Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Mungu ni uwezo,cheo,ujuzi flani wa kipekee au mkubwa sana.
Uthibitisho wa uwepo wa Mungu ni kupitia uimbaji wake tu. Yan hata kama huamini biblia na vitabu vingine maelezo yake,basi ukiangalia uumbaji wote,kwanzia mpangilio wa sayari zote kama jua, mwezi, nyota utashangaa. Hakuna mwanadamu anayeweza kupangilia hivyo.
Angalia dunia yetu ilivyopangwa vizuri bila kuingiliana kama bahari,maziwa,mito nchi kavu,milima na viumbe hai wote.
Ni mwanadamu gani amefanyiza huo mpango? Au amewahi kujaribu akaweza? Bila shaka kutakuwa na mkuu zaidi ya kila kitu ndio huyo mweza yote yaani Yehova Mungu.
Magufuli ana uwezo, ana cheo, ana ujuzi wa kipekee na mkubwa sana, anajua boiling point ya silver bila kusoma kwenye kitabu.
Definition yako ya Mungu imesema "Mungu ni uwezo, cheo, ujuzi flani wa kipekee au mkubwa sana".
Je, Magufuli ni Mungu?
Huo unaosema ni uumbaji wa Mungu, unathibitishaje kuwa ni uumbaji wa Mungu na si kitu kingine chochote?
Watu wanakufa kwa matetemeko ya ardhi, magonjwa, ma tsunami, utasemaje dunia imepangwa vizuri sana?
Huyo Mungu wako alishindwa kuumba dunia ambayo majanga hayo hayawezi kutokea?