Kila siku nawaambia laiti kama mngekuwa mnahakiki maandiko yenu. Asingesalia Mkristo hata mmoja.
MAJIBU KWA WAISLAMU
Yeremia 8:8
MWASEMAJE, SISI TUNA AKILI, NA TORATI YA BWANA TUNAYO PAMOJA NASI? LAKINI, TAZAMA, KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA KUWA UONGO.
Hili ni moja la andiko ambalo waislamu wamekuwa wakilitumia kupotosha ukweli wa torati ya YEHOVA aliyompa Nabii Musa, kwakusema kuwa torati hiyo haifai kwani imetiwa mikono.
SWALI
Je! ni kweli andiko hilo linamaana kuwa torati ya Bwana aliyompa nabii Musa imetiwa mikono.
JIBU
Hapana, andiko hilo la Yeremia 8:8, halimaanishi kuwa torati ya YEHOVA imetiwa mikono, bali kunamakosa ya kiusomaji kwa wale wapinzani wa Biblia ambao husoma maandiko nusunusu ilikupotosha maana halisi ya andiko hilo.
TUICHAMBUE AYA YA ANDIKO HILI.
1) Mwasemaje sisi tunaakili, NA TORATI YA BWANA TUNAYOPAMOJA NASI.
Kulikuwa na wapinzani wa torati ya Bwana ambao walikuwa wakitaka kuipotosha torati ya Bwana kwa kuwafundisha watu kinyume na torati inavyoelekeza ili torati ya Bwana ionekane ya uongo. Ndipo nabii Yeremia anawaambia wapinzani hao akisema;
[emoji116][emoji116]
"MWASEMAJE SISI TUNAAKILI (Kuwaambia wapinzani hao wa torati, kama walivyokuwa wakijinadi kuwa wao wanaakili), NATORATI YA BWANA TUNAYOPAMOJA NASI (wakati torati ya Bwana wanayo wao manabii wamehiifadhi sehemu salama, nabii Yeremia ameitunza).
NABII YEREMIA ANAWAAMBIA WAPINZANI HAO KUWA, HAWAWEZI KUIPOTOSHA TORATI YA BWANA, KWANI TORATI YA BWANA WANAYOWAO MANABII WAMEITUNZA SEHEMU SALAMA.
ANDIKO LINALOFUATA
3)lakini tazama, KALAMU yenye uongo ya Waandishi IMEIFANYA kuwa uongo.
KALAMU kibiblia maana yake ni ULIMI.
[emoji116][emoji116]
Zaburi 45:1
Moyo wangu umefurika kwa neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme; ULIMI WANGU NI KALAMU YA MWANDISHI MSTADI.
KALAMU YA WAANDISHI NI ULIMI, KIBIBLIA HAPO KALAMU MAANA YAKE NI ULIMI.
*Lakini tazama KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI [emoji118]hapo akiwa na maana ya kuwa, wapinzani hao walikuwa wakifundisha kinyume na maagizo ya torati. Mungu katika torati kasema hivi, na hao wapinzani wa torati wao wanafundisha hivi, kinyume na torati.
KIPANDE KINACHOFUATIA;
*Kalamu yenye uongo ya Waandishi, IMEIFANYA kuwa uongo.
MKTADHA WA NENO KUIFANYA.
Hapa haina maana kuwa, torati ya Bwana ni kweli kuwa niya uongo. Neno hili KUIFANYA hata katika maisha yetu ya kilasiku sisi wanadamu tunalitumia huku likiwa halina maana kama lilivyokuwa neno KUIFANYA, kuwa tayari kitu au jambo hilo kuwa ndivyo lilivyo.
MFANO 1
Unapomwambia mwenzako; Unanifanya Mimi kuwa mjinga. Je! nitayari kuwa wewe ni mjinga, Hapana wewe sio mjinga bali kuna mambo ambayo mwenzako kakufanyia ambayo yanalenga kukuchafua wewe, ndio maana ukamwambia, "UNANIFANYA MIMI KUWA MJINGA" huku ukweli ukibaki kuwa wewe sio mjinga.
MFANO 2
Qur'an 15:91(tafsiri ya Sheikh Al-Farsy)
"Ambao WAMEIFANYA Qur'an kuwa ni MKUSANYIKO WA UONGO"
Hapo limetumika neno "WAMEIFANYA", ambapo nisawa na neno IMEIFANYA kule kwenye Yeremia 8:8.
Swali Kwako Muislamu
Je! tukisema Qur'an unayoiamini ni mkusanyiko wa uongo kwasababu limetumika neno WAMEIFANYA ambalo ni sawa na neno IMEIFANYA, Je! utakubali kuwa Qur'an niya uongo kwa hoja hiyo?
Nabii Yeremia anaposema, kuifanya kuwa uongo haina maana kuwa torati imetiwa mikono(imepotoshwa), bali wapinzani wa torati ya Bwana kuna mambo ambayo walikuwa wanafanya yanayoenda kinyume na maagizo ya torati ilitorati ya Bwana ionekane niyauongo ilihali siyo ya uongo, bali yenyewe ilikuwa mikononi mwa manabii imehifadhiwa sehemu salama. Ndio maana nabii Yeremia anawaambia watu hao;Kuwa [emoji116][emoji116]
MWASEMAJE SISI TUNAAKILI (Nabii Yeremia kuwaambia watu hao wapinzani wa torati ya YEHOVA aliyompa Nabii Musa), NATORATI YA BWANA TUNAYOPAMOJA NASI ( Wakati torati ya Bwana tunayo sisi manabii tumeitunza sehemu salama kabisa). Ukienda aya inayofuata, aya ya 9 utaelewa zaidi, Nabii Yeremia anawaambia watu hao, anasema;
[emoji116][emoji116]
Yeremia 8:9
Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, WAMELIKATAA NENO LA BWANA, WANA AKILI GANI NDANI YAO?
Tunaona hapo aya ya 9, kutoka hiyo aya ya 8, jinsi nabii Yeremia anavyowaambia watu hao kwa kuwauliza. Wanaakili gani ndani yao, japo wanajifanya wanahekima, anawaambia, wamefadhaika, wameshikwa na shetani kwa kulikataa neno la Bwana, yaani hiyo torati ya Bwana ambayo ilikuwa mikononi mwa manabii imeifadhiwa sehemu salama kabisa, ndio maana anawaambia, "MNAAKILI GANI NDANI YENU, MAANA MMELIKATAA NENO LA BWANA.
Andiko hilo la Yeremia 8:8, halimaanishi kwamba torati imetiwa mikono kama tulivyoona bali kunamakosa ya kiusomaji kwa wapinzani wa Biblia ambao wamekuwa wakisoma maandiko nusunusu yaani vipande vipande ili kupotosha maana halisi ya andiko hilo, na sio andiko hilo tu, yapo maandiko mengi ambayo waislamu wamekuwa wakiyapotosha kwa kusoma maandiko hayo nusunusu, yaani vipande vipande ili kupotosha maana halisi ya maandiko hayo.
QUR'AN YATHIBITISHA UKWELI KUWA TORATI YA MUNGU ANAYEITWA YEHOVA HAIJATIWA MIKONO.
[emoji116][emoji116][emoji116]
Biblia ilitangulia kabla ya Qur'an, baada ya kupita zaidi ya MIAKA MIASITA(600), Ndipo ilipokuja Qur'an, nayo ilipokuja ikathibitisha ukweli kuwa Torati hiyo ya MUNGU YEHOVA haijatiwa mikono.
[emoji116][emoji116][emoji116]
Qur'an 45:16
Na hakika tuliwapa Wana wa Israili KITABU na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote.
Qur'an 40:53
Na kwa hakika tulimpa Musa UWONGOFU, na tukawarithisha Wana wa Israili KITABU,
Qur'an 28:43
Na bila shaka tulimpa Musa KITABU baada ya kuziangamiza uma za kwanza (zilizopita), kiwe kifumbua macho cha watu (kiwaangazie) na kiwe uwongofu, na rehema, ili wapate kukumbuka.
Qur'an 2:53
Na (kumbuka) Tulipompa Musa KITABU (KILICHOKUSANYA KILA YANAYOITAJIWA) na cha kupambanua baina ya yaliyo ya haki na yasiyokuwa ya haki ili mpate kuongoka.
Qur'an imeweka bayana kuwa, torati ya Nabii Musa ilitoka kwa Mungu na wala haijatiwa mikono, tena Qur'an inasema torati hiyo inapambanua mema na mabaya.
WAISLAMU ACHENI KUSOMA MAANDIKO NUSUNUSU ILI KUPOTOSHA MAANA HALISI YA MAANDIKO.