Sikia mkuu.
Mungu alipomuumba Adam na Hawa kusudi lilikua wamtii na Kumtumikia yeye tu, pamoja na yote aliyowapatia wafurahie lakini walikua bado hawajafunuliwa jema na Baya kwa wakati wote walikua wanajua yaliyo mema tu.
Ila Baada ya Ibilisi kuona na yeye anaweza kua na uwezo kuliko Mungu ndipo alipoasi sasa na kutupwa duniani, na ibilisi huyo alikua malaika huko Mbinguni lakini pia huyo ibilisi hakuwahi kufunuliwa uwepo wa Kristo ambae ni Mwana wa Mungu, yeye alimuona Mungu kama Mungu Pekee yake soma Mwanzo vizuri utaijua Biblia
Sasa baada ya kuja kuwadanganya Adam na Hawa na kulila tunda la ujuzi wa mema na mabaya ndipo walipofunuliwa ufahamu na kujua lipi jema na lipi baya na ndo maana wakati Mungu anakuja watembelea walikua wamejificha ni sababu ya kua walijua tayar mema na mabaya.
Na hakika baada sasa na wao kudanganywa na kuasi ndio Mungu akaanza kutoa hukumu alianza na ibilisi, Akaja kwa Mwanamke, akabaki Adam na Mungu alihitaji Adamu atubu aombe radhi hakika naamini wangesamehewa lakini hakuna sehemu yeyote Adamu alijutia au kutubu au kuomba samahani na ndipo Mungu akasema mwisho hakika Mtakufa. Hivyo tulideserve.
Lakini sababu ya Mungu kua mwingi wa huruma na rehema pamoja na Adamu kushindwa kutubu / kujutia bado alituhurumia akasema hivi sitaleta gharika wala maafa yeyote tena kwa kizazi cha wanadamu ilaaaa nitamtuma Mwanangu ili aje kuukomboa ulimwengu huu na dhambi zake, na ndio Maana yesu ama Kristo mwana wa Mungu alipokuja na kukamilisha kazi yake tulikombolewa kwa njia ya Imani na si Sheria tena na ndio maana sasa una uhuru wa kuchagua kumtumikia Mungu aliye Juu au Ibilisi ungali hai. Uchaguzi ni wako. Ili baada ya kufa mwili huu basi roho yako iwe mahali sawasawa na njisi ulivyoenenda na kumchagua wa kumtumia wakati ukiwa Duniani.
Mungu anasema Mautini Hakuna kumtumikia yeye wala kujua lolote bali ungalipo hai ndipo uwezapo kumtumikia.
Mwisho kupanga ni kuchagua na kila Mtu yupo anaemtumikia either ni Mungu au Shetani. Mungu yupo na Shetani yupo na mwisho kuna maisha mazuri zaidi ya haya baadae
Huna haja ya kuogopa kufa mwili huu ila tuogope kufa kwa roho zetu.