Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

..Cdm wamewahi kuwasiliana na Nec kuwaomba nyaraka zilizotumika kuwapeleka kina Halima bungeni, lakini hawakupewa ushirikiano.

..Ndio maana ninahusi kwamba hakuna nyaraka za uteuzi, na huenda kina Halima walikwenda moja kwa moja bungeni kwa MAAGIZO toka mamlaka fulani.
 
Yaani nimetokea kuwachukia sana hao wanawake, hivi unawezaje kudhalilisha chama kilichokupa jina mpaka unaenda mahakamani na unajua kabisa ume forge!!

Kuna wakati siasa za kibabe kma za Odinga zinahitajika.... Yaani mnawang'oa kwa maandamano mpaka wanatoroka nchi. Wanaudhi sana.
 
Sahihi kabisa, na vile sasa hivi siasa zinaamuliwa na vyombo vya dola na sio wananchi, hao wabunge wanafanya watakalo bila hofu kwani wana Backup ya vyombo vya dola. Kila siku nasema kwa hapa tulipofikia machafuko tu ndio yatafanya turudishe mambo kwenye mstari.
 
Wake zao hao hakina mbowe....mimi nawaambia kila siku
 
Kama hawakupeleka majina wanao uwezo wa kuwashitaki NEC. After that they can subpoena all relevant documents. Kama kulikuwa na udanganyifu, huo udanganyifu utafichuka mahakamani.
 
Kama hawakupeleka majina wanao uwezo wa kuwashitaki NEC. After that they can subpoena all relevant documents. Kama kulikuwa na udanganyifu, huo udanganyifu utafichuka mahakamani.

..mpaka sasa hivi hakuna aliyethibitisha kwamba Nec wamehusika ktk uteuzi wa Halima na wenzake.
 
CHADEMA hawajawahi kufanya mawasiliano yoyote rasmi na NEC baada ya Mdee, et al kutangazwa na NEC kuwa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA?

Mkuu, i am focus on “kesi ya kughushi”. Ninajibu tu mleta mada anayesema Chadema ingefungua kesi ya kugushi! Hata kama swali lako lina msingi, bila shaka mawasiliano hayakuwa ni kuhusu kuoneshwa ushahidi wa barua yao. Kama NEC waliionesha hiyo barua basi Chadema hawakuwa na msingi wa kudai kuwa wabunge hawa hawakuteuliwa na chama na hivyo waondolewe, hasa baada ya kupewa adhabu ya kufukuzwa kwa kukiuka utaratibu!!

Huenda unajua kuhusu mawasiliano kati ya NEC na Chadema. Unaweza kusaidia kuondoa maswali mengi. Kuhusu swali lako, mawasiliano ya Chadema hufanywa na katibu mkuu (kipindi husika alikuwa Dr. Mashinji). Aliyekuja kusema utaratibu ulikiukwa ni Mnyika baada ya Dr. Mashinji kujiuzulu na kuhamia CCM.
 
..kwa kumbukumbu zangu Dr.Mashinji aliondoka muda mrefu kabla ya uchaguzi.

..Dr.Mashinji aliondoka wakati kesi ya maandamano ya uchaguzi mdogo wa Kinondoni ikiunguruma.

..Na Dr.Mashinji alifungwa wakati akiwa tayari ni mwana-Ccm.

..John Mnyika ndiye Katibu Mkuu aliyesimamia uchaguzi mkuu wa 202O.

NB:

..Kama Kamati Kuu ya Cdm haikuteua wabunge wa Viti maalum.

..Na kama Katibu Mkuu wa Cdm amekana kujaza fomu za uteuzi.

..Na kama Tume haijatoa ushahidi kwamba imepokea fomu za viti maalum toka Cdm.

..Itoshe kusema Halima na wenzake walikwenda bungeni wakaapishwa bila kuthibitishwa na Cdm na kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi.

Cc Tindo, Erythrocyte
 
..mpaka sasa hivi hakuna aliyethibitisha kwamba Nec wamehusika ktk uteuzi wa Halima na wenzake.

Hivi wewe ukiwa na exclusive powers za kuteua mtu wa kujaza nafasi ya mbunge wa viti maalumu, huna wajibu wa kupaza sauti ya kanusho ikitokea mtu fulani, ambaye hukumteua, akaapishwa kuwa mbunge wa viti maalumu?
 
Kumbukumbu yako ina kutu vibaya sana. Uchaguzi wa 2020 ulifanyika wakati Dr. Mashinji akiwa ameshahamia CCM. Mnyika alikuwa ameshakuwa KM na ndiyo maana hakugombea hata ubunge kwenye jimbo lake la Kibamba!

Hivi wewe ukiwa na exclusive powers za kuteua mtu wa kujaza nafasi ya mbunge wa viti maalumu, huna wajibu wa kupaza sauti ya kanusho ikitokea mtu fulani, ambaye hukumteua, akaapishwa kuwa mbunge wa viti maalumu?

..uchaguzi ulivurugwa kila mahali, na katika kila hatua, chini ya uangalizi wa Nec.

..kwa msingi huo, sio ajabu Nec kukalia kimya madudu yanayohusiana na ubunge wa kina Halima.
 
..uchaguzi ulivurugwa kila mahali, na katika kila hatua, chini ya uangalizi wa Nec.

..kwa msingi huo, sio ajabu Nec kukalia kimya madudu yanayohusiana na ubunge wa kina Halima.

Ukiwashitaki NEC watawezaje kusema hawahusiki ilhali hawajawahi kuwakana hao wabunge?
 
Yaani watu wengine zero. Yaani wamewafukuza kwasababu ya kugushi halafu wawe wenyewe ndiyo wamewapitisha sasa kwa akili ya kawaida unaona hiyo sawa.

Wangefungua kesi kama wangekuwa na copy y barua lakini ofisi ya msajili hawaitoi kwasababu wenyewe ndiyo wamegushi
 
Hivi wewe ukiwa na exclusive powers za kuteua mtu wa kujaza nafasi ya mbunge wa viti maalumu, huna wajibu wa kupaza sauti ya kanusho ikitokea mtu fulani, ambaye hukumteua, akaapishwa kuwa mbunge wa viti maalumu?

Wakati wa Magufuli hizo taasisi zilikuwa na nguvu hiyo? Kama NEC ilithubutu kusema wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura ni 29m, yaani nusu ya watanzania wote tunaofikia 60m, hapo ulitegemea watoe kanusho gani? Kilichofanyika kwa akina Halima Mdee kuingia bungeni, ni ushahidi tosha kuhusu ubovu wa katiba yetu kuhusu madaraka ya rais.
 
Sorry, kama bado una amini kuwa tuna mahakama za kufungua kesi za kisiasa, hasa kwa hizi siasa chafu zilizoingizwa kwenye Muhimili wa mahakama, basi unahitaji maombi. Huhitaji akili kubwa kujua kiwango cha ombwe la kiutendaji la mihimili yetu, na taasisi nyingine za kimamlaka.
 
Ukiwashitaki NEC watawezaje kusema hawahusiki ilhali hawajawahi kuwakana hao wabunge?

Uko sahihi kinadharia, je unawashitaki NEC kwa mahakama zipi? Nawapongeza CDM kwa kutokupoteza muda wao kwenda kufungua kesi kwenye mahakama zilizojazwa siasa chafu.
 
Unajua, na kila mtu anajua, kwamba JPM hatunaye tangu March 2021. Hiyo NEC bado inamuogopa JPM kusema kwamba haijui chochote kuhusu uteuzi wa Mdee na wenzake?
 
..unawashtaki Nec kwa ushahidi gani kuwa wamehusika?

CHADEMA wanapofungua kesi, wanawashitaki:
[emoji828]️Mdee na wenzake kama walalamikiwa wa kwanza
[emoji828]️NEC kama mlalamikiwa wa pili
[emoji828]️AG kama mlalamikiwa wa tatu

Kesi wanayofungua CHADEMA ni ya kupinga uhalali wa ubunge wa Mdee na wenzake, kwa mtindo uleule unaotumika kupinga ubunge wa wabunge wa majimbo. Hoja ya CHADEMA ni kwamba hakijawahi kufanya nomination ya mwanachama wake yeyote ili ateuliwe na NEC kuwa mbunge wa viti maalumu.

Walalamikiwa wanao wajibu wa kutetea uhalili wa ubunge wa Mdee na wenzake. Kama hawana utetezi, ubunge wa walalamikiwa wa kwanza lazima utenguliwe. Kama wana utetezi, basi issue ya kughushi, if any, lazima itakuwa bayana.
 
Uko sahihi kinadharia, je unawashitaki NEC kwa mahakama zipi? Nawapongeza CDM kwa kutokupoteza muda wao kwenda kufungua kesi kwenye mahakama zilizojazwa siasa chafu.

Kama hivyo ndivyo, basi CDM hawana sababu ya kuhangaika na Mdee na wenzake. Kwanini wanapoteza muda kupeleka barua NEC na kwa Speaker huku wakijua hata wakitafuta relief mahakamani hawataipata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…