Flano
JF-Expert Member
- Aug 7, 2019
- 5,446
- 14,880
Hakuna utajiri mkubwa kama kua na afya njema na kuwa ni mtu mwenye kushukuru, haya maisha ya show off unaweza ingaza hata zaidi ya milioni 10 na ukawa ni mtu wa stress tu.
Ndugu zangu mara moja moja mkipata nafasi muwe mnatembelea mahospitalini kuwajulia hali wagonjwa msisubiri mpaka nyinyi wenyewe muugue ndio muende hospital.
Kuna rafiki yangu alitaka kujiua kisa duka lake limeungua, alijifungia ndani wiki nzima hataki hata chakula, baada kupata hizo habari nikaenda kwake nikaforce twende tukatembee apunguze stress, alinikatalia katakata baada ya kumlazimisha sana ndio akakubali, ilikua ni jumapili nilinunua vizawadi kidogo halafu moja kwa moja nikampeleka Ocean Road kwenda kuwajulia hali wagonjwa wa Cancer.
Baada ya kurudi tu home kitu cha kwanza jamaa aliomba ugali, baada ya kula na kushiba akipiga goti kumshukuru Mungu kwa neema kubwa ya afya aliyonayo.