Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Hahahahah... nyuzi kama hizi za kutiana hasira nazipenda sana. Umaskini ni fedheha. Sema jomba hiyo 5m umeweka kiwango cha juu kinoma.. mshahara wa mkuu wa mkoa huo. Huu uzi mimi nitauchukua kama mwongozo wangu kwa mwaka huu...
 
Hahahahah... nyuzi kama hizi za kutiana hasira nazipenda sana. Umaskini ni fedheha. Sema jomba hiyo 5m umeweka kiwango cha juu kinoma.. mshahara wa mkuu wa mkoa huo. Huu uzi mimi nitauchukua kama mwongozo wangu kwa mwaka huu...

Milioni tano ni maskini aliyechangamka hata wanaozimiliki kwa mwezi mbona wanalijua hili fika.
Watu tukazane tuikoe maisha ya kizazi chetu na nchi.
Hao wanaooma nawakatisha tamaa pole yao.
 
Wenye hela hawawezi weka avatar kama aliyoweka yeye.. hizo editing za picha zinapatikana infinix sijui 🤣
Ni maskini mwenzetu, aje tupeleke CV kwa Boss la DP World
Wewe unafaa kuwa mkurugenzi wa makuli pale bandarini, huna haja ya kuleta cv jumatatu njoo saa 2 kamili uanze kazi. Tafadhali fika na comment hii uwaoneshe walinzi ili uruhusiwe kuingia. Hongera sana kwa kuaga umaskini.
 
Hahaha...
Kumbe watu tu masikini na hatujui..!!
Sawa bwanaa.
 
Siamini kama kuna mtu anaweza kuendesha maisha kwa mshahara wa million 5 kwa mwezi mbona pesa ndogo mi nilipata kazi sehemu flan nikawa nalipwa 12M nikaacha kazi maana ilikua haitoshi , sahivi nipo mtaani sina kazi niliona kule napoteza muda
 
Yani mtu anaingiza mil 5 hawezi kula mlo kamili tena hafikishi mitatu? Nyie kwenu mnakula WATU nini

😃😃
Milo mitatu yenye mlo kamili. Hawezi kuoa kwa mwaka mzima bila kupasua matairi.
Hapohapo nyumba nzuri, au apartment kali, hapohapo mafuta ya Gari, hapohapo ada ya watoto wanaosoma shule standard, hapohapo nguo nzuri ambazo sio mtumba,

Inatosha kumuita tajiri
 
Haya maneno yalikuwepo zama za kikwete. Naona now yanarudi tena kwa kasi. Kwamba ndani ya nchi masikini Kuna masikini wanawaita masikini wenzao masikini. Safi sana kazi iendelee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…