Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Kwa hiyo bwana Robert haya ni maoni yako na mtazamo wako tu si uhalisi? Kwamba mtu anaepata 5m kwa mtazamo wako ni nasikini ila si uhalisia?

Umaskini na utajiri ni dhana aliyonayo mtu.
Ni mtazamo tuu.
Wapo Watu wanajiona matajiri na hawajawahi kushika pesa hata shilingi mia moja.

Umaskini wa Ulaya na umaskini wa Afrika ni tofauti.
Umaskini wa mjini na maskini wa kijijini ni tofauti.
Tukija kwenye uhalisia (mantiki), kwenye mantiki jambo likiwa kweli sehemu A lazima liwe kweli sehemu B.

Ni maoni na mtazamo tuu. Ndio maana humu kila mmoja anakuja na vile ajuavyo.
Ila wapo wale wafuatao upepo yaani waliokariri maoni na mitazamo ya wengine hasa wasomi waliozoea kukaririshwa na kupuuzia maoni na mitazamo yao
 
Mkuu,
Haya ni maoni na mtazamo wako, hauna mchanganuo wowote, huwezi kumshawishi mtu kuamini unachoongelea. Ili umshawishi mtu kuwa anayepata 5m kwa mwezi ni masikini, lazima uje na vigezo, takwimu zikiambatana na idadi ya watu, eneo husika nk. Sasa wewe ukisema anayepata 5m ni masikini, huku ukisema hata mlo kamili hawezi kumudu, huna uhalisia, huna vigezo wala huna takwimu za kukusaidia na kutushawishi.

Mfano, ukisema mwenye 5m kwa mwezi hawezi kumudu hata mlo kamili, kwako milo kamili mitatu kwa siku ni milo gani, isije kuwa watu unaongelea frequencies tofauti za maisha, huenda unamaanisha kula milo mitatu Serena hotel, wakati sisi tunaongelea kuipa familia yako milo kamili mitatu.

Funguka.
 


Wewe ni mtu wa hovyo sana
 

Mlo kamili inafahamika, ujumlisha na mahitaji mengine muhimu kwa kiwango cha juu.
 
Andika ili hata asiyefahamu ajue mlo kamili ni nini na kwa siku familia ya kawaida ya watu watano inaweza kutumia shilingi ngapi kupata mlo kamili.
Mlo kamili ni moja ya mfano wa mahitaji ya mtu anayotakiwa kuwa nayo.
Mtu mwenye kipato cha milioni tano hana uwezo wa kula mlo kamili alafu muda huohuo asomeshe shule za kitajiri, awe na nyumba ya kifahari, alafu hapohapo aendeshe gari kali, alafu hapohapo, yeye na familia wavae nguo Standard,

Sasa wewe umekalia hapohapo kwenye mlo utadhani ndio hitaji Pekee
 
Kipato cha Dola 2000 Kwa mwezi..naona unastandard nzuri YA maisha japo WW Sio tajiri Ila upo kwenye good standard of life
 
I rest my case!
 
I rest my case!

Tafuta Watu wenye KIPATO cha milioni tano. Si wapo. Kama Wakuu wa mikoa then angalia maisha yao.
Bado hawajafika middle Class.
Waulize wenyewe nje ya posho kama hiyo pesa inatosha kuwafanya waitwe matajiri wadogo
 
Duh hapa tunapeana presha na kupata mental illness!
Ila sawa mkuu...
Tutaishi hivyo hivyo....
 
Umaskini ni nini mkuu? Unapimwaje au unapimwa katika scale gani?
Mkuu wewe kama ukiwa huna mali za kuachia watoto wako na wajukuu wako siku ukiondoka hapa duniani wewe ni masikini. Achana na upumbafu wa kusema urithi wa mtoto ni elimu, achia watoto na wajukuu mali watayoiendeleza.
 
...Wewe uko Kundi Gani, Mkuu Mtibeti ?? [emoji848][emoji848]
 
Masikini ni mtu ambae hawezi kupata mahitaji ya msingi kama chakula,mavazi na malazi..

Kampeni iliopo duniani kwa sasa ni kupunguza masikini ila haimaanishi kuongeza matajiri kwa sababu kua tajiri sio hitaji la msingi la binadamu

Kama unasehemu ya kulala +unakula na kunywa+unapata mahitaji ya msingi Tambua kua unaendelea vizuri sana!! Hakuna kiwango cha fedha ambacho kinaweza kukutosheleza lakini hata wataalamu wamefanya tafiti kadhaa na kuthibitisha kua kama unaweza kutumia $5 kwa siku kwa nchi za kusini mwa Africa basi unaendelea vizuri..

Watz wengi wanakipato cha chini ya milioni1 kwa mwezi (sio nzuri na sio mbaya pia),Wenye kipato cha juu ya milioni 1>>> wengi bado wanaishi kwa kujibana sana..

Na hata ile 1% wanastress zao huko Masaki na Oysterbay
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…