Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Kama humuamin Rais wako basi wewe unapenda ubishi wa kitoto na mimi siwezi endelea kubishana na wakati hio ilikua habari kubwa

Nimekuletea video kabisa ya Rais sababu ningekuletea habari ya kawaida usingeamini
Tusitumie nguvu kubwa kwa jambo ambalo lilishatolewa ufafanuzi na Rais wa nchi
Mzee usizunguke, leta namba,
Huko shule ulikosoma mwenzetu ndio mliambiwa kitu akosema raisi inabidi uamini tu kama quran/bible? Kwamba unashindwa kufanya checkup kujua kama ni kweli au lah? Wew sema mwaka gani gdp per Capital yetu ilishuka na ilishuka kwa kiasi gani?
Unaleta maneno ya kwenye kanga 😂
 
Sina kiongozi, Sina tegemezi yoyote yule
Huo ndio mda wa ku save kama unaweza ku survive Kwa shilingi laki 2 zingine weka hakiba kila mwisho wa mwaka tafuta uwekeze. Kigoma huko ni pazuri sana nunua hata ardhi huko ni bei nafuu baada ya miaka kadhaa ukishakuwa na majukumu zitakusaidia.

Usioo save saa hizi ukaishia kupinda starejhe Kuna mahali utakwama ukiwa na majukumu
 
Mzee usizunguke, leta namba,
Huko shule ulikosoma mwenzetu ndio mliambiwa kitu akosema raisi inabidi uamini tu kama quran/bible? Kwamba unashindwa kufanya checkup kujua kama ni kweli au lah? Wew sema mwaka gani gdp per Capital yetu ilishuka na ilishuka kwa kiasi gani?
Unaleta maneno ya kwenye kanga 😂
Gdp per capita unaweza uka google na kama unafuatilia bunge la budget lilopota walisema
Usiwe unapenda kutafuniwa
 
Unategemea nini kwa dogo janja kama huyu
21FC7B3A-F4E8-478B-8FFA-6109EA7616C8.jpeg
 
Kwema Wakuu!

Kuna aina tatu za Maskini.
1. Maskini wa kutupwa (Fukara)
2. Maskini wa kawaida
3. Maskini aliyechangamka.

1. Maskini Fukara
Maskini Fukara hili kundi ni wale Watu ambào kula yao ni mshikeshike, hawana pakuishi, yaani hawa ndio huitwa hohehahe. Hawa kwa asilimia kubwa wamekata tamaa ya maisha. Na ukikutana nao moja kwa moja umaskini ndio utambulisho wao.

2. Maskini wa Kawaida.
Hili ni kundi ambalo wengi tupo hapa.
Hawa wanapata kiasi mahitaji yao ya msingi lakini sio Quality. Yaani atakula ndio chakula lakini sio mlo kamili.
Yaani yeye kila siku maugali na maharage sio shida. Kuvaa nguo za mtumba ni jambo la kawaida. Mpya ni mara mojamoja.

Makazi yao ni vibanda fulani ambavyo vinawastiri na baridi, jua na mvua. Ingawaje wao wenyewe huita nyumba lakini kimsingi sio nyumba.

3. Maskini waliochangamka.
Kundi hili ni lile la wenye vipato ambavyo ni kati ya milioni moja mpaka tano.
Kwa Tanzania kundi hili nalo hujiona limetoboa lakini kimsingi ni kundi maskini tuu kwani vipato vyao haviwezi kukidhi mahitaji ya msingi kwa kiwango kikubwa.

Mfano mtu mwenye kipato cha milioni moja mpaka tano hana uwezo wa kula milo mitatu kamili mwaka mzima pasipo kupasua matairi. Hapohapo hana uwezo wa kuishi kwenye makazi mazuri na kuvaa nguo Standard. Ni lazima kimoja atashindwa. Hapohapo awe anabima nzuri ya afya. Gari nzuri ambayo mafuta kwake sio tatizo, huku anasomesha watoto shule nzuri. Utagundua hicho kipato ni kidogo mno.

Kundi hili linanafasi ya kupambana na kuingia kundi la matajiri daraja la chini ambao kipato chao ni milioni 10 mpaka milioni mia moja.
Ishu inakuja pale ambapo Watanzania wengi tukishapata tumilioni mbili kwa mwezi ndio tunaona tumeshatoboa na tunaanza kubweteka ilhali kimsingi bado tupo tabaka la juu la maskini.

Unapoambiwa nchi yako ni maskini elewa kuwa robo tatu ya wananchi vipato vyao kwa mwezi havitoboi milioni tano.

Ukisikia mtu anakuita Maskini na unajiona una maisha mazuri. Sijui gari, nyumba na unapesa za kubadilisha mboga alafu muda huohuo kipato chako halifiki milioni tano jua anahaki ya kukuita hivyo.

Ingawaje umaskini kwa upande mwingine ni mtazamo. Mtu anaweza kuwa Maskini wa kipato lakini akawa anajiona tajiri(mental illness) alafu yupo mwenye kipato cha milioni 100 alafu anajiona maskini(hana shukrani).

Ijumaa Kareem
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Kazi ipo
 
Back
Top Bottom