Kama Kifo ni mpango wa Mungu basi Mungu wenu atakuwa katili sana, mnawezaje kuwa nae?

Mungu ni alfa na omega, kila kitu kinachofanyika ni mipango ya mungu na kazi ya mungu haina makosa at this point the future is set already regardless of his actions.

Je! Mungu anajua au hajui kwamba mtu fulani atakuwa mzuri au mbaya? Ikiwa unasema 'Anajua', basi kinachofuata kwamba mtu huyo analazimika kutenda kama Mungu alivyojua mapema jinsi atakavyotenda, vinginevyo, maarifa ya Mungu hayatakuwa kamili.

Mambo ya kiroho na kiimani unataka ufanye criticle thinking. Unatumia vitabu vitakatifu kama unavyotumia science book. Well ni sawa ila fikra zako hazibadili lolote endapo kuna ulimwengo wa roho.

Nyakati zinakuja ambazo ubongo wako utashindwa kutafsiri jambo lililo mbele yako na hapo ndipo nafasi ya roho yako itakapoonekana. Endapo kuna ulimwengu wa roho, wakati wako utakapofika ubongo wako utauacha kaburini ukiliwa na funza.

Wanasema maandiko matakatifu ni chakula cha rohoni.
 
Kabla ya kula tunda dhambi ilianza wewe. Hujui kuwa ukaidi ni dhambi?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
mbona kuua ni dhambi lakini akiua Mungu hamuhesabu kama ni dhambi?

hiyo dhambi ya ukaidi ilimuingia vipi shetani tena akiwa mahali patukufu sehemu ambayo inaaminiwa kua dhambi haiwezi kufanyika?
 
Mambo ya kiroho na kiimani unataka ufanye criticle thinking. Unatumia vitabu vitakatifu kama unavyotumia science book. Well ni sawa ila fikra zako hazibadili lolote endapo kuna ulimwengo wa roho.

Nyakati zinakuja ambazo ubongo wako utashindwa kutafsiri jambo lililo mbele yako na hapo ndipo nafasi ya roho yako itakapoonekana. Endapo kuna ulimwengu wa roho, wakati wako utakapofika ubongo wako utauacha kaburini ukiliwa na funza.

Wanasema maandiko matakatifu ni chakula cha rohoni.
ukipiga marufuku critical thinking hata wewe utajikuta inakua ni ngumu kuwapinga wahindu kua ng'ombe ni mungu wa kweli.

So unakubali ng'ombe ni mungu wa kweli kwasababu ni mambo ya kiimani yasiyo hitaji critical thinking?
 
kwa hiyo upeo wa mungu uliishia kumuona shetani akiwa malaika tu haukuweza kumuonesha extra miles kua atakuja ku change?
Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa kwa sababu ni roho isiyokatika matakwa ya aliyeiumba. Shetani ni roho iliyotamani nafasi isiyo yake ikaasi, una maamuzi ya kuitii au kutoitii.

Ni hivi suala hapa ni matakwa ya MUUMBA. Mwenye ulimwengu wake. Ana matakwa yake ili uli uwepo kwenye sehemu yake, na matakwa yake ni usitende dhambi maana ukiitenda utakufa.

Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Si suala la wewe maana si MUUMBA, si suala la shetani maana hana hayo mamlaka, ni suala la MUNGU. Ni matakwa ya MUNGU na ulimwengu wake. Usipoyafuata unakufa, unakuwa haupo tena, unarudi kwenye hali uliyokuwa nayo kabla ya ww kuumbwa. HAUPO.

HAPO KWAKO NYUMBANI UNA MASHARTI YAKO KWA WATOTO WAKO NA WASIPOYAFUATA UNAWAADHIBU. MFANYAKAZI ASIPOYAFUATA UNAMFUKUZA N.K NDIVYO MUNGU WAKO ALIVYO NA ULIMWENGU WAKE.
 
ukipiga marufuku critical thinking hata wewe utajikuta inakua ni ngumu kuwapinga wahindu kua ng'ombe ni mungu wa kweli.

So unakubali ng'ombe ni mungu wa kweli kwasababu ni mambo ya kiimani yasiyo hitaji critical thinking?
Ng'ombe ni mungu wa wahindi sio mungu wangu. Imani yangu hainitumi kuamini ng'ombe, siyo mawazo yangu hayanitumi bali imani. Sifikirii kuwa ng'ombe si mungu bali naamini hivyo. Wahindu hawaamini MUNGU wangu, ila hawafikiri kuwa ng'ombe si mungu, wakifikiri hawataamini katika MUNGU kama ww ulivyo na wasiwasi juu ya uwepo wake. Ni suala la imani sio critical thinking. Ni ulimwengu wa roho. Mm namtazama ng'ombe katika ulimwengu wa mwili na namla nyama, wahindu wanamtazama katika ulimwengu wa roho wanamuona mungu. Hawamtazami MUNGU kwa namna ambayo imani yangu inamtazama. Hizo ni tofauti za kiimani na kiroho. Hakuna critical thinking hapo.
 
Daa we jama hujui ki2 kimoja Mungu hakutaka kumkaribia kiumbe yoyote baad ya kuasi kwasababu yeye ni light kwasababu light ikutana na dark dark sio inaulizwa ni inapotea 2.. lakini kwa huruma yake akaamua isiwe hivo atume watu wake ili kuwapa na nyny nafasi...ndo maan mwisho wa siku akij katika ukuu wake hakuna dhambi itakayosalia. Mark my words

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
hoja yangu inazungumzia kabla hata uhasi haujafanyika

Mungu muweza wa yote aliumba malaika wa vita, malaika wa ulinzi wa kazi gani?

Malaika wana mapanga yakatayo kote na kote (sime) kwa ajili ya matumizi gani, huoni hiyo inaonesha mungu ni mortal kama sisi na ndio maana bila ulinzi hawezi ku survive?
 
Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa kwa sababu ni roho isiyokatika matakwa ya aliyeiumba. Shetani ni roho iliyotamani nafasi isiyo yake ikaasi, una maamuzi ya kuitii au kutoitii.

Ni hivi suala hapa ni matakwa ya MUUMBA. Mwenye ulimwengu wake. Ana matakwa yake ili uli uwepo kwenye sehemu yake, na matakwa yake ni usitende dhambi maana ukiitenda utakufa.

Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Si suala la wewe maana si MUUMBA, si suala la shetani maana hana hayo mamlaka, ni suala la MUNGU. Ni matakwa ya MUNGU na ulimwengu wake. Usipoyafuata unakufa, unakuwa haupo tena, unarudi kwenye hali uliyokuwa nayo kabla ya ww kuumbwa. HAUPO.

HAPO KWAKO NYUMBANI UNA MASHARTI YAKO KWA WATOTO WAKO NA WASIPOYAFUATA UNAWAADHIBU. MFANYAKAZI ASIPOYAFUATA UNAMFUKUZA N.K NDIVYO MUNGU WAKO ALIVYO NA ULIMWENGU WAKE.
unatatizo la kutoelewa swali

uliposema "Unakosea tu hapo unaposema shetani kaumbwa. Shetani kabla ya kuwa shetani (mpinzani) alikua malaika baada ya kuasi ndio akawa shetani."

mimi nimekuuliza "kwa hiyo upeo wa mungu uliishia kumuona shetani akiwa malaika tu haukuweza kumuonesha extra miles kua atakuja ku change?"

umeliona swali?
 
hoja yangu inazungumzia kabla hata uhasi haujafanyika

Mungu muweza wa yote aliumba malaika wa vita, malaika wa ulinzi wa kazi gani?

Malaika wana mapanga yakatayo kote na kote (sime) kwa ajili ya matumizi gani, huoni hiyo inaonesha mungu ni mortal kama sisi na ndio maana bila ulinzi hawezi ku survive?
Upo sahihi, Uliumbwa kwa mfano wa MUNGU. MUNGU yupo kama wewe isipokuwa si mortal maana ni roho. Na roho yako imeumbwa kwa mfano wake, ila ukapewa na mwili ambao ni mavumbi. Inawezekana Mwili kupitia ubongo ni kizuizi cha kutafsiri mambo ya roho kwa usahihi.

Unajua shetani aliona udhaifu akadhani anaweza kuchukua kile kiti akakikalia. Alishindwa. Alikuwa na mawazo ya aina yako, mawazo yako na yake hayatofautiani sana. Kuuchunguza udhaifu wa MUNGU na kujaribu kumshusha katika nafasi aliyopo.
 
Ng'ombe ni mungu wa wahindi sio mungu wangu. Imani yangu hainitumi kuamini ng'ombe, siyo mawazo yangu hayanitumi bali imani. Sifikirii kuwa ng'ombe si mungu bali naamini hivyo. Wahindu hawaamini MUNGU wangu, ila hawafikiri kuwa ng'ombe si mungu, wakifikiri hawataamini katika MUNGU kama ww ulivyo na wasiwasi juu ya uwepo wake. Ni suala la imani sio critical thinking. Ni ulimwengu wa roho. Mm namtazama ng'ombe katika ulimwengu wa mwili na namla nyama, wahindu wanamtazama katika ulimwengu wa roho wanamuona mungu. Hawamtazami MUNGU kwa namna ambayo imani yangu inamtazama. Hizo ni tofauti za kiimani na kiroho. Hakuna critical thinking hapo.
imani ya wahindu haisemi ng'ombe ni mungu maalumu wa wahindu. Hakuna dini ambayo imembinafsisha mungu kua ni wa upande wao tu, hata dini yako imetaja mungu wako kwamba ndio mtawala wa dunia (ikijumlisha na waumini wa dini zote hadi hao wahindu)

unawezaje kuamini bila kufikiria?
 
unatatizo la kutoelewa swali

uliposema "Unakosea tu hapo unaposema shetani kaumbwa. Shetani kabla ya kuwa shetani (mpinzani) alikua malaika baada ya kuasi ndio akawa shetani."

mimi nimekuuliza "kwa hiyo upeo wa mungu uliishia kumuona shetani akiwa malaika tu haukuweza kumuonesha extra miles kua atakuja ku change?"

umeliona swali?
Upeo wa MUNGU mm siufahamu, sifahamu kikomo chake. Inawezekana upo sahihi kuwa hakumuona shetani bali malaika, na inawezekana alimuona shetani ajae na akaandaa mpango wa kumdhibiti. Mm sijui maana ukomo wangu wa imani juu ya jambo hilo upo limited. Labda huenda tutakapokuwa katika ulimwengu wa roho tutafahamu haya kwa uwazi wake. Ninachofahamu katika ulimwengu wa roho kuna vita kati ya ubaya na wema, na ubaya mwisho wake ni kifo.
 
Umetegwa hapo ujisound ulivo mjinga kwa kufocus kweny tunda kuliko kweny ukaidi wa kufanya ulichokatazwa. Afu baadae muanze kulalamika mnachomwa kwa kuonewa..yani unaona muhimu kujua tunda kuliko neno la ukaidi kwa Mungu wako

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
kama sio muhimu kujua aina ya tunda kwanini habari hiyo imeandikwa?

Ntachomwa na moto ulioutengeneza wewe kwenye fikra zako, kama Mungu umeshindwa kuthibitisha yupo sembuse moto?
 
Hakuna product wakati ukizaliwa unakuwa empty headed mpka utakapoanza kulearn things na kupata akili ya kuchagua mbichi na mbivu kama alivoeleza mtalaamu hapo kuna Mungu anaeua kila kiube anavotaka au Mungu anaeokoa ukimkubali na una uwezo wa kumkubali kwa hiari Mungu mlipa kisasi au Mungu mwema wakati wote asiejihusisha na dhambi

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app

"...Mungu anaeokoa ukimkubali na una uwezo wa kumkubali kwa hiari Mungu mlipa kisasi au Mungu mwema wakati wote asiejihusisha na dhambi"

Nikuulize kutokana na maelezo yako hapa! Mungu wapo wangapi?
 
imani ya wahindu haisemi ng'ombe ni mungu maalumu wa wahindu. Hakuna dini ambayo imembinafsisha mungu kua ni wa upande wao tu, hata dini yako imetaja mungu wako kwamba ndio mtawala wa dunia (ikijumlisha na waumini wa dini zote hadi hao wahindu)

unawezaje kuamini bila kufikiria?
Kama kila jambo ni lazima kufikiria Moyo wako unawezaje kuendelea kufanya kazi bila fikra zako?

Imani ya wahindu ni ya wahindu. Sijui kwann wameamini hivyo. Siwezi wahukumu, sina mamlaka hayo.
 
Upeo wa MUNGU mm siufahamu, sifahamu kikomo chake. Inawezekana upo sahihi kuwa hakumuona shetani bali malaika, na inawezekana alimuona shetani ajae na akaandaa mpango wa kumdhibiti. Mm sijui maana ukomo wangu wa imani juu ya jambo hilo upo limited. Labda huenda tutakapokuwa katika ulimwengu wa roho tutafahamu haya kwa uwazi wake. Ninachofahamu katika ulimwengu wa roho kuna vita kati ya ubaya na wema, na ubaya mwisho wake ni kifo.
upeo wa Mungu haujui?

So hujui kua mungu ni mjuzi wa yote?
 
Kama kila jambo ni lazima kufikiria Moyo wako unawezaje kuendelea kufanya kazi bila fikra zako?

Imani ya wahindu ni ya wahindu. Sijui kwann wameamini hivyo. Siwezi wahukumu, sina mamlaka hayo.
irrelevant

nimeuliza unawezaje kuamini bila kufikiria?
 
Ndio. Ninaamini bila kufikiri. Kama jinsi ambavyo sina control na mapigo ya moyo wangu katika fikra zangu ndivyo hivyo hivyo ambavyo akili yangu ina nafasi ndogo sana ya control ya imani yangu. Huenda haina nafasi kabisa.

Imani ni suala la kiroho, roho haina ubongo huu wa mwili na nyama. Vita vya kiroho si vya mwili na nyama. Imani yangu inaniongoza na si fikra zangu. Iwapo kutatokea mabadiliko ya imani basi hayatatokana na critical thinking bali nafasi ya ushawishi ya kiroho. Na ndani utasikia amani. Kuna hali fulani ya kuwa na utulivu ndani yako katika masuala ya roho endapo mambo yako ya kiroho yapo sawa. Hali huwa tofauti kabisa mambo yanapokuwa si sawa. ukinitukana nikakuuwa, akili yangu inaweza niambia nipo sahihi maana umenitukana na nikapata hasira ila roho yangu haitakuwa na amani.

Imani yangu juu ya MUNGU itapotea kabisa kama nikifikiri kwa mawazo yangu bila msaada wa kiroho. Nitafanana na wewe. Nitaanza kuhoji udhaifu wa MUNGU n.k, mm sitaki hilo litokee. Nina mambo mengi ya kutumia ubongo wangu kama uchumi, afya, siasa n.k sina la kupoteza katika imani.
 
Wakati huo adam kashafanya dhambi we unahisi ukiwa na dhambi una thamani kwa Mungu kuliko shetani? Unajidanganya bro angefutwa shetani human race ingefutwa pia kwasababu tulikuwa fungu moja ni neema 2

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
hiyo dhambi aliyoifanya adam chanzo chake ni mungu mwenyewe, aliyeweka tunda la mabaya ni adam au mungu?

dhambi za farao zilipaswa kumuajibisha yeye binafsi lakini hilo Mungu hakuliona mpaka akaamuru watoto wakwanza wafe kwa lengo la kumkomoa farao?

inamaana hao watoto walikua hawana thamani kwa Mungu kutokana na dhambi za farao alizozifanya?
 
Ndio. Ninaamini bila kufikiri. Kama jinsi ambavyo sina control na mapigo ya moyo wangu katika fikra zangu ndivyo hivyo hivyo ambavyo akili yangu ina nafasi ndogo sana ya control ya imani yangu. Huenda haina nafasi kabisa.

Imani ni suala la kiroho, roho haina ubongo huu wa mwili na nyama. Vita vya kiroho si vya mwili na nyama. Imani yangu inaniongoza na si fikra zangu. Iwapo kutatokea mabadiliko ya imani basi hayatatokana na critical thinking bali nafasi ya ushawishi ya kiroho. Na ndani utasikia amani. Kuna hali fulani ya kuwa na utulivu ndani yako katika masuala ya roho endapo mambo yako ya kiroho yapo sawa. Hali huwa tofauti kabisa mambo yanapokuwa si sawa. ukinitukana nikakuuwa, akili yangu inaweza niambia nipo sahihi maana umenitukana na nikapata hasira ila roho yangu haitakuwa na amani.

Imani yangu juu ya MUNGU itapotea kabisa kama nikifikiri kwa mawazo yangu bila msaada wa kiroho. Nitafanana na wewe. Nitaanza kuhoji udhaifu wa MUNGU n.k, mm sitaki hilo litokee. Nina mambo mengi ya kutumia ubongo wangu kama uchumi, afya, siasa n.k sina la kupoteza katika imani.
we umewezaje kuamini Mungu yupo bila kufikiri?
 
Back
Top Bottom