Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Duuuh maelezo marefu mkuu
 
Unazunguka zunguka tu na arguments and claims kuhusu uwepo wa Mungu.

Bado Hujathibitisha Mungu yupo.

Bado Hujathibitisha imani yako ya uwepo wa Mungu ni ukweli.

Mungu huyo ni imani na mawazo ya kufikirika tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.
 
Unazunguka zunguka tu na arguments and claims kuhusu uwepo wa Mungu.

Bado Hujathibitisha Mungu yupo.

Bado Hujathibitisha imani yako ya uwepo wa Mungu ni ukweli.

Mungu huyo ni imani na mawazo ya kufikirika tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.
 
Bado hujathibitisha kutokuwepo kwa Mungu pia—au unafikiri akili zako limited zinaweza comprehend kila kitu in the universe? Logic yako ni kama kujaribu kupima bahari na kikombe.
Kutokuwepo kwa Mungu haithibitishwi kwa kudai kujua kila kitu, bali kwa ukosefu wa ushahidi thabiti unaoweza kupimika.
Kama tunavyokataa viumbe vya kubuni kama majini au mbuzi wanaoruka kwa sababu hatuna ushahidi wa kuwepo kwao, ndivyo pia tunavyokataa madai ya Mungu hadi uthibitisho wa wazi utolewe.
Ukosefu wa ushahidi ni msingi wa busara kutoamini, si kiburi cha kujua kila kitu.
 
Unazunguka zunguka tu na arguments and claims kuhusu uwepo wa Mungu.

Bado Hujathibitisha Mungu yupo.

Bado Hujathibitisha imani yako ya uwepo wa Mungu ni ukweli.

Mungu huyo ni imani na mawazo ya kufikirika tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.
Kusema “Mungu ni mawazo ya kufikirika tu” ni kudhani kwamba chochote kisichoonekana moja kwa moja hakiwezi kuwa kweli — lakini si kila kitu cha kweli lazima kiwe cha kuonekana au kupimika. For example, hatuoni akili (mind), upendo, au haki — lakini tunajua vipo kwa sababu ya athari na ushahidi wa uwepo wake katika maisha yetu.

Vivyo hivyo, existence ya Mungu haihitaji tu macho bali mantiki, uzoefu wa kiroho, na historical consistency ya imani ya mamilioni ya watu across ages and cultures.

Imani si udhaifu wa akili, bali ni jibu la kiakili kwa ukweli usio kamili kwa vipimo vya binadamu. Lack of physical proof ≠ lack of truth. Logic alone can't exhaust divine reality.
 
Hizi ni arguments tu zinazojaribu kuelezea na kufosi uwepo wa huyo Mungu.

Kwanza, thibitisha Mungu yupo.

Sio kurukia kusema mara ooh! Mungu ni "necessary being"

Necessary being kutoka wapi?
 
Sababu ya kuhitimisha kutokuwepo ni kutoonekana tu? Umeshawahi kuyaona mawazo?
Si kutoonekana tu, sababu ya msingi ya kutoamini kuwepo kwa Mungu ni ukosefu wa ushahidi wa kuaminika, si tu kutomwona.
Mawazo yanaathiri ulimwengu kwa njia inayoonekana, unaweza kuyaona kwa vipimo vya ubongo, lugha, maandiko, na matendo.
Lakini Mungu hadhihiriki kwa njia yoyote inayopimika au kujaribiwa.
Kudai Mungu yupo bila ushahidi ni sawa na kudai kuna joka lisiloonekana kwenye dari na haiwezi kuthibitishwa wala kupingwa, lakini haimaanishi ni la kweli.
 
Unafanya Logical fallacy ya argument from popularity, Argumentum ad populum.

Kwa vile mabilioni ya watu wanaamini Mungu yupo, Na wewe unafuata mkumbo huohuo kusema na kudai Mungu yupo bila uthibitisho wala uhakika.

Mamilioni ya watu duniani kuamini kuna Mungu, Hakufanyi Mungu huyo awepo. Na wala sio kigezo cha kusema kwamba Mungu yupo!

Thibitisha imani yako kuhusu uwepo wa Mungu ni ukweli na si imani zako uchwara ulizo aminishwa na kupumbazwa.
 
Hoja yako inajenga msingi wa kutokuwapo kwa Mungu juu ya ukosefu wa ushahidi wa kisayansi tu, lakini truth haipimwi kwa njia moja tu. Lack of empirical evidence is not evidence of absence.

Vitu vingi ambavyo hatuvioni au hatuvipimi moja kwa moja — kama upendo au dhamira bado vinaathari halisi,, watu wengi wana ushuhuda wa kiroho binafsi, unaovuka vipimo vya maabara. So, wisdom siyo tu kukataa bila kuona, bali pia kufungua akili kwa uwezekano wa reality iliyo juu ya uwezo wetu wa sasa wa kupima.
 
Tofauti ya anayeamini bila uthibitisho na wewe ni nini?
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa ili tuhakikishe imani zenu ni ukweli na si uongo, toeni uthibitisho wenye uhakika kabisa kwamba Mungu yupo.

Msifosi imani zenu za kidini za vitabuni zisizo na uthibitisho wowote ule.

Mimi siamini. Sihitaji kuamini nataka kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.
 
Si kutoonekana tu, sababu ya msingi ya kutoamini kuwepo kwa Mungu ni ukosefu wa ushahidi wa kuaminika,
Umetumia maneno kutoamini na ukosefu wa ushahidi. Meaning kutoamini uwepo wa MUNGU ni suala la imani lisilo na ushahidi. Au utajipinga na hapa pia?
si tu kutomwona.
Mawazo yanaathiri ulimwengu kwa njia inayoonekana, unaweza kuyaona kwa vipimo vya ubongo, lugha, maandiko, na matendo.
Lakini Mungu hadhihiriki kwa njia yoyote inayopimika au kujaribiwa.
Inatofauti gani na uwepo wa MUNGU kuathiri ulimwengu kwa njia ya dini, ibada, maandiko na matendo ya kiimani?
Kudai Mungu yupo bila ushahidi ni sawa na kudai kuna joka lisiloonekana kwenye dari na haiwezi kuthibitishwa wala kupingwa, lakini haimaanishi ni la kweli.
Unathibitisha vipi hakuna joka darini iwapo huwezi kufika darini?
 
Proof!!???
Kama huwezi kuiona pumzi lakini unajua ipo kwa sababu unaishi, basi kuwepo kwa Mungu si lazima kuthibitishwe kwa macho — athari na mpangilio wa uhai unaoishi ni ushahidi tosha wa nguvu iliyo juu ya uelewa wetu.
 
Sayansi haisemi hakuna MUNGU, inasema hakuna uthibitisho/ushahidi kuwa yupo. Sayansi pia haisemi upo uthibitisho kuwa hayupo. Na hapa ndo sisi wasomi wa Tanganyika tunapopotezwa.
 
Hizi ni arguments tu zinazojaribu kuelezea na kufosi uwepo wa huyo Mungu.

Kwanza, thibitisha Mungu yupo.

Sio kurukia kusema mara ooh! Mungu ni "necessary being"

Necessary being kutoka wapi?
Kitu hakiwezi kujiumba.

Ulimwengu una mwanzo (umethibitishwa kisayansi—Big Bang).

Lazima kuwe na kisababishi kisicho na mwanzo (kisingesababishwa)—hicho ndicho tunaita ni Mungu mwenyewe.


Hii ni hoja ya kisababu (cosmological argument) kwa kifupi, inayojibu pingamizi bila kulazimisha imani, bali kwa mantiki.
 
Sayansi haisemi hakuna MUNGU, inasema hakuna uthibitisho/ushahidi kuwa yupo. Sayansi pia haisemi upo uthibitisho kuwa hayupo. Na hapa ndo sisi wasomi wa Tanganyika tunapopotezwa.
kutokuwa na ushahidi wa jambo fulani si uthibitisho kuwa halipo. Pili, kuelewa dhana ya Mungu si suala la kisayansi pekee, bali linahusisha falsafa, imani, na tafakuri ya ndani. Kwa hivyo mkuu kusema kwamba wasomi tunapotezwa kwa sababu ya sayansi kutokuwa na uthibitisho wa Mungu ni kupotosha muktadha wa sayansi yenyewe. Ukweli ni kwamba sayansi inajibu maswali ya jinsi, wakati imani na falsafa zinajibu maswali ya kwa nini.
 
Reactions: Tsh
Upo sawa. Hoja za waamini kutokuwepo huwa zinaegemea kisayansi, sayansi ambayo yenyewe haikubaliani na hoja zao isipokuwa moja tu ya hakuna ushahidi.
 
Kutoamini si imani bali ni msimamo wa kutosadiki jambo hadi ushahidi wa kutosha utolewe. Ukosefu wa ushahidi si ushahidi wa kutokuwepo, lakini ni sababu tosha ya kukataa madai hadi yatakapothibitishwa. Si kupinga, ni kutosadiki.


Mawazo yanaonekana kwa athari zake zinazothibitika . Dini na ibada hazithibitishi Mungu kama kiini cha athari hizo ila ni tafsiri ya binadamu. Miungu mingi imetajwa kihistoria, zote zikiwa na ibada na maandiko. Je, zote ni kweli kwa sababu ziliathiri jamii?


Na kuhusu joka lisiloonekana darini ni kwamba ikiwa mtu anadai liko pale, ni wajibu wake kutoa ushahidi, si wangu kupanda darini kuthibitisha halipo. Madai ya ajabu yanahitaji ushahidi wa ajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…