Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Uelewa wa Mungu hautokani na utafiti wa kisayansi, kwani sayansi inachunguza vitu vinavyoonekana na kupimika. Mungu, kwa asili ya dhana hiyo, ni metaphysical—yani yuko juu au nje ya ulimwengu wa kimaumbile.

Chanzo cha dhana hiyo ni mchanganyiko wa:

Nadharia za kifalsafa: Wanafalsafa kama Aristotle walizungumza juu ya “The Unmoved Mover” – kilichoanzisha kila kitu bila chenyewe kuanzishwa.

Imani za kidini na tamaduni. Mila na maandiko ya dini nyingi kama Uyahudi, Ukristo, na Uislamu humuwasilisha Mungu kama chanzo cha kila kitu, mwenye akili, asiye na mwanzo wala mwisho.

Uchunguzi wa kiakili (reasoning). Baadhi ya watu hufikia wazo la Mungu through logical inference—kama vile hoja ya "First Cause" (Sababu ya kwanza) au "Design Argument" (Hoja ya mpangilio).

Mimi nimejifunza kuhusu dhana ya Mungu kutoka kwenye baadhi ya maandiko,, vitabu vya falsafa, Biblia, maandiko ya kihistoria, na mijadala ya kisayansi na kijamii.

Kwahiyo Mungu hakugunduliwa kama sayari mpya—bali ni dhana iliyojengwa, kupitishwa, na kuboreshwa na vizazi vya wanadamu kupitia tafakari, imani, na uzoefu wa ndani.

God is not seen with eyes, but sensed through reason, spirit,
and tradition.

UMEELEWA??
Nimeelewa vizuri kabisa, umekubali kwamba Mungu hajagunduliwa bali amejengwa tu kichwani — kwamba ni dhana ya binadamu, si uhalisia.

Umesema Mungu “hakugunduliwa kama sayari mpya bali ni dhana iliyojengwa, kupitishwa, na kuboreshwa na vizazi vya wanadamu.” Kwa kusema hivyo, umejiondoa mwenyewe kwenye msingi wa ukweli wa kisayansi au kihalisia.

Kitu kilichojengwa na binadamu kupitia tafakari, mila, na maandiko ya kale— bila msingi wa uchunguzi huru, wa moja kwa moja au ushahidi usiopingika — ni dhana ya kiutamaduni, si ukweli wa kuufanya kuwa wa lazima.

Hii inamaanisha kuwa Mungu, kama unavyomweleza, si kiumbe halisi aliyejitambulisha kwa uhakika, bali ni njia ya binadamu kujibu maswali ambayo hawakuwa na majibu yake kwa wakati huo.

Hoja ya “First Cause” au “chanzo kisicho na mwanzo” ni hoja ya zamani ya kifalsafa, lakini haina ulazima wa kumhusisha Mungu ambaye unamtaja kama mwenye akili, nia na mapenzi.

Tunachojua ni kwamba ulimwengu upo — lakini hatujui kwa uhakika ulianzia wapi au kwa nini. Kukosa jibu kamili hakumaanishi tunaruhusiwa kuweka jibu la imani (Mungu) mahali pa pengo hilo bila kutoa maelezo ya kina.

Huo ni mtego wa kimantiki ujulikanao kama "God of the Gaps" — kutumia Mungu kufunika kile tusichokijua. Katika historia, kila mara binadamu waliposhindwa kuelewa jambo, walitunga kiumbe au roho ili kueleza mfano zilipopiga Radi walisema Mungu anapiga ngoma. Lakini ujinga wa wakati huo si ushahidi wa kuwepo kwa Mungu.

Umetetea hoja yako kwa kusema Mungu ni "metaphysical" — yaani haonekani, hapimiki, yuko nje ya upeo wa sayansi. Hili linaonekana kama kinga ya hoja, lakini kwa kweli ni udhaifu. Kama kitu hakiwezi kuonekana, kupimika, kuchunguzwa, wala kujidhihirisha kwa njia yoyote — basi kimantiki, hakiwezi kutofautishwa na kitu kisichokuwepo.

Tunahitaji kuweka mipaka, kama hatuwezi kuthibitisha kitu, tusidai kuwa ni ukweli. Tunaweza kukikubali kama imani, lakini si kama maarifa. Kwa hiyo, kudai Mungu yupo kwa sababu ya “hisia, mila na reasoning” si ushahidi — ni urithi wa fikra.
 
Mkuu usiniulize mimi kwasababu mimi sijui.

Nadhani hiyo logic haujaielewa vizuri, first, not all truths are scientific. Kuna ukweli wa kihisia, wa kiakili (rational), wa kiroho, na hata wa kimaadili (moral truths) ambao haupimiki kwa “data” lakini bado una uzito mkubwa katika maisha ya mwanadamu.

Kusema kwamba Mungu ni “concept ya binadamu” kwa sababu hatuwezi kumpima kisayansi ni sawa na kusema upendo haupo kwa sababu huwezi kuuona kwenye microscope. Absence of physical proof is not proof of absence. Kuna mambo mengi ya metaphysical tunayoyakubali ,,kama uwepo wa nafsi au dhamiri bila ya kuwa na "material proof."

Kuhusu "God of the gaps" — ni kweli kumtumia Mungu kufunika ujinga wetu ni tatizo. Lakini hilo halifuti uwezekano wa kuwepo kwa Mungu. Kutokujua chanzo cha ulimwengu hakumaanishi Mungu hayupo ,, . So, we must remain open.

Na kuhusu hoja ya kwamba “Mungu hajajidhihirisha kwa uhakika,” that’s a matter of perspective. Wengine wanadai wamemwona katika maisha yao, kupitia maombi, miujiza, au mabadiliko ya tabia. Huwezi kupima experience ya mtu kwa ruler ya maabara.

Kusema Mungu ni fikra ya binadamu pekee ni kukwepa ukweli kwamba kuna maswali makubwa yanayohitaji majibu ambayo sayansi pekee haiwezi kuyatoa. Reasoning, tradition, experience, and yes — faith — ni njia halali za kutafuta ukweli.

SIJUI NAELEWEKA MKUU?
 
Kufuatia maelezo hayo mazuri, sasa turudi kwenye hoja yenyewe: neno "Mungu", kwa sabubu hatuwezi kuthibitisha jambo fulani ni ukweli au ni uongo bila kujua nini maana ya jambo hilo.

Neno "Mungu" maana yake ni nini au Mungu ni nini?
Sahihi, hatuwezi kuanza kuthibitisha au kukataa jambo bila kwanza kuelewa maana yake.

Msimamo wangu ni kwamba mjadala kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu hauna maana yoyote mpaka pale tutakapokuwa na maelezo ya wazi, sahihi, na yanayoweza kueleweka kwa njia ya mantiki kuhusu neno 'Mungu'.

Bila kufafanua vizuri maana ya neno hilo, hatuwezi hata kuanza kuchambua hoja kwa misingi ya ukweli, ushahidi, au uthabiti wa kimantiki.

Kwa hiyo kabla ya chochote kingine, ningependa mtu atoe tafsiri bayana ya Mungu anayemzungumzia.

Labda je ulikua unajua maana yake kulingana na Imani yako?
 
Nadhani hiyo logic haujaielewa vizuri, first, not all truths are scientific. Kuna ukweli wa kihisia, wa kiakili (rational), wa kiroho, na hata wa kimaadili (moral truths) ambao haupimiki kwa “data” lakini bado una uzito mkubwa katika maisha ya mwanadamu.

Kusema kwamba Mungu ni “concept ya binadamu” kwa sababu hatuwezi kumpima kisayansi ni sawa na kusema upendo haupo kwa sababu huwezi kuuona kwenye microscope. Absence of physical proof is not proof of absence. Kuna mambo mengi ya metaphysical tunayoyakubali ,,kama uwepo wa nafsi au dhamiri bila ya kuwa na "material proof."

Kuhusu "God of the gaps" — ni kweli kumtumia Mungu kufunika ujinga wetu ni tatizo. Lakini hilo halifuti uwezekano wa kuwepo kwa Mungu. Kutokujua chanzo cha ulimwengu hakumaanishi Mungu hayupo ,, . So, we must remain open.

Na kuhusu hoja ya kwamba “Mungu hajajidhihirisha kwa uhakika,” that’s a matter of perspective. Wengine wanadai wamemwona katika maisha yao, kupitia maombi, miujiza, au mabadiliko ya tabia. Huwezi kupima experience ya mtu kwa ruler ya maabara.

Kusema Mungu ni fikra ya binadamu pekee ni kukwepa ukweli kwamba kuna maswali makubwa yanayohitaji majibu ambayo sayansi pekee haiwezi kuyatoa. Reasoning, tradition, experience, and yes — faith — ni njia halali za kutafuta ukweli.

SIJUI NAELEWEKA MKUU?
Mkuu, Hoja zako zinahitaji mtu kukubali "Mungu" ni dhana halali hata kabla ya kuijadili. Lakini hilo ndilo tatizo kuu ninalolizungumzia kama ignostic.

Sijasema kuwa kila kitu lazima kipimwe na microscope - Wewe ndiye unaamini hivyo sio mimi na unalazimisha mimi niamini kama wewe, Sorry I can't.

Nimesema kabla ya kujadili kama "Mungu yupo au hayupo", ni lazima kwanza dhana ya "Mungu" iwe imeelezwa kwa njia isiyoegemea upande wowote—yenye consistency ya kifalsafa.

Kwani wewe hutambui kwamba kabla ya mjadala wowote let say "Ajali za barabarani" lazima uanze ufafanuzi wa hiyo dhana kisha ndipo mjadala wa chanzo cha hizo ajali uanze.

Tuseme Mungu ni “chanzo kisicho na mwanzo chenye akili” — hiyo ni tafsiri, siyo maana ya neno hilo kwa ujumla.

Tafsiri yako inategemea rational na metaphysical tradition, ambazo zinatofautiana baina ya watu na tamaduni. Hivyo basi, tafsiri hiyo haiwezi kuchukuliwa kama msingi wa mjadala huru bila kuhojiwa.

Na kuhusu kusema kuwa - Kuna ukweli wa kihisia, wa kiroho, wa kiakili na wa kimaadili hakufanyi moja kati ya hizo kuprove “Mungu” anayeongelewa ni real au ni abstract idea yenye thamani ya kisaikolojia tu.

Ukitaja miujiza, mabadiliko ya tabia, au maombi yanayojibiwa — kuna maelezo mbadala yanayothibitika, yasiyo ya kidini ambayo yanaweza kuelezea mambo hayo bila kuhitaji dhana ya Mungu.

Je, tukichunguza ushahidi huo wote bila kutumia neno "Mungu," bado utathibitisha kuwepo kwa kitu hicho kisichoelezeka vizuri?

Kusema kwamba Mungu ni wazo la binadamu ni kukwepa maswali makubwa ni sawa na kusema "Kumuweka Mungu kama jibu kwa maswali hayo ni kukwepa kazi ya kuyatafakari kwa kina.”

Kama Mungu anazungumziwa, basi aelezwe kwanza kwa lugha ya uwazi isiyotegemea imani au hisia — ndipo tuanze mjadala.

Kama huwezi kutoa maana ya "Mungu" isiyotegemea Hisia, Imani na Makisio ya watu tofauti ni afadhali ukapotea kimya kimya - mimi ninahekima nitaelewa.
 
Kwako:
Ujuzi maana yake ni nini?
Uwezo maana yake ni nini?
Upendo maana yake ni nini?
Hayo ni maswali kwenu mnaosema kuna Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote.

Si maswali kwangu niliyeambiwa kuwa Mungu wenu ana sifa hizo.

Niambie maana yake, thibitisha Mungu yupo na ana sifa hizo.

Kama huwezi ku define hizo sifa, hujui hata sifa za Mungu wako na hivyo huwezi kusema yupo.
 
Kama unahitaji hundred percent certainty kabla ya kuamini kitu, basi huenda hata hujui kama mama yako ni mama yako kweli — unless uwe umewahi kufanya DNA test mwenyewe?

Ukiuliza uhakika wa kwamba Mungu aliumba ulimwengu, ni kama mtu kuuliza uhakika kwamba mwandishi fulani aliandika kitabu wakati anaangalia hicho kitabu mikononi. Ulimwengu una order, complexity, na harmony kiasi ambacho kusema “ilimake tu yenyewe” ni kama kusema iPhone ilijiunda yenyewe baada ya volcano kulipuka karibu na Apple HQ.

Kuhusu philosophers ,hawa jamaa hawakukaa miaka mingi wakivuta bangi ya mawazo tu. Kina Aquinas, Descartes, Leibniz walipiga hesabu nzito and that's why Walisema hivi kwa kifupi

"Anything that begins to exist has a cause. The universe began to exist. Therefore, the universe has a cause — and that cause is something beyond space, time, and matter… which is basically what we mean by God."

But najua itapinga, sasa ukipinga, uje na jibu kabisa kuwa ni kitu gani hicho kilicho anzisha time yenyewe?

Hiyo line yako ya "imani inaweza kuwa ya uongo" ni kama kusema “mapenzi yanaweza kuwa ya uongo,” lakini bado unalia ukiachwa. Kwa hiyo, ikiwa uongo waweza kuwa na nguvu hivyo, vipi kuhusu ukweli? Don’t underestimate genuine faith just because fakes exist — hata pesa bandia zipo kwa sababu kuna original.

Kwa hiyo , kabla hujatupa imani kama karatasi ya toilet, jiulize: Je, hoja zako za kutokuamini zina nguvu kuliko hoja za kuamini? Au unafanya tu “intellectual gymnastics” ili uendelee kula maisha bila accountability?

Imani ya kweli haiji kwa kuona tu, inakuja kwa kufikiri, kutafakari, na kukubali kwamba huwezi kuwa chanzo cha kila kitu kwa akili yako yenye mipaka. Kama huwezi kujieleza ulianzia wapi, usijione mtaalamu wa kueleza ulimwengu ulianzaje.

Na kama bado unauliza uhakika wa Mungu kama vile unatafuta receipt ya creation, basi hujaelewa kwamba faith is not blindness — it’s trust built on reason, not ego

Chew on that.
When exactly did the universe begin to exist?
 
"God doesn't need anyone to speak for Him
Then why are you speaking on behalf of him?
, but people share their understanding of Him based on faith, experience, and scripture. Just like love or justice, not everything true needs to appear physically to be real.
How do you prove your understanding about God is true?
 
Mungu doesn't exist (mungu hayupo na hajawahi kuwepo) sijuwi kwanini watu bado wana amini hizi stori za uongo.
Ngono za uwepo wa mungu ni binadamu tu aliyetunga baada ya kuanza kuwa civilized na kugundua lugha. Ndo mana ile miungu ya zamani ilikuwa inaonekana na ilikuwa na maumbile ya binadamu( binadamu wa kale walimtengeneza mungu Kwa fikra zao). Ila mungu hayupo
 
Mkuu, Hoja zako zinahitaji mtu kukubali "Mungu" ni dhana halali hata kabla ya kuijadili. Lakini hilo ndilo tatizo kuu ninalolizungumzia kama ignostic.

Sijasema kuwa kila kitu lazima kipimwe na microscope - Wewe ndiye unaamini hivyo sio mimi na unalazimisha mimi niamini kama wewe, Sorry I can't.

Nimesema kabla ya kujadili kama "Mungu yupo au hayupo", ni lazima kwanza dhana ya "Mungu" iwe imeelezwa kwa njia isiyoegemea upande wowote—yenye consistency ya kifalsafa.

Kwani wewe hutambui kwamba kabla ya mjadala wowote let say "Ajali za barabarani" lazima uanze ufafanuzi wa hiyo dhana kisha ndipo mjadala wa chanzo cha hizo ajali uanze.

Tuseme Mungu ni “chanzo kisicho na mwanzo chenye akili” — hiyo ni tafsiri, siyo maana ya neno hilo kwa ujumla.

Tafsiri yako inategemea rational na metaphysical tradition, ambazo zinatofautiana baina ya watu na tamaduni. Hivyo basi, tafsiri hiyo haiwezi kuchukuliwa kama msingi wa mjadala huru bila kuhojiwa.

Na kuhusu kusema kuwa - Kuna ukweli wa kihisia, wa kiroho, wa kiakili na wa kimaadili hakufanyi moja kati ya hizo kuprove “Mungu” anayeongelewa ni real au ni abstract idea yenye thamani ya kisaikolojia tu.

Ukitaja miujiza, mabadiliko ya tabia, au maombi yanayojibiwa — kuna maelezo mbadala yanayothibitika, yasiyo ya kidini ambayo yanaweza kuelezea mambo hayo bila kuhitaji dhana ya Mungu.

Je, tukichunguza ushahidi huo wote bila kutumia neno "Mungu," bado utathibitisha kuwepo kwa kitu hicho kisichoelezeka vizuri?

Kusema kwamba Mungu ni wazo la binadamu ni kukwepa maswali makubwa ni sawa na kusema "Kumuweka Mungu kama jibu kwa maswali hayo ni kukwepa kazi ya kuyatafakari kwa kina.”

Kama Mungu anazungumziwa, basi aelezwe kwanza kwa lugha ya uwazi isiyotegemea imani au hisia — ndipo tuanze mjadala.

Kama huwezi kutoa maana ya "Mungu" isiyotegemea Hisia, Imani na Makisio ya watu tofauti ni afadhali ukapotea kimya kimya - mimi ninahekima nitaelewa.
Unadai kwamba kabla ya mjadala kuhusu kuwepo kwa Mungu, lazima kwanza niwe na definition isiyoegemea upande wowote ???

Hilo haliwezekani (impossible burden). Hakuna dhana yoyote kubwa—iwe ni “justice,” “love,” “freedom,” au hata “consciousness”—inayoweza kueleweka bila muktadha wa kitamaduni, kihistoria au falsafa. Kwa hiyo kuhitaji definition ya “Mungu” isiyoguswa na imani, hisia au historia ya binadamu ni kutaka kuwa na mjadala usio kuwa na mantiki yoyote.

You’re asking for a metaphysical concept to be framed like a scientific variable — that’s a category error.

Na kuhusu kusema kuwa “Mungu” hawezi kuwa tafsiri ya binadamu kwa sababu zipo tafsiri tofauti — hiyo ni sawa na kusema “maana ya neno ‘uhuru’ si halali kwa kuwa kila mtu anaiona tofauti.” Lakini tafsiri nyingi hazifuti uhalali wa kujadili dhana hiyo; zinaitajika ili kufanikisha mjadala.

Hoja yako ya kusema "tusitumie neno Mungu kuchunguza ukweli" ni kama kusema “tusitumie neno ‘akili’ kuchunguza consciousness kwa sababu akili haieleweki kwa pamoja.”

Hii si hoja ya ignosticism tu,,ni denial disguised as epistemic purity. Unahitaji kila mtu atupilie mbali uzoefu, historia, falsafa na maadili ili tuanze kwenye “blank slate” ambayo haipo katika uhalisia wa binadamu.

Kama unadai tusijadili Mungu hadi upate definition "pure," basi hata hutaki mjadala, na unataka kusitisha mjadala kwa sababu hoja zako ni dhaifu sana.

Na hiyo si hekima.Hiyo ni episte
mic evasion.
 
Then why are you speaking on behalf of him?

How do you prove your understanding about God is true?
Just like gravity, or thoughts ,you don't see them, but you see their effects. The existence of God isn’t about Him standing in front of you with an ID card. It’s about the evidence in creation, order in the universe, morality, and the personal experiences people have.

Your doubt doesn't cancel His existence ,,, it just exposes your limited lens.
 
Sahihi, hatuwezi kuanza kuthibitisha au kukataa jambo bila kwanza kuelewa maana yake.

Msimamo wangu ni kwamba mjadala kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu hauna maana yoyote mpaka pale tutakapokuwa na maelezo ya wazi, sahihi, na yanayoweza kueleweka kwa njia ya mantiki kuhusu neno 'Mungu'.

Bila kufafanua vizuri maana ya neno hilo, hatuwezi hata kuanza kuchambua hoja kwa misingi ya ukweli, ushahidi, au uthabiti wa kimantiki.

Kwa hiyo kabla ya chochote kingine, ningependa mtu atoe tafsiri bayana ya Mungu anayemzungumzia.

Labda je ulikua unajua maana yake kulingana na Imani yako?
Ye yote makini atajiuliza: kwa nini au sababu gani zinazofanya mtu aseme kuna Mungu? Pia mtu anapoita neno Mungu ana maanisha nini? Na je, sababu za haya yote ni nini: ni ulimwengu umetoka wapi na unaenda wapi?
 
Unauliza "Mungu ni nini?” Aisee, huo ni mtego classic wa watu mnaojifanya thoughtful. Mungu siyo toothbrush mpaka umuelezee kwa manual. He is not a cosmic vending machine ya kutupa blessings tukitupa maombi. Tunamuita Mungu maana wanajua kuna nguvu isiyoelezeka, ambayo haibadiliki kila jioni kama mood ya ex wako.

Na kuhusu “ulimwengu umetoka wapi na unaenda wapi,” bro, ulimwengu hauna Google Maps. Hatuna destination pinned kwenye sayari ya mwisho. Lakini kama kila kitu kina mwanzo, kuna logic kusema lazima kuna Chanzo – ni kama vile microwave haianzi tu kupika chakula bila mtu yoyote kubonyeza start. Unless unadhani tunaishi kwenye episode ya Rick and Morty permanently, logic bado inafanya kazi.

Kwa hiyo mtoa hoja, before uanze kuuliza maswali ya “existential” kama vile unaandika script ya documentary ya Netflix, pengine uliza pia: kama hakuna Mungu, kwa nini unauliza maswali kama haya kana kwamba kuna majibu makubwa yakusubiri?

Au labda unatafuta tu reason ya ku-ignore mamlaka ya juu ili uendelee kuishi kama universe iko kwenye payroll
yako.???
 
Mkuu, kama umeweza kujiiza maswali hayo basi wewe ni miongoni mwa binadamu wachache wasiotaka kuwekewa ukomo kwenye kufikiri.

Watu wanaopenda kuhitimisha vitu kwa lojiki na mantiki ili kupata majibu ya kuridhisha.

Afadhali kusimama upande wa kusema hujui, kuliko kusema unajua halafu unashindwa kuelezea.
 
Kuhusu Mungu ni nini au neno Mungu maana yake ni nini? Nakubaliana na maana ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki, ambayo imeeleza maana ya Mungu kuwa ni neno tunaloita "Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili".
 
Aisee, hongereni kwa kusimama upande wa 'sijui',,huo ni msingi mzuri wa kutokujifunza kabisa. Kwa sababu kila ukikutana na jambo gumu, suluhu ni kujifunika blanketi la 'sina majibu' na kulala kwa raha.

Unajua, akili ya kufikiri bila mipaka ni nzuri sana, mpaka inapoanza kuzunguka bila dira kama mlevi. Wanaopenda lojiki na mantiki wanaelewa kuwa hata kutokuwa na jibu ni sehemu ya mchakato wa kupata jibu,,lakini siyo kibali cha kubweteka.

Kusema hujui ni ujasiri, sawa. Lakini kama kila siku unasimama kwenye mstari wa 'sijui' bila kutafuta kuelewa, basi wewe hauna tofauti na msafiri aliyekataa ramani kwa madai ya kupenda msitu.

Mtu wa kweli hupenda ukweli, hata kama ni mgumu. Lakini kudai hamtaki mipaka ya fikra huku mnakimbia mantiki, mnakuwa hamna tofauti na dereva dereva anayetaka uhuru wa barabara bila sheria, halafu alalamike gari likipinduka.
 
Safi kabisa kwa kulitambua hilo...
 
Unadai kwamba kabla ya mjadala kuhusu kuwepo kwa Mungu, lazima kwanza niwe na definition isiyoegemea upande wowote ???

Hilo haliwezekani (impossible burden). Hakuna dhana yoyote kubwa—iwe ni “justice,” “love,” “freedom,” au hata “consciousness”—inayoweza kueleweka bila muktadha wa kitamaduni, kihistoria au falsafa. Kwa hiyo kuhitaji definition ya “Mungu” isiyoguswa na imani, hisia au historia ya binadamu ni kutaka kuwa na mjadala usio kuwa na mantiki yoyote.

You’re asking for a metaphysical concept to be framed like a scientific variable — that’s a category error.

Na kuhusu kusema kuwa “Mungu” hawezi kuwa tafsiri ya binadamu kwa sababu zipo tafsiri tofauti — hiyo ni sawa na kusema “maana ya neno ‘uhuru’ si halali kwa kuwa kila mtu anaiona tofauti.” Lakini tafsiri nyingi hazifuti uhalali wa kujadili dhana hiyo; zinaitajika ili kufanikisha mjadala.

Hoja yako ya kusema "tusitumie neno Mungu kuchunguza ukweli" ni kama kusema “tusitumie neno ‘akili’ kuchunguza consciousness kwa sababu akili haieleweki kwa pamoja.”

Hii si hoja ya ignosticism tu,,ni denial disguised as epistemic purity. Unahitaji kila mtu atupilie mbali uzoefu, historia, falsafa na maadili ili tuanze kwenye “blank slate” ambayo haipo katika uhalisia wa binadamu.

Kama unadai tusijadili Mungu hadi upate definition "pure," basi hata hutaki mjadala, na unataka kusitisha mjadala kwa sababu hoja zako ni dhaifu sana.

Na hiyo si hekima.Hiyo ni episte
mic evasion.

Nakazia tena tusijadili “Mungu” hadi tupate definition “pure” isiyoegemea upande wowote.

Acha kuzunguka zunguka kwenye historia, imani na mafundisho ya falsafa za kale — basically, nataka ufanye brain factory reset kabla ya mjadala ili uweze kufree think hiyo dhana broh 🧠

Mbona tukiacha tafsiri za falsafa na Imani bado We can sense love, hate, hot, heat - We can see things moving and we can feel them. why ikija kujadili "Mungu" lazima tuegemee fasiri za kiimani na kihistoria bila kujali hatumuoni, hatumfeel, Hatumsense wala hatuthink obout Him/Her/It.

Hiyo si mantiki, hiyo ni epistemic gymnastics ya mtu anayejua hoja zake hazina uzito kama tu akijaribu kutoa ukungu wa kiimani.

Kwanza, hakuna dhana kubwa inayokubalika kwa wote bila tafsiri tofauti — hata “uhuru” au “upendo” hazina muundo rasmi — lakini bado tunajadili na zina tafsiri.

Sasa kama tafsiri nyingi za “Mungu” lazima zitegemee imani bila ushahidi, hicho ni kisingizio cha kunyamazisha mjadala kwakua tu nimesema tupate maana ndipo mjadala uanze, Infact huna hoja — unajaribu kuogelea kwenye bwawa la kifilosofa tu.

Halafu hiyo ya kusema “tusitumie neno Mungu kuchunguza ukweli kwa sababu halijaeleweka vizuri” ni kama kusema tusitumie “akili” kuelewa consciousness.

Yaani unataka tufute tools kwa sababu haziko sterile vya kutosha kwa hadhi yako ya imaginary neutrality? That’s not deep thinking, that’s intellectual catwalking.

Watu wanajenga hoja, wewe unajenga mistari ya kujificha. Ukiulizwa “Mungu ni nini?” unarudi na emotions na mistari ya Nacha kwenye ile ngoma yake ya spoken word poetry — unafanya mjadala uwe ni endless spoken word night.

Tafsiri tu imekushinda na umedata — na hapo bado hatujazama deep kutaka kujua alikotoka. Tayari umekuwa emotional, unaanza kuchanganya logics na feelings kama assignment ya mwanafunzi wa Form Two aliyeamka saa kumi kuandika speech ya debate.

Mjadala hauanzi kwa kutengeneza mazingira yasiyowezekana — huo ni uzembe wa kufikiri uliopakwa rangi ya “neutrality.” Kama huwezi define, Hujui unachojadili, Simple.

Nasisitiza usilete maelezo yeyote mengi yasiyo na tija, Njoo direct na maana ya "Mungu" itayoweza kueleweka na kila mtu isiyoegemea tafsiri za kiimani inayohisika, fikirika, oneka, shikika, onjeja au kusikika.

Otherwise itakua tunafanya circular reasoning ni sawa na kusombelea maji kwa kutumua roba la katani.
Aisee, hongereni kwa kusimama upande wa 'sijui',,huo ni msingi mzuri wa kutokujifunza kabisa. Kwa sababu kila ukikutana na jambo gumu, suluhu ni kujifunika blanketi la 'sina majibu' na kulala kwa raha.

Unajua, akili ya kufikiri bila mipaka ni nzuri sana, mpaka inapoanza kuzunguka bila dira kama mlevi. Wanaopenda lojiki na mantiki wanaelewa kuwa hata kutokuwa na jibu ni sehemu ya mchakato wa kupata jibu,,lakini siyo kibali cha kubweteka.

Kusema hujui ni ujasiri, sawa. Lakini kama kila siku unasimama kwenye mstari wa 'sijui' bila kutafuta kuelewa, basi wewe hauna tofauti na msafiri aliyekataa ramani kwa madai ya kupenda msitu.

Mtu wa kweli hupenda ukweli, hata kama ni mgumu. Lakini kudai hamtaki mipaka ya fikra huku mnakimbia mantiki, mnakuwa hamna tofauti na dereva dereva anayetaka uhuru wa barabara bila sheria, halafu alalamike gari likipinduka.
Mkuu mimi sijui, Hivyo ninapokutana na mtu anayekiri anajua lazima nimuhoji ili nijue.

Nikipata majibu ya kuridhisha niko tayari kubadilika kuwa upande wowote kati ya "Theist" au "Atheist" ikiwa kutakua na hoja zenye nguvu.

Lakini ukitoa majibu yasiyopatana na mantiki na lojiki nakuchapa, maswali ukishindwa - nakuweka kwenye kundi la wasiojua.

Infact mpaka sasa sijapata majibu ya kuridhisha ya dhana "Mungu" ambayo inaridhisha, inafikirika, oneka, shikika, sikika, hisika au nusika.

Kama zinavyofikirika na kuhisika dhana nyingine tata like Upendo, Consciousness au Mind.

This is it.
 
Kama kitu;
•Hakifikiriki,
•Hakihisiki,
•Hakishikiki,
•Hakionjeki,
•Hakionekani na
•Hakisikiki.

•Na hakuna njia ya kuathiri wala kuathiriwa nacho...

Basi kwa viwango vyote vya falsafa, sayansi, na mantiki ya kawaida ya binadamu — hicho kitu hakipo.

Au kama kiko, basi ni kama vile hakipo, kwa sababu hakina uhusiano wowote na uhalisia wetu.

Isipokuwa watu huchomeka neno "imani" ili kukiweka kwenye mawasiliano — lakini ukiondoa imani, hakiachi alama yoyote.

Na kama hakiachi alama yoyote — ni dhana tupu isiyo na uzito wa kiakili wala wa kweli.

Mimi sijui, lakini niko tayari kujifunza.

Ukijua, nipe hoja ya kueleweka; ukijidai kujua halafu hoja zako ni dhaifu, nakuweka kwenye kundi la wasiojua pamoja nami.
 
Back
Top Bottom