Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Huo ni ukweli mtupu. Una 5M kwa mwezi halafu unaishi kwenye hotel ya nyota tano kwa maana unakula, unalala na unakunywa katika hoteli hiyo. Hapo unautafuta umasikini kwa kuishi maisha ambayo yapo juu ya kipato chako. Lakini kwa wale ambao wanaishi maisha ya kawaida hutwo tuela tunatosha kwa kubadilisha mboga, malazi na kinywaji bila wasiwasi.
Hakunaga maisha ya kawaida unless ni kauli ya kujifariji, kuna maisha ya umasikini na utajiribasi.
 
Hakuna kitu kinaitwa anasa, Anasa ni kauli za kimaskini.
Kijana wangu sasa hapa unavuka mipaka. FUTA HII. Anasa zipo jomba na ndo zinazowafanya watu warudi kwenye ufukara. Kama unapata hela unazitumia kishenzi bado wewe unakuwa hujaepuka umaskini hata kama unapata zaidi ya 5m. Matajiri wote huhakikisha pesa hazitumiki kizembe ili zisiwaponyoke.
 
Sasa kama kila weekend unaangamiza million 2 kwenye starehe tu unadhani hio 10M itakutosha kwa lipi?
Kuna umuhimu mkubwa watu wakapata elimu ya fedha. Kimsingi utajiri na ubahili ni ndugu wa damu. Vijana wakiona tajiri anakula bata huwa hawajui tayari mhasibu wake kashapigia hesabu ili kuepusha balaa. Tena matajiri wengine hujilipa mishahara kabisa ili wasiingilie biashara zao.
 
Kijana wangu sasa hapa unavuka mipaka. FUTA HII. Anasa zipo jomba na ndo zinazowafanya watu warudi kwenye ufukara. Kama unapata hela unazitumia kishenzi bado wewe unakuwa hujaepuka umaskini hata kama unapata zaidi ya 5m. Matajiri wote huhakikisha pesa hazitumiki kizembe ili zisiwaponyoke.
Hizo zinazoitwa anasa hazina shida kama unajiweza kiakili na kiuchumi. Uzembe wa akili na umasikini ndo unafanya maisha fulani yaonekane ni anasa lakini infact hakuna anasa.
 
Kuna umuhimu mkubwa watu wakapata elimu ya fedha. Kimsingi utajiri na ubahili ni ndugu wa damu. Vijana wakiona tajiri anakula bata huwa hawajui tayari mhasibu wake kashapigia hesabu ili kuepusha balaa. Tena matajiri wengine hujilipa mishahara kabisa ili wasiingilie biashara zao.
Nakubaliana na hoja Yako aisee
 
Milioni tano kwa mwezi ni kama 160,000 kwa siku, huwezi kumudu milo mitatu Serena Hotel, bado ni masikini wa kutupwa
Mil 5
Uko sahihi mkuu ndomana huwaga sitaki kutaka kumiliki gari wakati mm ni maskini...kipato cha kuwa gari atleast uwe unapiga 10ml per month hapo gar halitokusumbua...jamaa yangu analipwa 800k kwa mwezi halafu ana gari la mkopo huwa namuonea huruma sana[emoji23]
Acha undina inategeana na aina ya gari
 
Utajiri na afya ni category mhili tofauti kabisa Mkuu.
Afya ni Afya, utajiri ni utajiri, umaskini ni umaskini.
Mtu anaweza kuwa na afya na akawa maskini.
Na mtu anaweza kuwa anaumwa na akawa tajiri.
Na mtu anaweza kuwa maskini na tajiri na asiwe na afya
Hapa ndio mimi baadhi ya watanzania wananikera na kuona wababaishaji. Mtu kaleta Mada yake anaongelea utajiri wa kuwa na fedha nyingi mtu awe na spending power inayoeleweka, jitu linatoka kushiba mihogo yake huko linaanzaa ooh utajiri ni afya. Ebu tustick kwenye Mada hizo habari za afya weka pembeni kwanza.
 
Hahahahah... nyuzi kama hizi za kutiana hasira nazipenda sana. Umaskini ni fedheha. Sema jomba hiyo 5m umeweka kiwango cha juu kinoma.. mshahara wa mkuu wa mkoa huo. Huu uzi mimi nitauchukua kama mwongozo wangu kwa mwaka huu...
Kwamba kwa sababu hiyo 5M anapokea mkuu wa mkoa basi ni nyingi?
 
Usijidangaye, material things wala sio utajiri mkuu. Kwa umri wangu, nimetambua na kuelewa afya na kumjua Mungu ndio utajiri na sio hizo blah blah.

Maandiko yako mengi huku mkuu unayaandika tokana na upepo wa umri wako kwa sababj bado unajitafuta. Ukishajitafuta na kujipata ndipo utaona hayo uyaonayo ya maana si kitu.
Wewe kama ni mkristo kasome upya biblia acha kujificha kwenye unyonge. Biblia inamtaka mtu mwema aache urithi kwa watoto na watoto wa wanawe
Usijidangaye, material things wala sio utajiri mkuu. Kwa umri wangu, nimetambua na kuelewa afya na kumjua Mungu ndio utajiri na sio hizo blah blah.

Maandiko yako mengi huku mkuu unayaandika tokana na upepo wa umri wako kwa sababj bado unajitafuta. Ukishajitafuta na kujipata ndipo utaona hayo uyaonayo ya maana si kitu.
Mithali 13: 22 kaisome vizuri kama wewe ni mkristo. Hata huyo Mungu alimuumba Adam akamweka bustani ya Eden ikiwa na kila kitu ambacho angekiitaji. Huo mstari hapo juu unakutaka wewe kama kweli ni mtu mwema uache urithi wa mali kwa wanako na wajukuu zako.

Sasa unaweza kuacha urithi kwa Hao wote kama wewe ni masikini??
 
Hoja yako ni Kwa miji ya DSM na Arusha na Dodoma , kuna miji hapa tz ukiwa na mshahara wa laki 5 , unaishi kifalme
Hahahah una laki 5 yako upo Manyara huko, , hakuna nauli, kodi ya nyumba full ni 80k, hakuna sherehe nyingi, bill ya maji ipo chini, umeme pia bill ipo chini,
Nje umefuga kuku 20 ambao kila week unachinja mmoja kubadili ladha ya mboga,
Upande wa pili una bustani yako ya mboga majan unayomwagilia kwa majibya bure 😂😂

Kwa laki tano lazima uishi kifalme ,😂 mziki Dar, kodi tu 200k, nauli familia nzima 100k kwa mwezi bado misosi sasa 😂
 
What is Poverty? Is a failure or unable to meet Basic needs, eg, Food, clothes and shelter.

Kwa definition Yako ya umaskini unachanganya needs vs wants.

Utakuwa Bado uko Kwa dada ukianza maisha utajua ukweli.
Hii definition yako ya poverty ni ya form one B. Ukienda level za juu za education Kuna Maslow Hierarchy of needs.
 
Hii imewauma wengi ambao hujiona wametoboa maisha kwa sababu vipato vyao ni milioni moja au mbili. Sasa kusikia kuwa bado ni maskini ndio wanashangaa.

Hawa ndio wale wakiona mtu anatoa milioni tano wanamuita fogo
Mkuu,
Hakuna mahali umetoa takwimu za kiuchumi/kimahesabu kusupport hoja zako, yaani umeendeshwa na mihemko ndio maana utapata upinzani kimtazamo. Huwezi kusema 5m ni masikini bila kutoa facts za kuichumi, huwezi kusema mtu wa 5m per month hata milo mitatu kamili ni shida tukakuacha tu upotoshe jamii.
 
Back
Top Bottom