Kama mpaka leo hujui shida za wananchi, wewe hufai kuongoza!

Kama mpaka leo hujui shida za wananchi, wewe hufai kuongoza!

Huenda hana kazi ya kufanya kwahiyo anaona asiposikika kila siku watu watajua hafanyi kazi. Utaratibu wa rais kila siku kutengenezewa habari ulianzia kipindi cha mzee wa msoga, Mzee wa chato naye akaiga kama ambavyo machawa walivyoanza kusikikika katika kipindi chake na kuendelea hadi kwa kizimkazi Mkapa hakuwa na mpenda mambo madogo madogo kila siku kutaka kusikikika na kusifiwa.

Kwa kweli urais umekuwa mrahisi sana. Haifai rais kila siku kusikika tena kwenye mambo cheap sana.
Mlipenda rais pimbi anayejifungia ndani kama mwali,
Nachukia watu wazima kujitoa ufahamu, matatizo ya watanzania yanajulikana kwa ujumla wake, umeme, maji, bei ndogo za mazao, Pembejeo kuwa juu na kadhalika,
TUFAHAMU MBALI NA HAYO,
Yapo matatizo ya mmoja mmoja miongoni mwetu ambayo ni sugu na yameshindikana kutatuliwa kutokana na kuwa complicated sasa haya ndiyo yanakwenda kupatiwa ufumbuzi, tukumbuke yapo matatizo ya kijumla Jumla na yale sugu ya watanzania mmoja mmoja.
# OVER!
Hapana mkuu kuna sehemu wanajua wametushika atufurukuti kupitia kura zetu.

Unafikiri huyu tupige kura na zihesabiwe kwa haki, atatoboa?

Anachopaswa angetenga siku hio moja katika mwezi kuwawajibisha aliowateua kumsaidia kazi kama mawaziri, wakuu wa mikoa wafanya kazi ofisi za umma n.k.
Wananchi zaidi ya milioni 60 utasikiliza kero za kila mtu?

Kero gani hizo zimekosa utatuzi hadi raisi aje kutatua, alio wateua wanafanya nini?
Aanze na rpt ya CAG.
 
Mama anaishi kwenye "bubble", aidha kasahau shida alizopitia akiwa raia wa kawaida au MARAHA YAMEZIDI!
Kifupi, uongozi umemzidia uwezo kiakili, kifikra na uongozaji. Hana timu nzuri ya kumshauri, aliyonayo ni MACHAWA YALIYOJAA FUNZA KICHWANI!
 
Back
Top Bottom