Sasa mmeamua kuwachezea waTanzania wananchi wenye maisha ngumu kila kona!.Tumeshatoka huko. Huko ambako Rais anatenga muda wa kukutana na wananchi wachache na kuzungumza nao juu ya shida zao.
Kwa wakati huo, hizo shida za wananchi zilipata afueni? Jibu ni hapana.
Jana imetangazwa kwamba Bi. Kiguu na Njia [nasikia jana katua Nigeria huko]naye ataanza tena huo utaratibu.
Ukisikia kufilisika kifikra ndo huko sasa!
Wamekaa madarakani zaidi ya miaka 60 na bado tu hawazijui shida za wananchi.
Sasa kama hawazijui shida za wananchi, watawezaje kuleta maendeleo?
Halafu tunashangaa na kulalamika eti umeme shida, maji shida, n.k.
Majibu ya kwa nini tupo kwenye hali tuliyonayo, yapo wazi kabisa.
Jingine, iweje huyu Rais wetu asizijue shida za Watanzania?
Kwani yeye anaishi wapi? Kaishi wapi? Katokea wapi mpaka asizijue shida za watu?
Nchi ina maajabu hii!!!
Hivi kwa akili ndogo tu kukaa Lumumba kusikiza shida za wananchi unamsaidiqje mwananchi mwenye ako na shida kibao na hana hata hiyo pesa ya kufunga safari kutoka pale Ifakara kuja kukueleza mashida yake! Huu ndio usanii!
Wanqnchi wamedhulumiwa mno na hao hao walioko nyima yako mama hebu acha usanii.
Tenga hiyo sikunyako uende hata hapo Kibaha tu kwa siku nzima wauze hata kuku zao wakuje ndipo utajua kweli huna wasaidizi!
Hapo hujaenda Manyara!, Kondoa, Mfaranyaki, Ludewa, Kilombero tunalima miwa lakini sukari hatuna!