Kwa hiyo umekosa ushahidi? Basi Upo kwenye upotoshaji.
Wewe unauhakika Gani kama mungu aliwaagiza watu wake waandike vitabu.
Na kwanini mungu achague watu Fulani ndio Tu 😂 waandike vitabu, wakati kwenye hivyo vitabu vinasema mungu ni wawote.
Na ukicheki baadhi ya waandishi walikuwa na historia mbaya kama za ujambazi, wauwaji, ndio waje kuwa waandishi wa vitabu vya Dini.
Yan vitabu vya Dini vimeandikwa na majambazi, wauwaji.
Ameshakuwa mateka wa Dini, hatumii akili Tena kufikiri,anaogopa atachomwa Moto wa milele
Kama nitachukulia wewe ni mtu unayeamini kuhusu uwepo wa Mungu na unaamini pia katika sayansi na historia, labda hivi ni baadhi ya vitu ambavyo naweza kukuonesha kama Ushahidi wa Biblia kuwa ni maandiko matakatifu ya Mungu. (Hapa ninakiri imenibidi niingie online kutafuta sources zitakazonisaidia kunikumbusha kirahisi au zingine pia kuwa mpya kwangu lakini zitafaa kwa wewe na wengine kuziona)
1. Uvumbuzi wa kisayansi
Yako mambo yalioandikwa katika Biblia miaka mingi sana kabla ya uvumbuzi wa ukweli wake au matumizi yake. Mfano;
Ukweli kuhusu dunia kuelea yenyewe bila kushikiliwa na kitu.
Ayubu 26:7 “Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.”
Mwanadamu amefahamu ukweli huu mwaka 1650 kupitia sayansi lakini hayo maandiko yamekuwepo miaka mingi sana kabla ya ugunduzi huu.
Kutajwa kwa umbile la dunia kwa mfano wa duara
Isaya 40:22 “Yeye ndiye anayeketi juu ya
duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;”
Neno duara lililotumika hapo lina indicate kitu ambacho kina spherical shape sio kitu ambacho ni flat au mraba
Mtu wa kale kuamini hivi inasemekana ni Aristotle aliyeishi miaka 384 mpaka 322 BC. Lakini nabii Isaya alitumiwa na Mungu kuandika kuhusu ukweli huu around 600 BC.
Mithali 8:27 “Alipozithibitisha mbingu nalikuwako; Alipopiga
duara katika uso wa bahari;”
Kutajwa kwa Bahari kwamba ina mikondo yake
Zaburi 8:8 “Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho
njia za baharini.”
Ni mpaka around karne ya 17 ndo sayansi ikagundua kitu kinachoitwa ocean currents.
Ustaarabu wa kunawa kwa maji tiririka na kuweka wagonjwa karantini
Walawi 15:13 “Na huyo aliye na kisonono atakapotakaswa na kisonono chake, atajihesabia siku saba kwa kutakaswa kwake, naye atazifua nguo zake; naye ataoga mwili wake
katika maji ya mtoni, naye atakuwa safi.”
Walawi 13:46 “Siku zote ambazo pigo li ndani yake, yeye atakuwa mwenye unajisi; yeye yu najisi;
atakaa peke yake; makazi yake yatakuwa nje ya marago.”
-- Hayo mambo unaweza kuona ya kawaida lakini ugunduzi wa hizi njia wala haukutokea miaka mingi sana kutokea leo na kutokufahamika kwa njia hizi kumesababisha mamilioni ya watu kufa
(hasa nchi za Ulaya ambako rekodi zipo lakini waisraeli wakiwa taifa changa kabisa katika miaka ya kale walipewa hizi mbinu kama maagizo na yaliwasaidia kuepuka na kuambukizana na magonjwa na baadaye maafa)
Hapa nimechagua mambo machache ya kisayansi kati ya mengi ili kuthibitisha kuwa isingekuwa akili ya binadamu kuweza kuandika mambo hayo ambayo sayansi ya ulimwengu imekuja kuyathibitisha mamia ya miaka baadaye.
2. Kutimia kwa unabii wa Biblia.
Hapa ndo naweza kuandika kitabu kingine kabisa, maana kuna mambo makubwa zaidi ya 1000 ambayo Biblia imeyatabiri na mpaka sasa yametimia, mengine yametimia katika kipindi hicho hicho cha Biblia na mengine yametimia baada ya kuandikwa kitabu cha mwisho cha Biblia. Sasa hapa naomba nisiandike mistari ya Biblia ila chukua muda kufanya utafiti mwenyewe.
3. Ushahidi wa miujiza iliyotajwa na Biblia
Mifano michache:
1) Ushahidi wa kuzama baharini kwa magari ya wanajeshi wa kimisri katika safari ya waisraeli (check for yourself from online sources, lots of documentaries are available)
2) Kufufuka kwa Yesu -- mtu ambaye kaburi lake lililindwa na utawala hodari na maaskari shujaa na kwa amri ya mtawala lakini walishindwa kuzuia kufufuka kwake. Kaburi lake lipo mpaka leo na halina mwili wa Yesu.
Naombeni niishie hapa kwanza, mambo mengi mtu unaweza kufanya utafiti binafsi na ukathibitisha hayo niliyoandika kama kweli una nia ya kutaka kujua na sio tu kubeza bila hoja