Pre GE2025 Kama Mbowe atachukua fomu kugombea uenyekiti, ni bora kuanzisha chama kipya cha siasa. Watanzania wanataka mabadiliko lakini CHADEMA ni tatizo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sema nilichogundua kwa muda wote huu ni kwamba; siasa kwa Tanzania, ni biashara! na pia ni ajira!
Kauli za Boni Yai na Yericko Nyerere zinathibitisha ugunduzi wako. Hawa watu wanatokwa povu majukwaani kumbe ni kwasababu Mbowe anawashibisha kwa vyeo na fedha.

Hivyo hawataki mkuu wa meza wao aondoke . Rubbish kabisa.
 
Kumwondoa Mbowe kuna faida nyingi kuliko hasara na faida moja wapo ni chama kuwa na sura ya kitaifa kuliko ukanda na ukabila.
 
Mkuu hapo namba 2 alizingua muda mbaya kabisa...alishamwandaa Dr. Slaa...naungana na wewe hapo kwenye No. 4 itakuwa vigumu mno kwa CDM kuhimili vishindo vya uzinguaji endapo Lissu hata kuwa Chairman.
 
Mkuu hapo namba 2 alizingua muda mbaya kabisa...alishamwandaa Dr. Slaa...naungana na wewe hapo kwenye
Na tangu amuengue Dr. Slaa, Ari ya watanzania kujitokeza kukipwmbania chama ikapungua sana. Kabla ya hapo ilikuwa maandamano yakiitishwa na chadema nchi inatetemeka. Lkn hivi Sasa ni Mbowe na boni Yai tu ndiyo huwa wanafanya maigizo ya maandamano.

Lkn kuonewa kwa Dr. Slaa na manung'uniko ya Dr. Slaa wakati anaondoka yaliwapa watu mwanga kuwa kumbe jasho la mtu ndani ya chadema halithaminiwi.
 
Sema nilichogundua kwa muda wote huu ni kwamba; siasa kwa Tanzania, ni biashara! na pia ni ajira!
Kuna tatizo siasa ikiwa ni ajira?
Biashara nini kinanunuliwa na kuuzwa kwenye siasa?
 
Hili ni wazo zuri Sana linaloweza kuwaweka pamoja wafuasi wa Lissu na Mbowe ambao sasa wamegawanyika.
Wakilifanyia kazi hili wazo, cdm itavuka salama.
 
Erythrocyte na Retired nini maoni yenu kuhusu hili
 
Matusi aliyoporomoshewa mzee wa Watu, akiwa amekipambania CDM toka 1995, na baadaye kwenye jimbo lake alipowaingiza viongozi wengi wa serikali za vijiji na Mwaka 2000 kukifanya CCM kupotea kabisa Karatu....mtu aliyekipigania Chama kwa kiwango hicho unamwondoa tu kirahisi....

Sasa hivi uchaguzi wa serikali za mtaa umeporwa na wanyang'anyi tamko linalotoka ni kulaani tu..... kwa kweli tunahitaji mtu anayeweza kuwakemea hawa wahuni
 
Mbowe kapoteza ushawishi, akae pembeni awapishe watu wengine, asishupaze shingo.
 
Hata km ulikua hufuatilii siasa inafikia kipindi unajiuliza mbona Lissu kugombea uenyekiti inaonekana ni dhambi! Uenyekiti inatakiwa ugombewe na binadamu, mbona Lissu akigombea inakua kesi
 
Lissu akiwa Mwenyekiti wa chama hata mimi nitajiunga CHADEMA
 
Kabisa mkuu. Wanatia kinyaa kwenye demokrasia kwa kukataza watu wengine kugombea uenyekiti. Hiki bila shaka ni mradi wa familia ya Mbowe.
Lissu katangaza kugombea, Mbowe kimya. Lissu amechukua fomu za kugombea, Mbowe kimya. Sijui amemkataza vipi kugombea kama unavyodai? Na kuna mwingine pia aliyetangaza nia, nae hakuzuiwa.

Amandla...
 
R.I.P Chacha Wangwe...
 
Mimi sijui kwa nini watu wanasema kuwa uongozi wa sasa wa CDM hawataki Lissu agombee wakati kapewa fomu hadharani?

Au mnaweka mazingira ya kuleta machafuko katika chama kama mtu wenu atashindwa? Sio vizuri mnavyofanya.

Amandla...
 
Kila anaeondoka chadema, humnyooshea kidole mwenyekiti, mbowe ajitafakari.
 
Mbowe akishinda itakuwaje ?... Pro-Lissu watakubali matokeo na kubakia chamani?

Chadema ipo kwenye wakati mgumu na muhimu Sana kwake.

Tindo econonist Mag3 Nguruvi3
Naamini Mbowe anaweza kushinda sababu ya kwamba viongozi wa chadema at least 90% wamekua kisiasa au kuingia chadema kwa invitation na mentorship ya Mbowe including Lissu.

Having said that, Mbowe akitumia incumbency, intimidation, threats na figisu kushinda ndio ataharibu ila akikeep his cool apige kampeni kwa wajumbe mbona atashinda tu na ndio demokrasia tunayotaka.

Tatizo ni hawa machawa, wanataka apite bila kupingwa au ashinde kwa kishindo na ndio wataharibu hata ushindi wake (in case atashinda).

Mimi ni Team Lissu ila nina uhakika hata Lissu akishinda itakua 50-55% hata Mbowe hawezi pata zaidi ya 60%. Kwa lissu itakua ni ushindi ila kwa mbowe 50-55% ya ushindi itakua imetia doa credibility yake na mandate. Kwahiyo hawa machawa ndio watataka wafanye figisu zote ili Mbowe ashinde kwa 90%!! Na hiki ndio kinafanya waanze rafu mapema sana licha ya Mbowe mwenyewe kuwa kimya.

Ushauri: Mbowe achague, agombee na ashindwe au ashinde kwa simple majority akose mandate au ajitoe ili watu wengi zaidi wachukue fomu na ndio tuone demokrasia ya kweli. Otherwise matokeo yotote yale yatakua damage kubwa kwa Mbowe na chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…