Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Kwema Wakuu!

Kuna aina tatu za Maskini.
1. Maskini wa kutupwa (Fukara)
2. Maskini wa kawaida
3. Maskini aliyechangamka.

1. Maskini Fukara
Maskini Fukara hili kundi ni wale Watu ambào kula yao ni mshikeshike, hawana pakuishi, yaani hawa ndio huitwa hohehahe. Hawa kwa asilimia kubwa wamekata tamaa ya maisha. Na ukikutana nao moja kwa moja umaskini ndio utambulisho wao.

2. Maskini wa Kawaida.
Hili ni kundi ambalo wengi tupo hapa.
Hawa wanapata kiasi mahitaji yao ya msingi lakini sio Quality. Yaani atakula ndio chakula lakini sio mlo kamili.
Yaani yeye kila siku maugali na maharage sio shida. Kuvaa nguo za mtumba ni jambo la kawaida. Mpya ni mara mojamoja.

Makazi yao ni vibanda fulani ambavyo vinawastiri na baridi, jua na mvua. Ingawaje wao wenyewe huita nyumba lakini kimsingi sio nyumba.

3. Maskini waliochangamka.
Kundi hili ni lile la wenye vipato ambavyo ni kati ya milioni moja mpaka tano.
Kwa Tanzania kundi hili nalo hujiona limetoboa lakini kimsingi ni kundi maskini tuu kwani vipato vyao haviwezi kukidhi mahitaji ya msingi kwa kiwango kikubwa.

Mfano mtu mwenye kipato cha milioni moja mpaka tano hana uwezo wa kula milo mitatu kamili mwaka mzima pasipo kupasua matairi. Hapohapo hana uwezo wa kuishi kwenye makazi mazuri na kuvaa nguo Standard. Ni lazima kimoja atashindwa. Hapohapo awe anabima nzuri ya afya. Gari nzuri ambayo mafuta kwake sio tatizo, huku anasomesha watoto shule nzuri. Utagundua hicho kipato ni kidogo mno.

Kundi hili linanafasi ya kupambana na kuingia kundi la matajiri daraja la chini ambao kipato chao ni milioni 10 mpaka milioni mia moja.
Ishu inakuja pale ambapo Watanzania wengi tukishapata tumilioni mbili kwa mwezi ndio tunaona tumeshatoboa na tunaanza kubweteka ilhali kimsingi bado tupo tabaka la juu la maskini.

Unapoambiwa nchi yako ni maskini elewa kuwa robo tatu ya wananchi vipato vyao kwa mwezi havitoboi milioni tano.

Ukisikia mtu anakuita Maskini na unajiona una maisha mazuri. Sijui gari, nyumba na unapesa za kubadilisha mboga alafu muda huohuo kipato chako halifiki milioni tano jua anahaki ya kukuita hivyo.

Ingawaje umaskini kwa upande mwingine ni mtazamo. Mtu anaweza kuwa Maskini wa kipato lakini akawa anajiona tajiri(mental illness) alafu yupo mwenye kipato cha milioni 100 alafu anajiona maskini(hana shukrani).

Ijumaa Kareem
Yaani wewe jamaa hua kichwa chako kimejaa dillusions na vitu vya kufirika sana

Nikajua makala itakua imejaa takwimu na definitions zinazokubalika kwenye economics na standards za world bank kumbe tuko hapa unatuletea unachofikiri wewe kichwani mwako with no stats to back up your nonsense whatsoever!

Upunguze rarerareee mzee

Toa scholarly work watu tusome tupate elimu,kumbe blah blah za uswahilini
 
Usijidangaye, material things wala sio utajiri mkuu. Kwa umri wangu, nimetambua na kuelewa afya na kumjua Mungu ndio utajiri na sio hizo blah blah.

Maandiko yako mengi huku mkuu unayaandika tokana na upepo wa umri wako kwa sababj bado unajitafuta. Ukishajitafuta na kujipata ndipo utaona hayo uyaonayo ya maana si kitu.
Kujipata ni perception ya mtu na si fact, Afya na mungu hawalipi ya international school
 
Kuna vitu vingi sana mdogo wangu Mtibeli havijui tokana na umri wake. Hii Dunia ni "very complicated", kuna matajiri ila hawawezi kula chakula kwani wagonjwa na hata huo mlo mmoja haupiti wala haruhusiwi kula, anaona bora asingekuwa hata na 100 ila anakula na kuwa mwenye furaha. Kuna maskini anakula chochote na mwenye furaha na amani. Kuna mwenye miguu hawezi kutembea na kuna ambaye hana miguu ila anatembea.

Refer kwa Pogba anakiri ni bora alivyokuwa maskini alikuwa na furaha na amani kuliko sasa ni tajiri ila hana furaha wala amani.

Kwa umri wangu na baada ya kujipata kiuchumi, nakiri hakuna kitu bora kuliko kuwa na afya njema na kumjua Mungu wa kweli na Yesu Kristo aliyemtuma. Haya yote ni kujilisha upepo. Dunia inasumbua wanadamu hususani sisi Wanaume katika vitu vitatu. Utajiri(Mali za duniani), Umiliki(Utawala) na Mpenzi(Wanawake). Katika hilo Suleiman pamoja na utajiri na ufalme wake pamoja na kuwa na wanawake wengi, anakiri ni upuuzi mtupu na kujilisha upepo. Mkikua mtaelewa.
Utajiri ni utajiri na unahusisha matireal things, hizo zingine ulizozisema ni changamoto za kiafya bila kujali wewe ni maskini ama tajiri.
 
Mkuu hapo Unazungumzia mambo mawili tofauti.
Kuna afya Vs Maradhi
Kuna utajiri Vs Umaskini
Kuna Haki Vs Dhulma
Kuna wema Vs Ubaya
Kuna Furaha Vs huzuni n.k.

Unaweza ukawa na pesa lakini usiwe na furaha.
Unaweza ukawa na Afya lakini usiwe na Furaha.
Unaweza ukawa maskini lakini usiwe na furaha au ukawa nayo.

Wewe ushaingia kwenye mkondo mbaya wa negativity.
Furaha kwenye umaskini ni mental illness
 
What is Poverty? Is a failure or unable to meet Basic needs, eg, Food, clothes and shelter.

Kwa definition Yako ya umaskini unachanganya needs vs wants.

Utakuwa Bado uko Kwa dada ukianza maisha utajua ukweli.
Hiyo definition ya poverty ni ya dark age, leo ukishindwa kumlipia mtoto wako elimu bora ni sehemu ya umaskini.
 
Siko kwenye formal sector,navuna kitaa ila nakusadia tu ukweli pesa sio maembe amka ukatafute wanao hustle wanajua.

Hizi ndo mentality unapata opportunity huna mbele wa nyuma unaambiwa utalipwa laki 2 Kwa Mwezi unaona Bora uendelee kukaa Kwa shemeji.

Stories za kahawa na kuota magorofa na V8 Kwa mwaka 1 zinaharibu mentality za vijana. # No easy money may be ukawe shoga
Wingi wa changamoto haimanishi kidogo kionwe kikubwa
 
Zinaitwa maskini kwa kutumia gdp per capita income kipindi cha magufuli gdp per capita ilipanda tukaondoka kwenye nchi maskini kipindi cha samia gdp per capita imeshuka tumerudi tena kwenye kundi la nchi maskini

Nimeshangaa sana na hiki ulikua hukijui hivi huko shuleni mnasomaga au mnasukuma siku ziende
Hujui gdp per capita ndo kipimo cha kujua nchi ni maskini au tajiri na bado hujui aiseeee
Propaganda za kisiasa hazina uhalisia, Tanzania watu wake ni hohehahe na haijawaitoka daraja hilo.
 
[emoji2][emoji2]
Elimu ya kukariri mbaya Sana.

Nchi yetu itachukua miaka mia mbili kuondoka kwenye nchi maskini.
Sasa hivi tupo kwenye level ya poorest countries hatujafikia kweney Umaskini wa kawaida.
Kipi hauelewi ndugu
Unabishana na mtu aliekariri notisi za form three C
 
Back
Top Bottom