Notorious_Marcc
JF-Expert Member
- Feb 16, 2024
- 2,598
- 6,147
ExactlyPoint yangu ndio ilikuwa kama yako, akili ya mwanadamu ndio chanzo cha matatizo au furaha yake
ExactlyPoint yangu ndio ilikuwa kama yako, akili ya mwanadamu ndio chanzo cha matatizo au furaha yake
We chagua Moja tu acha kupoteza muda wako hili swali mpaka INAKUFA hutopata jibu.Wapo wanaoamini kuwa Mungu yupo – Muumba wa kila kitu, mwenye uwezo wa kubadilisha chochote.
Lakini wapo pia wanaoamini hakuna Mungu, na maisha haya ni matokeo ya mabadiliko ya asili, bahati, na akili ya binadamu.
Swali linakuja:
Kama Mungu yupo kweli, kwa nini kuna mateso, vita, magonjwa, vifo vya watoto wasio na hatia?
Na kwa upande mwingine:
Kama hakuna Mungu, binadamu anajiongoza kwa misingi gani? Maadili yanatoka wapi? Haki ni nini bila Mungu?
---
Maswali kwa mjadala:
Unaamini Mungu yupo au hakuna? Kwa nini?
Kama huamini, maisha yako yanapata maana wapi?
Kama unaamini, unawezaje kuelezea uwepo wa maovu na mateso?
Je, dini ni njia ya watu kutuliza hofu yao ya kifo au ni kweli kuna nguvu ya juu isiyoonekana?
Kutokujua chanzo cha kitu si ushahidi kwamba hakikuumbwa. Kusema “ulimwengu upo tu” bila kueleza kwa nini au vipi ni sawa tu na kusema “Mungu yupo tu— zote ni statements zinazohitaji msingi wa hoja.Kwani lazima ulimwengu uwe umeumbwa?
Kama kila kitu lazima kiwe kimeumbwa, Je muumbaji wa kila kitu aliumbwa na nani?
Sikuwepo na wala wewe hukuwepo.
Wote tumezaliwa ndani ya ulimwengu ambao tayari upo.
Wewe unayedai Mungu ndio muumba wa ulimwengu unatakiwa uthibitishe madai yako.
Thibitisha Mungu ndiye muumba wa ulimwengu.
Na si imani zako ulizo aminishwa na kupumbazwa.
Nilishakwambia, Mimi siamini kwenye kuamini. Sihitaji kuamini.
Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.
Mungu na Big-Bang ni nadharia za kubuni na kufikirika tu, Hazina ushahidi wala uthibitisho wowote ule.
Ni nadharia zisizo jitosheleza.
Ulimwengu tayari upo. Na si lazima kwamba uliumbwa.
Ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo milele.
Hakuna anayefahamu ulimwengu ulianzaje.
Habari za Mungu na Bing- Bang ni theory uchwara zisizo na uthibitisho wala ushahidi wowote ule.
Mateso ni nini?Injustice doesn't cancel God's justice. Mateso yapo kwa sababu ya uhuru wa mwanadamu (free will), dhambi, na pia kama sehemu ya majaribio ya kiimani.
God allows suffering not because He is unjust, but because through suffering, character is shaped, imani inaimarika, na watu hujifunza rehema, upendo, na uvumilivu.
"Maana mateso ya sasa si kitu kama tutakayofunuliwa baadaye." Warumi 8
Kwa hivyo, Mungu huruhusu mateso kwa sababu ana mpango mkuu unaopita uelewa wetu wa sasa, na kwa kila maumivu, kuna kusudi.
Mateso ni maumivu yanayomgusa mtu ndani au nje, yanayomtengeneza au kumvunja—depending on how he responds.Mateso ni nini?
Nakushukuru kwa kushiriki katika mjadala huu wa kina. Kama waumini wa mantiki, tunathamini sana jitihada zako kueleza uwezekano wa Mungu kupitia dhamiri, maana, na mpangilio wa asili.Swali lako lina mantiki,, haswa kutokana mtazamo wa agnosticism na stoicism, ambao unathamini reason, virtue, na natural order kuliko imani isiyo na ushahidi.
“Kwa nini Mungu hajifunui kwa njia ya wazi kama jua au nguvu ya uvutano?”
Sheria za asili kama gravity au seasonal cycles zinaweza kuonekana, kupimwa, na kuthibitishwa—lakini je, kila kitu cha muhimu lazima kiwe kinapimika kwa vipimo vya maabara?
Fikiria vitu kama upendo, maumivu ya ndani, au thamani ya maisha—vipo, vinaathiri maisha ya kila mtu, lakini haviwezi kupimwa au kuonekana moja kwa moja. Existence ya Mungu inaweza kuwa ya namna hii: not a material object, bali a metaphysical reality. Siyo kila ukweli lazima uwe wa kisayansi (empirical) ili uwe halisi.
"Kama Mungu ni muumba wa nature, basi anaweza kuwa zaidi ya nature yenyewe (transcendent), na hawezi kudhibitika kwa kanuni zile zile alizoziweka kwa viumbe."
– C.S. Lewis aliwahi kusema: “To expect God to be obvious to us is like expecting Shakespeare to appear in Hamlet’s play as a character.”
"Circular reasoning kutumia maandiko kuthibitisha Mungu."
Kutumia Biblia kuthibitisha Mungu halafu kusema Mungu ndiye aliyetupa Biblia ni circular.
Lakini wengi wanaamini kwamba revelation ya Mungu ina ngazi mbili:
General revelation (ufunuo wa asili): conscience, moral awareness, desire for meaning, awe before the universe (ambayo hata Stoics waliheshimu).
Special revelation (maandiko, manabii, nk): ambayo ni ya historia fulani, lakini hujaribu kueleza kwa undani chanzo cha ufunuo huo wa asili.
Kwa hiyo, wanaosema “Biblia ni ushahidi wa Mungu” hawaanzi papo hapo—wanadai kwamba kuna maelezo ya kina ya yale mambo ya ndani tunayopitia ambayo hayawezi kuelezwa vizuri bila kupitishwa katika lensi ya kiroho.
Kwa mfano: Kiu ya haki, kusudi, na upendo usio na masharti (agape) ni vitu ambavyo haviwezi kuelezwa tu kwa survival instincts.
Kwa nini ufunuo wa Mungu uko localized kwenye jamii fulani?”
Kama Mungu ni wa wote, kwa nini asijifunue kwa namna ya universal accessibility?
Hoja moja inayojitokeza hapa ni kwamba mawasiliano yoyote ya maana yanahitaji muktadha fulani. Hata physics ilianza Mesopotamia, Ugiriki na India, lakini leo inahesabiwa kuwa ya dunia nzima. Vivyo hivyo, dini inaweza kuanzia kwa mtu au jamii fulani lakini isiwe imekusudiwa kwao tu.
“Particularity is not partiality.” – The fact that God spoke through Hebrew prophets doesn’t mean He rejected others, bali alianza na njia ambayo binadamu anaweza kuelewa.
Dini nyingi hutoa maadili mazuri—hii haithibitishi kwamba zote ni sawa, lakini huonyesha kwamba Mungu anaweza kuwa ameacha alama Yake kwa namna mbalimbali kwa jamii tofauti.
“Kwa nini dhamiri na kiu ya maana tuviite dalili za Mungu?”
Kama vile njaa ni ishara ya uhitaji wa chakula, na kiu ya maji ni dalili ya uwepo wa maji, basi:
Couldn’t the thirst for meaning, justice, transcendence, and love be evidence of something beyond ourselves?
Wanafalsafa kama Immanuel Kant na Alvin Plantinga walieleza kuwa moral obligation haielezeki kirahisi bila chanzo chenye mamlaka ya juu—maana mtu anaweza kuuliza: Kwa nini ni lazima niwe mwema, kama hakuna Nguvu ya Juu inayosema hivyo?
"Maadili yasiyo na hofu wala thawabu ndiyo ya kweli”
Ni kweli, maadili bora hayawezi kujengwa kwa misingi ya hofu au zawadi tu. Hapo Stoicism na hata Ukristo wa kweli wanakutana.
Yesu hakufundisha maadili kwa sababu ya jehanamu tu, bali aliwaita watu waishi kwa upendo wa kweli, haki, rehema, na kujikana nafsi. Katika hili, Stoics na Wakristo wanaweza kukubaliana kwamba uadilifu wa kweli unapaswa kuwa kwa ajili ya mema yenyewe.
“Kwa nini kuna dini nyingi kila moja ikisema ni ya kweli?”
Ukweli mmoja unaweza kuakisiwa kwa njia tofauti na zenye dosari. Kama watu 10 wakitazama jua kutoka pande tofauti, watatoa maelezo tofauti, lakini jua ni moja.
Pluralism haimaanishi kuwa hakuna ukweli, bali kwamba watu wanauona kwa mitazamo tofauti. Jukumu la kila mmoja ni kutafuta ule ukweli ambao unaendana na akili, moyo, historia na matokeo yake katika maisha halisi.
Japo huwezi “kumthibitisha” Mungu kwa microscope au lab, huwezi pia kumkataa kirahisi kwa vile hajajifunua kama graviti. Mungu, kama ni halisi, ni zaidi ya viwango vya majaribio ya binadamu, na njia ya Yeye kujifunua inaweza kuwa ya kina zaidi—kupitia dhamiri, kiu ya maana, historia, na hata mateso.
Imani si kinyume cha mantiki – ni kupanua mantiki hadi kwenye maeneo ambayo data za kawaida haziwezi kufika.
Unaweza kusema: “Sina ushahidi wa kutosha kusema Mungu yupo,” lakini pia kwa uaminifu wa kiakili unaweza kusema: “Sina ushahidi wa kutosha kusema Hana nafasi yoyote."
Mimi sijui ulimwengu ulianza vipi.Unasema eti, "Ulimwengu unaweza kuwa kitu kisicho na chanzo." Halafu hapo hapo unaukataa uwezekano wa Mungu kuwa necessary being, hiyo ni kama kusema "mimi siamini kwenye uchawi, lakini najua kuna wachawi." Unaamini katika kitu kisicho na chanzo, lakini unapinga dhana ya necessary being kwa sababu tu haikupendezi? Hiyo siyo deep thinking bro, hiyo ni intellectual gymnastics.
Ukisema "hao kina Leibniz, Aquinas, Craig Lane na Swinburne wanatoa opinions tu", basi hata wewe uko kwenye ligi yao — ya watu wanaotoa opinions. Kwa hiyo hoja zako siyo special, ni “maoni yako tu.” So usijifanye referee wakati na wewe ni mchezaji uwanjani.
Nimesema "Mungu yupo tu, siyo kwa bahati kama unavyosema, kama ulimwengu ni novel, lazima kuna mwandishi. Na kama unaona novel inaweza kujitunga yenyewe, basi hujui tofauti ya Stephen King na printer ya HP.
Bado hujajibu swali la msingi, kama kila kilichoanza kuwepo kina chanzo, na ulimwengu umeanza kuwepo, chanzo chake ni nini? Ukitaka kusema ulimwengu hauna chanzo, basically unadai kuna kitu kisicho na chanzo — hiyo hiyo unayopinga kwa Mungu.
You’re not rejecting God because of logic — you’re just rejecting Him because you don’t like the implications. Na hiyo ni fair, lakini siyo hoja ya kishujaa. Ni kama kusema "sitaki sheria ya mvutano kwa sababu siipendi." Gravitation haijali feelings zako.
Kwa hiyo, kama unataka kupinga existence ya Mungu, leta hoja zenye meno, si hizi za kusugua keyboard ukitegemea watu tuamini giza ni chanzo cha mwanga. 😎
Wewe una uhakika na ushahidi upi kwamba Mungu ndio kaumba ulimwengu?Kutokujua chanzo cha kitu si ushahidi kwamba hakikuumbwa. Kusema “ulimwengu upo tu” bila kueleza kwa nini au vipi ni sawa tu na kusema “Mungu yupo tu— zote ni statements zinazohitaji msingi wa hoja.
Big Bang si hadithi ya kufikirika – ni model ya kisayansi inayotegemea ushahidi wa observational, kama cosmic background radiation na redshift ya galaxies. Haijasema nini kilikuwa "kabla", lakini inaeleza vizuri jinsi ulimwengu ulivyo anza kupanuka.
Kusema kila kitu lazima kiwe na chanzo (cause) ni hoja yenye mantiki itayokuongoza hadi kwenye First Cause — ambacho hakikusababishwa na chochote kingine. Hii ndiyo hoja ya classic ya Cosmological Argument. Huwezi kusababisha msururu usio na mwisho wa sababu.
Kwa hiyo, ukisema:
"Hakuna aliyejua mwanzo wa ulimwengu" –ni
sawa, lakini pia usidai kwamba "ulimwengu haukuumbwa/hauna Muumbaji .
Hiyo nayo ni imani, sio maarifa.
Siyo kwamba tuna uhakika wa kila kitu, lakini kati ya kusema ulimwengu haukuumbwa bila ushahidi na kusema ulimwengu una chanzo fulani, labda Muumba, hoja ya pili ina uzito wa kifalsafa na kisayansi zaidi – hata kama si majibu yote yapo.
Not knowing is not a license to deny.
Kabla ya kuuliza kama Mungu yupo, tujiulize—tunaposema "Mungu", tunamaanisha nini?Nakushukuru kwa kushiriki katika mjadala huu wa kina. Kama waumini wa mantiki, tunathamini sana jitihada zako kueleza uwezekano wa Mungu kupitia dhamiri, maana, na mpangilio wa asili.
Hata hivyo, kama Agnostics-Ignostics, tunaamini kwamba mijadala kuhusu Mungu mara nyingi huzunguka dhana ambayo haijafafanuliwa vya kutosha hata kabla ya kuanza kuijadili— aidha kuikubali au kuikataa.
• Mara nyingi tunaombwa kumchukulia huyu Mungu kama wa kweli kabla hatujaelewa "Mungu" inamaanisha nini kwa njia ya wazi.
Sihitaji circular reasoning inayozunguka kwenye imani ili kumuelewa.
Nahitaji kuelezewa dhana ya “Mungu” kwa njia isiyotegemea maandiko, hisia, au mila fulani? Njia ambayo akili yoyote huru inaweza kuielewa na kuiweka mezani kwa uchambuzi wa wazi?
Niko tayari kusikiliza. Lakini kama hatuwezi kuelewa “Mungu” kama dhana, basi mjadala wa “kama yupo au hayupo” hauwezi kuendelea.
Kwasababu itakua si busara kwa watu wenye Maarifa kujadili kitu wasichokijua.
Ah, kumbe hujui ulimwengu ulianza vipi lakini unakuwa na confidence ya kupinga nguvu ambayo ndiyo chanzo cha huo ulimwengu.Funny how you dismiss God kwa kusema hakuna proof, lakini unaamini theory ya explosion iliyo-organize vitu perfectly bila director,,even explosion ya gas haipangi viti sebuleni!Mimi sijui ulimwengu ulianza vipi.
Wewe unadai Mungu ndiye muumbaji wa ulimwengu na huna uthibitisho wala uhakika.
Unaleta hoja uchwara zisizo na kichwa wala miguu.
Nipo kwenye hii stage kila kitu naona kama ilikuwa ndotoUnapoanza kijiuliza maswali ya aina hii, mwanzoni utaanza kujihisi mchanganyiko wa hofu, mfadhaiko, na kushtushwa pale unapoona umetumia sehemu kubwa ya maisha yako katika Imani ya Mungu.
Baadae taratibu utaanza kukaa sawa. Utaona Sheria ya kweli imejengwa katika misingi ya Humanity.
Nitamsaidia mwenye uhitaji, sitamuonea mtu, sitamlaghai mtu, etc. kwa sababu ninaongozwa na misingi ya Utu, na siyo kwa sababu naogopa nitachomwa moto na Mungu
Ukienda mbali utatunza mazingira hasa ya asili, kwa sababu Dunia ni nyumba ya wote
Wewe una uhakika na ushahidi upi kwamba Mungu ndio kaumba ulimwengu?
Au unatetea imani zako za vitabuni ulizo aminishwa na kukaririshwa?
Kuna watu wanapenda scientific evidence, wengine wanachukua faith kama “shortcut.” So, unaweza kusema, “If God is just a myth, explain how the universe came from nothing—no energy, no matter, no logic? Hiyo ni kama kusema hakuna muumba, lakini kila kitu kina muundo, sheria, na purpose. So, either una imani au una logic, lakini mixing both without evidence ni kama trying to swim on dry land.”Wewe una uhakika na ushahidi upi kwamba Mungu ndio kaumba ulimwengu?
Au unatetea imani zako za vitabuni ulizo aminishwa na kukaririshwa?
Kama hoja ni kwamba Mandela hakuchagua azaliwe Afrika Kusini au hata kuzaliwa kwenyewe, ni wazi kwamba Mungu hakuamua sio tu Mandela azaliwe lakini pia azaliwe wapi.Freewill is an illussion.
Mandela hakuchagua kuzaliwa.
Hakuchagua kuzaliwa South Africa.
Hakuchagua kuzaliwa South Africa mwaka 1918.
Mandela hakuchagua kuzaliwa mweusi Africa Kusini mwaka 1918.
Haya mambo yote yali impact maisha yake sana.
Hakuwa na freewill kuhusu yote hayo.
Freewill is an illussion.
Nadhani tunarudi kule kule kwenye tatizo la msingi 😇Kabla ya kuuliza kama Mungu yupo, tujiulize—tunaposema "Mungu", tunamaanisha nini?
Mungu (kwa muktadha wa mantiki huru) nitaeleza ifuatavyo
Chanzo kisicho na mwanzo, chenye akili au nguvu ya hali ya juu, kinachosababisha kuwepo kwa mpangilio, sheria, na uwepo wa ulimwengu huu.
Hii haimaanishi Mungu wa dini fulani. Inamaanisha:
Chanzo (source) – kitu au hali iliyosababisha kila kitu kilicho hai au kisicho hai.
Kisicho na mwanzo (uncaused) – kwa sababu kila kitu tulichonacho kina chanzo, tunahitaji kujiuliza ikiwa kuna kitu ambacho hakikuanzishwa na kingine.
Chenye akili au nguvu ya mpangilio – si lazima kiwe "kiumbe", lakini kinaonekana kupitia muundo wa akili, sheria thabiti, na utaratibu wa maumbile.
Kwa hiyo, unaweza kuweka dhana hii mezani na kujiuliza:
Je, kuna ushahidi wa "mpangilio" unaoashiria chanzo chenye akili au nia fulani?
Ikiwa ndiyo—unaweza kuchunguza dhana hii zaidi. Ikiwa hapana—basi bado hatuna msingi wa kuendelea mbele.
Dhana ya Mungu inayoweza kuchunguzwa na akili yoyote ni:
“A necessary, possibly intelligent cause of existence and natural order.”
Wewe wala huelewi unacho andika unakurupuka tu.Ah, kumbe hujui ulimwengu ulianza vipi lakini unakuwa na confidence ya kupinga nguvu ambayo ndiyo chanzo cha huo ulimwengu.Funny how you dismiss God kwa kusema hakuna proof, lakini unaamini theory ya explosion iliyo-organize vitu perfectly bila director,,even explosion ya gas haipangi viti sebuleni!
Nakuuliza hivi 👇So, kabla hujaita hoja za wengine “uchwara,” angalia hizo zako ambazo hazina kichwa, miguu, wala spine.
Una uhakika gani kwamba Mungu aliumba ulimwengu?Kuna watu wanapenda scientific evidence, wengine wanachukua faith kama “shortcut.” So, unaweza kusema, “If God is just a myth, explain how the universe came from nothing—no energy, no matter, no logic? Hiyo ni kama kusema hakuna muumba, lakini kila kitu kina muundo, sheria, na purpose. So, either una imani au una logic, lakini mixing both without evidence ni kama trying to swim on dry land.”
Yeah sure.Siku baada ya siku
Sio msomi sana lakini najitahidi kusoma kadri ninavyoweza lakini
Kadri nazidi kusoma napata ukakasi kwenye maswala ya Mungu na dini kwa ujumla
Mpaka sasa kuna muda nahisi hakuna Mungu kuna muda najipa imani yupo ila najiuliza
Mbona ukiishi kwa sheria za kibinadamu za kawaida unakuwa mtu bora kuliko mtu wa dini au anayeamini katika Mungu
Itoshe kusema HAKUNA MUNGU
Kwanza kabisa, hujathibitisha Mungu yupo.Kama hoja ni kwamba Mandela hakuchagua azaliwe Afrika Kusini au hata kuzaliwa kwenyewe, ni wazi kwamba Mungu hakuamua sio tu Mandela azaliwe lakini pia azaliwe wapi.
Kama watu wote popote, hakuna mtu ambaye hakuzaliwa na ambaye anakuja duniani pasipo utashi au uhuru wa wazazi ama ni mchakato wa kimaabara au wa asili.
Mungu hawambii watu wazae. Watu wenyewe ndio huamua wazae au wasizae, wapi na kwanini.
Unataka uthibitisho wa kisayansi kwamba Mungu ndiye aliumba dunia?Wewe wala huelewi unacho andika unakurupuka tu.
Nilikwambia mimi siamini habari za Mungu wala Big-Bang.
Nakuuliza hivi, Una uhakika, uthibitisho na ushahidi upi kwamba Mungu ndiye kaumba ulimwengu?
Hivi unaelewa kiswahili?
Nakuuliza hivi 👇
Una uhakika na uthibitisho upi kwamba Mungu ndiye kaumba ulimwengu?
Usitetee na kufosi arguments zako uchwara za vitabuni zisizo na kichwa wala miguu.