Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Kiroja Muhammadi hakutahiriwa na hayupo katika(nasaba) asili ya koo za Nabii Ibrahimu.SIFA ZA MUNGU
(a) Kutoka 33:17-20- Mungu haonekani:
“Bwana akamwambia Mussa nitafanya na neno hili ulilolinena kwa maana umepata neema mbele zangu nami na kujua jina lako, akasema nakusihi unioneshe utukufu wako . Akasema nitapitisha wema wangu wote mbele yako nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili ,nitamrehemu yeye nitakayemrehemu . Kisha akasema , Huwezi kuniona uso wangu , maana mwanadamu hataniona akaishi .
(b) Timotheo (1) 6:16 – Mungu haonekani wala hafi :
“Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribia , Wala hakuna mwanadamu aliyemuona , Heshima na uwezo una yeye hata milele Amina.
(c) Yohana 5:37- Sauti ya Mungu haijasikika:
Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote ,wala sura yake hamkuiona .
(d) Yakobo 1:17- Mungu habadiliki:
“Kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika wala kivuli cha kugeuka geuka”
YESU ALIVYOPACHIKWA UUNGU
(a) Warumi 9:5
“Ambao mababu ni wao ,katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili . Ndiye aliye juu ya mambo yote . Mungu mwenye kuhimidiwa milele Amina.”
(b) Timotheo 3:16
“Na bila shaka siri ya utawa ni kuu, Mungu alidhihirishwa katika mwili , akajulikana kuwa na haki katika roho , Akaonekana na malaika akahubiriwa katika mataifa akaaminiwa katika ulimwengu , Akachukuliwa juu katika utukufu”
(c) Tito 2:13
Tukilitazamia tumaini lenye Baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na mwokozi wetu.
YESU ALIVYOUKANA UUNGU
(a) Luka 18:18
“Tena mtu mkubwa mmoja alimuuliza akasema , mwalimu mwema nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja , naye ndiye Mungu”
(b) Yohana 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma”
(c) Yohana 14:28
“Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia naenda zangu tena naja kwenu kama mngalinipenda mngalifurahi kwasababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni Mkuu kuliko mimi”
Mwanzo 17:7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Mwanzo 17:10
Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.
Mwanzo 17:13
Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.