na forgery ili yawe katika muktadha wa kiarabu
 
Iliyotiwa mikono si hayo maandiko yaliyo kwenye hicho kitabu cha biblia au unataka tuanze kuonesha jinsi biblia ilivyotiwa mikono?
Unatakiwa uwe na nakala Yako ambayo haijatiwa mikono tulinganishe na hii ilitiwa mikono

Kinyume Cha apo unajifurahisha tu
 
Nani kasema Quran sio Maneno ya Mungu?
Quran imenukuu maneno ya Biblia na kuyafanyia plagiarism na forgery ili yawe katika muktadha wa kiarabu

Hujaleta hata aya moja kuthibitisha maneno yako , zaidi ya kutuletea mungu wako aliyestarehe weekend , labda akinywa safari na nyama choma 😛
 
Back
Top Bottom