Kama Biblia ni kitabu cha kutungwa, nani alikitunga na chanzo na kusudio lake ni nini?

Kama Biblia ni kitabu cha kutungwa, nani alikitunga na chanzo na kusudio lake ni nini?

Wewe Una ushahidi wowote kwamba mungu aliwatuma watu ,mitume , wanafunzi wa yesu waandike Bible?
Kwenye Biblia yako maeneo kadha wa kadha ambayo Mungu aliwaagiza watu wake waandike, sijui wewe unawezaje ku validate ushahidi huo kwa sababu Mungu ni Roho, na mambo ya Mungu ni ya kiimani zaidi.
 
Siviamini coz vina contradiction, makosa kibao, uongo mwingi, upotoshaji wakushangaza,

Vitabu vilivyo andikwa na mungu haviwezi kuwa na mapungufu Haya👆.

Hivi vitabu vimeandikwa na watu waliokuwa na uwezo wa elimu ya psychology
Ungekua umewahi kusoma Biblia angalau kidogo tu, ungejua kutofautisha "mungu" na "Mungu".
 
Ungekua umewahi kusoma Biblia angalau kidogo tu, ungejua kutofautisha "mungu" na "Mungu".
Haya ukiandika mungu AU Mungu, MUNGU, unakuwa umepata faida Gani? Kwani ukiandika Kwa herufi kubwa ndio Tabia nzuri, binadamu anajengwa na matendo yake mwenyewe.
Mkuu Una haja ya kujitambua wewe mwenyewe kwanza

Uwoga wenu ndio umaskini wenu
 
Kwenye Biblia yako maeneo kadha wa kadha ambayo Mungu aliwaagiza watu wake waandike, sijui wewe unawezaje ku validate ushahidi huo kwa sababu Mungu ni Roho, na mambo ya Mungu ni ya kiimani zaidi.
Kwa hiyo umekosa ushahidi? Basi Upo kwenye upotoshaji.

Wewe unauhakika Gani kama mungu aliwaagiza watu wake waandike vitabu.

Na kwanini mungu achague watu Fulani ndio Tu 😂 waandike vitabu, wakati kwenye hivyo vitabu vinasema mungu ni wawote.

Na ukicheki baadhi ya waandishi walikuwa na historia mbaya kama za ujambazi, wauwaji, ndio waje kuwa waandishi wa vitabu vya Dini.

Yan vitabu vya Dini vimeandikwa na majambazi, wauwaji.
 
BINAFSI NINAPO SANA BIBLIA KWA MAMBO MENGI MNO
.

HAPA NITAORODHESHA MACHACHE TU.
1. NGUVU YA JINA LA YESU.

2. DAMU YA YESU.

3. MIUJIZA YA ISLAEL NA WANA WA ISLAEL.

4. KAFARA YA DAMU, MNYAMA.

5. UNABII MKUBWA NA MZITO WA VITABU VYA KINABII.

6. KUTABILIWA TAREHE NA MWAKA WA KUJA YESU KRISTO.

7. KUTABIRIWA MWEZI TAREHE NA MWAKA WA KUANZISHWA TAIFA LA MAREKANI.

8. KUTABIRIWA TAREHE NA MWAKA WA KUANZISHWA DINI YA MOHAMED.

9. HEKALU LA SULEMAN KUJENGWA NAKUBOMOLEWA.

10.MSIKITI WA AL AKSA NA DOME OF ROCK KUBOMOLEWA.

11. KUTOKEA KWA MPINGA KRISTO.

12. KUTOKEA KWA MUWAKILISHI WA SHETANI DUNIANI MZEE WA SIKU.

13. UKWELI WOTE KWENYE KANISA LA ROMAN CATHOLIC.

14. MIUJIZA YA SADAKA ZANGU NA MAOMBI YA KUFUNGA.

MAMBO YAKO MENGI MNO

NAMUOGOPA SANA MUNGU
Kwanza maana ya neno "biblia" ni nini?
 
Haya ukiandika mungu AU Mungu, MUNGU, unakuwa umepata faida Gani? Kwani ukiandika Kwa herufi kubwa ndio Tabia nzuri, binadamu anajengwa na matendo yake mwenyewe.
Mkuu Una haja ya kujitambua wewe mwenyewe kwanza

Uwoga wenu ndio umaskini wenu
Sio suala la kuwa na tabia njema wala sio kwamba ndo unakuwa na heshima ila ukiandika "mungu" tafsiri ni unazungumzia moja ya miungu wa kipagani iliyokuwa ikiaminiwa na jamii zisizomfahamu Mungu wa kweli.
 
Kuna dhana kwamba Biblia imejaa hadithi za kutungwa. Wasemaji wa utungaji huo wa hadithi za Biblia ni wale wapinzani wa yaliyomo hasa dhana na nadharia kwamba kuna MUNGU.

Lakini utungaji wa Biblia ulianza lini?

Hadithi za Biblia zilitungwa na kina nani na jee majina yao yanajulikana?

Watunzi Wa hadithi za kwenye Biblia walikuwa wangapi?

Hao watunzi walikuwa kutoka taifa Moja ama walitoka mataifa tofauti tofauti?

Walikubaliana wapi na vipi kuwa watunge hadithi hizo za Biblia na lengo lao lilikuwa lipi?

Jee walitumia vigezo gani kuchagua wahusika wa hizo hadithi zao na majina ya wahusika hao?

Ilichukua miaka mingapi hadithi hizo za Biblia kutungwa?

Baada ya utunzi wa hadithi hizo nani aliyetoa majina ya vitabu vinavyobeba hadithi hizo za kutungwa?

Baada ya wao kumaliza kutunga hizo hadithi Kuna watu wakati Wa zama zao waliowahi kutunga kitabu kingine kukanusha hizo hadithi zilizotungwa na hao watunzi wa hadithi za kwenye Biblia?
Hawakutunga ila walikuwa wana copy wanafanya kitu kinaitwa PLAGIARIZING -UGIGISI wanacopy kisha wanabadilisha majina ya wahusika na baadhi ya Stori wanageuza kidogo au wanaongezea Tamaduni zao kidogo.

Walikopy Maandiko ya Kale ya SUMERIA ya kale na MISRI YA KALE KHEMET ambayo yaliitangulia Biblia maelfu ya miaka kabla hata ya Uyahudi, ukristo, Uislamu na Biblia na Qur'an havijakuwepo
 
biblia maana yake ni mkusanyiko wa vitabu vingi. Waandishi wake waliandika kwa kuongozwa na roho mtakatifu. Kama unaamini uislam na quran yake why usiamini biblia? Quran yenye imekopi biblia. Waislam hamna haki kuhoji hoji uandishi wa biblia wakati quran imejaa utata wa kuandikwa kwake. Tulieni acheni kutikisa setting za dunia
Settings za dunia [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwa hiyo umekosa ushahidi? Basi Upo kwenye upotoshaji.

Wewe unauhakika Gani kama mungu aliwaagiza watu wake waandike vitabu.

Na kwanini mungu achague watu Fulani ndio Tu 😂 waandike vitabu, wakati kwenye hivyo vitabu vinasema mungu ni wawote.

Na ukicheki baadhi ya waandishi walikuwa na historia mbaya kama za ujambazi, wauwaji, ndio waje kuwa waandishi wa vitabu vya Dini.

Yan vitabu vya Dini vimeandikwa na majambazi, wauwaji.

Ameshakuwa mateka wa Dini, hatumii akili Tena kufikiri,anaogopa atachomwa Moto wa milele
Kama nitachukulia wewe ni mtu unayeamini kuhusu uwepo wa Mungu na unaamini pia katika sayansi na historia, labda hivi ni baadhi ya vitu ambavyo naweza kukuonesha kama Ushahidi wa Biblia kuwa ni maandiko matakatifu ya Mungu. (Hapa ninakiri imenibidi niingie online kutafuta sources zitakazonisaidia kunikumbusha kirahisi au zingine pia kuwa mpya kwangu lakini zitafaa kwa wewe na wengine kuziona)

1. Uvumbuzi wa kisayansi

Yako mambo yalioandikwa katika Biblia miaka mingi sana kabla ya uvumbuzi wa ukweli wake au matumizi yake. Mfano;

Ukweli kuhusu dunia kuelea yenyewe bila kushikiliwa na kitu.
Ayubu 26:7 “Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.”
Mwanadamu amefahamu ukweli huu mwaka 1650 kupitia sayansi lakini hayo maandiko yamekuwepo miaka mingi sana kabla ya ugunduzi huu.

Kutajwa kwa umbile la dunia kwa mfano wa duara
Isaya 40:22 “Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;”
Neno duara lililotumika hapo lina indicate kitu ambacho kina spherical shape sio kitu ambacho ni flat au mraba
Mtu wa kale kuamini hivi inasemekana ni Aristotle aliyeishi miaka 384 mpaka 322 BC. Lakini nabii Isaya alitumiwa na Mungu kuandika kuhusu ukweli huu around 600 BC.

Mithali 8:27 “Alipozithibitisha mbingu nalikuwako; Alipopiga duara katika uso wa bahari;”

Kutajwa kwa Bahari kwamba ina mikondo yake
Zaburi 8:8 “Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.”
Ni mpaka around karne ya 17 ndo sayansi ikagundua kitu kinachoitwa ocean currents.

Ustaarabu wa kunawa kwa maji tiririka na kuweka wagonjwa karantini

Walawi 15:13 “Na huyo aliye na kisonono atakapotakaswa na kisonono chake, atajihesabia siku saba kwa kutakaswa kwake, naye atazifua nguo zake; naye ataoga mwili wake katika maji ya mtoni, naye atakuwa safi.”

Walawi 13:46 “Siku zote ambazo pigo li ndani yake, yeye atakuwa mwenye unajisi; yeye yu najisi; atakaa peke yake; makazi yake yatakuwa nje ya marago.”
-- Hayo mambo unaweza kuona ya kawaida lakini ugunduzi wa hizi njia wala haukutokea miaka mingi sana kutokea leo na kutokufahamika kwa njia hizi kumesababisha mamilioni ya watu kufa

(hasa nchi za Ulaya ambako rekodi zipo lakini waisraeli wakiwa taifa changa kabisa katika miaka ya kale walipewa hizi mbinu kama maagizo na yaliwasaidia kuepuka na kuambukizana na magonjwa na baadaye maafa)

Hapa nimechagua mambo machache ya kisayansi kati ya mengi ili kuthibitisha kuwa isingekuwa akili ya binadamu kuweza kuandika mambo hayo ambayo sayansi ya ulimwengu imekuja kuyathibitisha mamia ya miaka baadaye.

2. Kutimia kwa unabii wa Biblia.
Hapa ndo naweza kuandika kitabu kingine kabisa, maana kuna mambo makubwa zaidi ya 1000 ambayo Biblia imeyatabiri na mpaka sasa yametimia, mengine yametimia katika kipindi hicho hicho cha Biblia na mengine yametimia baada ya kuandikwa kitabu cha mwisho cha Biblia. Sasa hapa naomba nisiandike mistari ya Biblia ila chukua muda kufanya utafiti mwenyewe.

3. Ushahidi wa miujiza iliyotajwa na Biblia
Mifano michache:
1) Ushahidi wa kuzama baharini kwa magari ya wanajeshi wa kimisri katika safari ya waisraeli (check for yourself from online sources, lots of documentaries are available)
2) Kufufuka kwa Yesu -- mtu ambaye kaburi lake lililindwa na utawala hodari na maaskari shujaa na kwa amri ya mtawala lakini walishindwa kuzuia kufufuka kwake. Kaburi lake lipo mpaka leo na halina mwili wa Yesu.

Naombeni niishie hapa kwanza, mambo mengi mtu unaweza kufanya utafiti binafsi na ukathibitisha hayo niliyoandika kama kweli una nia ya kutaka kujua na sio tu kubeza bila hoja
 
Kuna dhana kwamba Biblia imejaa hadithi za kutungwa. Wasemaji wa utungaji huo wa hadithi za Biblia ni wale wapinzani wa yaliyomo hasa dhana na nadharia kwamba kuna MUNGU.

Lakini utungaji wa Biblia ulianza lini?

Hadithi za Biblia zilitungwa na kina nani na jee majina yao yanajulikana?

Watunzi Wa hadithi za kwenye Biblia walikuwa wangapi?

Hao watunzi walikuwa kutoka taifa Moja ama walitoka mataifa tofauti tofauti?

Walikubaliana wapi na vipi kuwa watunge hadithi hizo za Biblia na lengo lao lilikuwa lipi?

Jee walitumia vigezo gani kuchagua wahusika wa hizo hadithi zao na majina ya wahusika hao?

Ilichukua miaka mingapi hadithi hizo za Biblia kutungwa?

Baada ya utunzi wa hadithi hizo nani aliyetoa majina ya vitabu vinavyobeba hadithi hizo za kutungwa?

Baada ya wao kumaliza kutunga hizo hadithi Kuna watu wakati Wa zama zao waliowahi kutunga kitabu kingine kukanusha hizo hadithi zilizotungwa na hao watunzi wa hadithi za kwenye Biblia?

Mkuu biblia ilivyo sasa ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyo kusanywa pamoja miaka 400 baada ya kufariki Yesu chini ya mfalme wa rumi Constantino.

Kabla ya hapo kulikuwa na vitabu vingi zaidi ya 200. Biblia vitabu vilivyotungwa na wayahudi wa kale kwa ajili ya kutunza sheria, miiko, desturi, historia, utamaduni na imani yao.

Biblia ni vitabu vinavyotumika kama muongozo kwenye imani ya wayahudi, waislamu na wakristo.

Kwa mujibu historia ya wayahudi, Maandishi ya torati yalianza kipindi cha Musa, Alipo pokea amri kumi za Mungu kwenye mawe mawili kutoka kwa Mungu akiwa mlima Sinai.

Kabla ya kipindi cha Musa sheria, Kani na taratibu zilihifadhiwa na makuhani vichwani mwao.
 
Safi sana, kwa hiyo tumekubaliana Yesu haijuwi biblia wala hajawahi kuiona.

Kwa hiyo hata biblia yenyewe haijijuwi, ina maa hilo jina kuna mtu alikipa hicho kitabu, ni nani huyo?

👍👍👍☑️🎁🏆🎖️
 
Back
Top Bottom