Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #641
Nani alikwambia Mungu ni Cheo ? Unajua maana ya jina na maana ya Mungu na maana ya Cheo ?
Mungu ni Cheo
Unaelimu yoyote walau ya Kidato cha nne?
Kama unayo nafikiri ukisoma Aina ya maneno, ukakuta Aina iitwayo Nomino, kwenye nomino kuna Aina zake nyingi tuu.
KAZI ya nomino ni kutambulisha mtu, kitu, mahali au Jambo na kulitofautisha na jingine/wengie.
Mfano ukisema neno Rais umetaja Cheo cha mtu lakini mtu hatajui unamzungumzia Rais yupi, hata mahakamani wanataka Personal name au kingereza kinakuchanganya inaitwa nomini ya pekee,
Jina Mungu sio nomini ya pekee hivyo haimtambulishi ni mungu yupi.
Kwani kila mungu anajina lake kulingana na jamii husika. Kama ilivyo kila jamii ina Rais au Mfalme wake mwenye jina.
Ndio maana nikakuambia mahakamani Quran haiwezi kutoboa maana hata haitambui kuwa Neno Mungu sio personal name Bali ni Cheo.
Na kamwe huwezi shtakiwa Kwa kumtukana Mungu kama alivyofanya Afande Sele Ila unaweza kushtakiwa endapo utataja jina la huyo Mungu.
Mungu aliyemtokea Ibrahimu, isaka, na Yakobo anaitwa Yehova ndivyo alivyojitambulisha,
Kutoka 6:2
Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;
Kutoka 6:3
nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Unaweza kufuatilia Historia ya Yehova hata kihistoria.
Wakati mungu aliyejitokeza Kwa Muhammad person name yake ni Allah.
Pia kihistoria unaweza fuatilia CV ya Allah maana alikuwepo na alikuwa anaabudiwa na Waarabu hapo makka hata kabla Muhammad hajazaliwa, ni Mungu wa waarabu wa kabila la Kurdi.
Sasa sijui wapi huelewi.
Kwa mfano mtu akisema Baba wewe utajua Baba anayetajwa ni yupi?
Mkiambiwa muende shule mnaona watu hamnazo. Sasa mnahangaika Kwa vitu vidogo.
Yaani hujui God/Mungu/Eloi/ mrungu/ ni Cheo Kama Baba/Father/papa/ Tata?