Kama kawaida yetu 'Waswaholi' Ajali ya Mtwara imeua Wengi, ila sasa Wote tuko tu kwa Mzazi aliyepoteza Watoto wake Wawili

Kama kawaida yetu 'Waswaholi' Ajali ya Mtwara imeua Wengi, ila sasa Wote tuko tu kwa Mzazi aliyepoteza Watoto wake Wawili

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Niendelee kutoa Pole zangu za dhati kabisa kwa Familia zilizopoteza Wapendwa wao na kwa wale waliopatwa na Majeraha nawaombeni kwa Mwenyezi Mungu awaponye upesi na huko mnakotibiwa mpate Tiba stahiki.

Huu Msiba ni wa Jumla na hata tukiwa tunauongelea basi tuuongelee Kiujumla jumla na siyo kama Kawaida ya Uswahili wetu kuanza Kuubagua na Kuona kuwa aliyefiwa hasa ni Mzazi ( Wazazi ) wa Watoto Wawili tu.

Kila Mtu akiwa anaonyesha tu Huruma na kuwa so emotional kwa aliyefiwa na Wanawe Wawili je, wale Wafiwa wengine ambao hatuwaongelei hapa tunawajengea Picha gani? Kwahiyo Wao hawajafiwa au kwa Kufiwa Kwao na Watoto / Watu wachache hawapaswi Kusikitika sana na hata Kuonewa nasi Huruma?

Na hapa kwa 75% lawana zangu nyingi nazipeleka kwa Vyombo vya Habari vya Tanzania mpaka vya Mitandaoni kwani Wao ndiyo Waanzilishi wa huu 'Uswahili' wakiwa wanataka Kuitendea vyema dhana ya 'Novelty' katika News Values na Media zao zipate Mvuto kutoka kwa Audience wao wakiwa Wamesahau kuwa pamoja na yote kwa Tukio kama hili 'Balancing' na 'Fairness' ya Kuhabarisha inatakiwa zaidi.

Poleni Wafiwa, Wahanga na Watanzania kwa huu Msiba na tuendelee Kuwafariji Wafiwa na Kuwatia Nguvu Majeruhi wote, ila tusisahau kwa Wamiliki wa Vyombo vyote vya Usafiri kuhakikisha Magari yetu yanafanyiwa Service mara kwa mara lakini pia Ukaguzi kwa Madereva ni muhimu ili tusije kuwa tunawapa Watu ambao labda hawajalala vyema au wamelala na Pombe au wana Stress za Maugomvi yao na Wake zao huko watokako.
 
Kweli if noma sasa hivi bushman umeanza kujua jua kiswahili. Hapo ulipo andika " vyombo vya habari vya Tanzania mpaka vya mtandaoni" wakati bado upo Bunda vijijini ungeandika " vyombo vya habari vya Tanzania MPAKA NA HADI vya mtandaoni". Sasa hivi umehamia Bunda mjini kiswahili kimechange kidogo.

Mkuu iheshimu sana Bunda mjini.
 
pole ziwafikie majeruhi na wafiwa pia kwa pamoja
Hiki ndicho kinatakiwa Kisemwe na Watanzania wote kwa Wafiwa na Majeruhi wa hiyo ( ile ) Ajali na siyo Kuwabagua wengine na Kumuonea tu Huruma Mmoja aliyefiwa na Watoto wake Wawili.
 
Hiki ndicho kinatakiwa Kisemwe na Watanzania wote kwa Wafiwa na Majeruhi wa hiyo ( ile ) Ajali na siyo Kuwabagua wengine na Kumuonea tu Huruma Mmoja aliyefiwa na Watoto wake Wawili.
naaam kabisa
 
Tz kuna uswahili sana
Nimeacha muda kusikiliza redio sababu ya waandishi wa habari uchwara.
 
Back
Top Bottom