Nimeelewa vizuri kabisa, umekubali kwamba Mungu hajagunduliwa bali amejengwa tu kichwani — kwamba ni dhana ya binadamu, si uhalisia.Uelewa wa Mungu hautokani na utafiti wa kisayansi, kwani sayansi inachunguza vitu vinavyoonekana na kupimika. Mungu, kwa asili ya dhana hiyo, ni metaphysical—yani yuko juu au nje ya ulimwengu wa kimaumbile.
Chanzo cha dhana hiyo ni mchanganyiko wa:
Nadharia za kifalsafa: Wanafalsafa kama Aristotle walizungumza juu ya “The Unmoved Mover” – kilichoanzisha kila kitu bila chenyewe kuanzishwa.
Imani za kidini na tamaduni. Mila na maandiko ya dini nyingi kama Uyahudi, Ukristo, na Uislamu humuwasilisha Mungu kama chanzo cha kila kitu, mwenye akili, asiye na mwanzo wala mwisho.
Uchunguzi wa kiakili (reasoning). Baadhi ya watu hufikia wazo la Mungu through logical inference—kama vile hoja ya "First Cause" (Sababu ya kwanza) au "Design Argument" (Hoja ya mpangilio).
Mimi nimejifunza kuhusu dhana ya Mungu kutoka kwenye baadhi ya maandiko,, vitabu vya falsafa, Biblia, maandiko ya kihistoria, na mijadala ya kisayansi na kijamii.
Kwahiyo Mungu hakugunduliwa kama sayari mpya—bali ni dhana iliyojengwa, kupitishwa, na kuboreshwa na vizazi vya wanadamu kupitia tafakari, imani, na uzoefu wa ndani.
God is not seen with eyes, but sensed through reason, spirit,
and tradition.
UMEELEWA??
Nadhani hiyo logic haujaielewa vizuri, first, not all truths are scientific. Kuna ukweli wa kihisia, wa kiakili (rational), wa kiroho, na hata wa kimaadili (moral truths) ambao haupimiki kwa “data” lakini bado una uzito mkubwa katika maisha ya mwanadamu.Mkuu usiniulize mimi kwasababu mimi sijui.
Nimeelewa vizuri kabisa, umekubali kwamba Mungu hajagunduliwa bali amejengwa tu kichwani — kwamba ni dhana ya binadamu, si uhalisia.
Umesema Mungu “hakugunduliwa kama sayari mpya bali ni dhana iliyojengwa, kupitishwa, na kuboreshwa na vizazi vya wanadamu.” Kwa kusema hivyo, umejiondoa mwenyewe kwenye msingi wa ukweli wa kisayansi au kihalisia.
Kitu kilichojengwa na binadamu kupitia tafakari, mila, na maandiko ya kale— bila msingi wa uchunguzi huru, wa moja kwa moja au ushahidi usiopingika — ni dhana ya kiutamaduni, si ukweli wa kuufanya kuwa wa lazima.
Hii inamaanisha kuwa Mungu, kama unavyomweleza, si kiumbe halisi aliyejitambulisha kwa uhakika, bali ni njia ya binadamu kujibu maswali ambayo hawakuwa na majibu yake kwa wakati huo.
Hoja ya “First Cause” au “chanzo kisicho na mwanzo” ni hoja ya zamani ya kifalsafa, lakini haina ulazima wa kumhusisha Mungu ambaye unamtaja kama mwenye akili, nia na mapenzi.
Tunachojua ni kwamba ulimwengu upo — lakini hatujui kwa uhakika ulianzia wapi au kwa nini. Kukosa jibu kamili hakumaanishi tunaruhusiwa kuweka jibu la imani (Mungu) mahali pa pengo hilo bila kutoa maelezo ya kina.
Huo ni mtego wa kimantiki ujulikanao kama "God of the Gaps" — kutumia Mungu kufunika kile tusichokijua. Katika historia, kila mara binadamu waliposhindwa kuelewa jambo, walitunga kiumbe au roho ili kueleza mfano zilipopiga Radi walisema Mungu anapiga ngoma. Lakini ujinga wa wakati huo si ushahidi wa kuwepo kwa Mungu.
Umetetea hoja yako kwa kusema Mungu ni "metaphysical" — yaani haonekani, hapimiki, yuko nje ya upeo wa sayansi. Hili linaonekana kama kinga ya hoja, lakini kwa kweli ni udhaifu. Kama kitu hakiwezi kuonekana, kupimika, kuchunguzwa, wala kujidhihirisha kwa njia yoyote — basi kimantiki, hakiwezi kutofautishwa na kitu kisichokuwepo.
Tunahitaji kuweka mipaka, kama hatuwezi kuthibitisha kitu, tusidai kuwa ni ukweli. Tunaweza kukikubali kama imani, lakini si kama maarifa. Kwa hiyo, kudai Mungu yupo kwa sababu ya “hisia, mila na reasoning” si ushahidi — ni urithi wa fikra.
Sahihi, hatuwezi kuanza kuthibitisha au kukataa jambo bila kwanza kuelewa maana yake.Kufuatia maelezo hayo mazuri, sasa turudi kwenye hoja yenyewe: neno "Mungu", kwa sabubu hatuwezi kuthibitisha jambo fulani ni ukweli au ni uongo bila kujua nini maana ya jambo hilo.
Neno "Mungu" maana yake ni nini au Mungu ni nini?
Mkuu, Hoja zako zinahitaji mtu kukubali "Mungu" ni dhana halali hata kabla ya kuijadili. Lakini hilo ndilo tatizo kuu ninalolizungumzia kama ignostic.Nadhani hiyo logic haujaielewa vizuri, first, not all truths are scientific. Kuna ukweli wa kihisia, wa kiakili (rational), wa kiroho, na hata wa kimaadili (moral truths) ambao haupimiki kwa “data” lakini bado una uzito mkubwa katika maisha ya mwanadamu.
Kusema kwamba Mungu ni “concept ya binadamu” kwa sababu hatuwezi kumpima kisayansi ni sawa na kusema upendo haupo kwa sababu huwezi kuuona kwenye microscope. Absence of physical proof is not proof of absence. Kuna mambo mengi ya metaphysical tunayoyakubali ,,kama uwepo wa nafsi au dhamiri bila ya kuwa na "material proof."
Kuhusu "God of the gaps" — ni kweli kumtumia Mungu kufunika ujinga wetu ni tatizo. Lakini hilo halifuti uwezekano wa kuwepo kwa Mungu. Kutokujua chanzo cha ulimwengu hakumaanishi Mungu hayupo ,, . So, we must remain open.
Na kuhusu hoja ya kwamba “Mungu hajajidhihirisha kwa uhakika,” that’s a matter of perspective. Wengine wanadai wamemwona katika maisha yao, kupitia maombi, miujiza, au mabadiliko ya tabia. Huwezi kupima experience ya mtu kwa ruler ya maabara.
Kusema Mungu ni fikra ya binadamu pekee ni kukwepa ukweli kwamba kuna maswali makubwa yanayohitaji majibu ambayo sayansi pekee haiwezi kuyatoa. Reasoning, tradition, experience, and yes — faith — ni njia halali za kutafuta ukweli.
SIJUI NAELEWEKA MKUU?
Hayo ni maswali kwenu mnaosema kuna Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote.Kwako:
Ujuzi maana yake ni nini?
Uwezo maana yake ni nini?
Upendo maana yake ni nini?
When exactly did the universe begin to exist?Kama unahitaji hundred percent certainty kabla ya kuamini kitu, basi huenda hata hujui kama mama yako ni mama yako kweli — unless uwe umewahi kufanya DNA test mwenyewe?
Ukiuliza uhakika wa kwamba Mungu aliumba ulimwengu, ni kama mtu kuuliza uhakika kwamba mwandishi fulani aliandika kitabu wakati anaangalia hicho kitabu mikononi. Ulimwengu una order, complexity, na harmony kiasi ambacho kusema “ilimake tu yenyewe” ni kama kusema iPhone ilijiunda yenyewe baada ya volcano kulipuka karibu na Apple HQ.
Kuhusu philosophers ,hawa jamaa hawakukaa miaka mingi wakivuta bangi ya mawazo tu. Kina Aquinas, Descartes, Leibniz walipiga hesabu nzito and that's why Walisema hivi kwa kifupi
"Anything that begins to exist has a cause. The universe began to exist. Therefore, the universe has a cause — and that cause is something beyond space, time, and matter… which is basically what we mean by God."
But najua itapinga, sasa ukipinga, uje na jibu kabisa kuwa ni kitu gani hicho kilicho anzisha time yenyewe?
Hiyo line yako ya "imani inaweza kuwa ya uongo" ni kama kusema “mapenzi yanaweza kuwa ya uongo,” lakini bado unalia ukiachwa. Kwa hiyo, ikiwa uongo waweza kuwa na nguvu hivyo, vipi kuhusu ukweli? Don’t underestimate genuine faith just because fakes exist — hata pesa bandia zipo kwa sababu kuna original.
Kwa hiyo , kabla hujatupa imani kama karatasi ya toilet, jiulize: Je, hoja zako za kutokuamini zina nguvu kuliko hoja za kuamini? Au unafanya tu “intellectual gymnastics” ili uendelee kula maisha bila accountability?
Imani ya kweli haiji kwa kuona tu, inakuja kwa kufikiri, kutafakari, na kukubali kwamba huwezi kuwa chanzo cha kila kitu kwa akili yako yenye mipaka. Kama huwezi kujieleza ulianzia wapi, usijione mtaalamu wa kueleza ulimwengu ulianzaje.
Na kama bado unauliza uhakika wa Mungu kama vile unatafuta receipt ya creation, basi hujaelewa kwamba faith is not blindness — it’s trust built on reason, not ego
Chew on that.
Then why are you speaking on behalf of him?"God doesn't need anyone to speak for Him
How do you prove your understanding about God is true?, but people share their understanding of Him based on faith, experience, and scripture. Just like love or justice, not everything true needs to appear physically to be real.
Unadai kwamba kabla ya mjadala kuhusu kuwepo kwa Mungu, lazima kwanza niwe na definition isiyoegemea upande wowote ???Mkuu, Hoja zako zinahitaji mtu kukubali "Mungu" ni dhana halali hata kabla ya kuijadili. Lakini hilo ndilo tatizo kuu ninalolizungumzia kama ignostic.
Sijasema kuwa kila kitu lazima kipimwe na microscope - Wewe ndiye unaamini hivyo sio mimi na unalazimisha mimi niamini kama wewe, Sorry I can't.
Nimesema kabla ya kujadili kama "Mungu yupo au hayupo", ni lazima kwanza dhana ya "Mungu" iwe imeelezwa kwa njia isiyoegemea upande wowote—yenye consistency ya kifalsafa.
Kwani wewe hutambui kwamba kabla ya mjadala wowote let say "Ajali za barabarani" lazima uanze ufafanuzi wa hiyo dhana kisha ndipo mjadala wa chanzo cha hizo ajali uanze.
Tuseme Mungu ni “chanzo kisicho na mwanzo chenye akili” — hiyo ni tafsiri, siyo maana ya neno hilo kwa ujumla.
Tafsiri yako inategemea rational na metaphysical tradition, ambazo zinatofautiana baina ya watu na tamaduni. Hivyo basi, tafsiri hiyo haiwezi kuchukuliwa kama msingi wa mjadala huru bila kuhojiwa.
Na kuhusu kusema kuwa - Kuna ukweli wa kihisia, wa kiroho, wa kiakili na wa kimaadili hakufanyi moja kati ya hizo kuprove “Mungu” anayeongelewa ni real au ni abstract idea yenye thamani ya kisaikolojia tu.
Ukitaja miujiza, mabadiliko ya tabia, au maombi yanayojibiwa — kuna maelezo mbadala yanayothibitika, yasiyo ya kidini ambayo yanaweza kuelezea mambo hayo bila kuhitaji dhana ya Mungu.
Je, tukichunguza ushahidi huo wote bila kutumia neno "Mungu," bado utathibitisha kuwepo kwa kitu hicho kisichoelezeka vizuri?
Kusema kwamba Mungu ni wazo la binadamu ni kukwepa maswali makubwa ni sawa na kusema "Kumuweka Mungu kama jibu kwa maswali hayo ni kukwepa kazi ya kuyatafakari kwa kina.”
Kama Mungu anazungumziwa, basi aelezwe kwanza kwa lugha ya uwazi isiyotegemea imani au hisia — ndipo tuanze mjadala.
Kama huwezi kutoa maana ya "Mungu" isiyotegemea Hisia, Imani na Makisio ya watu tofauti ni afadhali ukapotea kimya kimya - mimi ninahekima nitaelewa.
Just like gravity, or thoughts ,you don't see them, but you see their effects. The existence of God isn’t about Him standing in front of you with an ID card. It’s about the evidence in creation, order in the universe, morality, and the personal experiences people have.Then why are you speaking on behalf of him?
How do you prove your understanding about God is true?
Ye yote makini atajiuliza: kwa nini au sababu gani zinazofanya mtu aseme kuna Mungu? Pia mtu anapoita neno Mungu ana maanisha nini? Na je, sababu za haya yote ni nini: ni ulimwengu umetoka wapi na unaenda wapi?Sahihi, hatuwezi kuanza kuthibitisha au kukataa jambo bila kwanza kuelewa maana yake.
Msimamo wangu ni kwamba mjadala kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu hauna maana yoyote mpaka pale tutakapokuwa na maelezo ya wazi, sahihi, na yanayoweza kueleweka kwa njia ya mantiki kuhusu neno 'Mungu'.
Bila kufafanua vizuri maana ya neno hilo, hatuwezi hata kuanza kuchambua hoja kwa misingi ya ukweli, ushahidi, au uthabiti wa kimantiki.
Kwa hiyo kabla ya chochote kingine, ningependa mtu atoe tafsiri bayana ya Mungu anayemzungumzia.
Labda je ulikua unajua maana yake kulingana na Imani yako?
The universe began around 13.8 billion years ago—right on schedule.When exactly did the universe begin to exist?
Unauliza "Mungu ni nini?” Aisee, huo ni mtego classic wa watu mnaojifanya thoughtful. Mungu siyo toothbrush mpaka umuelezee kwa manual. He is not a cosmic vending machine ya kutupa blessings tukitupa maombi. Tunamuita Mungu maana wanajua kuna nguvu isiyoelezeka, ambayo haibadiliki kila jioni kama mood ya ex wako.Ye yote makini atajiuliza: kwa nini au sababu gani zinazofanya mtu aseme kuna Mungu? Pia mtu anapoita neno Mungu ana maanisha nini? Na je, sababu za haya yote ni nini: ni ulimwengu umetoka wapi na unaenda wapi?
Mkuu, kama umeweza kujiiza maswali hayo basi wewe ni miongoni mwa binadamu wachache wasiotaka kuwekewa ukomo kwenye kufikiri.Ye yote makini atajiuliza: kwa nini au sababu gani zinazofanya mtu aseme kuna Mungu? Pia mtu anapoita neno Mungu ana maanisha nini? Na je, sababu za haya yote ni nini: ni ulimwengu umetoka wapi na unaenda wapi?
Kuhusu Mungu ni nini au neno Mungu maana yake ni nini? Nakubaliana na maana ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki, ambayo imeeleza maana ya Mungu kuwa ni neno tunaloita "Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili".Unauliza "Mungu ni nini?” Aisee, huo ni mtego classic wa watu mnaojifanya thoughtful. Mungu siyo toothbrush mpaka umuelezee kwa manual. He is not a cosmic vending machine ya kutupa blessings tukitupa maombi. Tunamuita Mungu maana wanajua kuna nguvu isiyoelezeka, ambayo haibadiliki kila jioni kama mood ya ex wako.
Na kuhusu “ulimwengu umetoka wapi na unaenda wapi,” bro, ulimwengu hauna Google Maps. Hatuna destination pinned kwenye sayari ya mwisho. Lakini kama kila kitu kina mwanzo, kuna logic kusema lazima kuna Chanzo – ni kama vile microwave haianzi tu kupika chakula bila mtu yoyote kubonyeza start. Unless unadhani tunaishi kwenye episode ya Rick and Morty permanently, logic bado inafanya kazi.
Kwa hiyo mtoa hoja, before uanze kuuliza maswali ya “existential” kama vile unaandika script ya documentary ya Netflix, pengine uliza pia: kama hakuna Mungu, kwa nini unauliza maswali kama haya kana kwamba kuna majibu makubwa yakusubiri?
Au labda unatafuta tu reason ya ku-ignore mamlaka ya juu ili uendelee kuishi kama universe iko kwenye payroll
yako.???
Aisee, hongereni kwa kusimama upande wa 'sijui',,huo ni msingi mzuri wa kutokujifunza kabisa. Kwa sababu kila ukikutana na jambo gumu, suluhu ni kujifunika blanketi la 'sina majibu' na kulala kwa raha.Mkuu, kama umeweza kujiiza maswali hayo basi wewe ni miongoni mwa binadamu wachache wasiotaka kuwekewa ukomo kwenye kufikiri.
Watu wanaopenda kuhitimisha vitu kwa lojiki na mantiki ili kupata majibu ya kuridhisha.
Afadhali kusimama upande wa kusema hujui, kuliko kusema unajua halafu unashindwa kuelezea.
Safi kabisa kwa kulitambua hilo...Kuhusu Mungu ni nini au neno Mungu maana yake ni nini? Nakubaliana na maana ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki, ambayo imeeleza maana ya Mungu kuwa ni neno tunaloita "Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili".
Unadai kwamba kabla ya mjadala kuhusu kuwepo kwa Mungu, lazima kwanza niwe na definition isiyoegemea upande wowote ???
Hilo haliwezekani (impossible burden). Hakuna dhana yoyote kubwa—iwe ni “justice,” “love,” “freedom,” au hata “consciousness”—inayoweza kueleweka bila muktadha wa kitamaduni, kihistoria au falsafa. Kwa hiyo kuhitaji definition ya “Mungu” isiyoguswa na imani, hisia au historia ya binadamu ni kutaka kuwa na mjadala usio kuwa na mantiki yoyote.
You’re asking for a metaphysical concept to be framed like a scientific variable — that’s a category error.
Na kuhusu kusema kuwa “Mungu” hawezi kuwa tafsiri ya binadamu kwa sababu zipo tafsiri tofauti — hiyo ni sawa na kusema “maana ya neno ‘uhuru’ si halali kwa kuwa kila mtu anaiona tofauti.” Lakini tafsiri nyingi hazifuti uhalali wa kujadili dhana hiyo; zinaitajika ili kufanikisha mjadala.
Hoja yako ya kusema "tusitumie neno Mungu kuchunguza ukweli" ni kama kusema “tusitumie neno ‘akili’ kuchunguza consciousness kwa sababu akili haieleweki kwa pamoja.”
Hii si hoja ya ignosticism tu,,ni denial disguised as epistemic purity. Unahitaji kila mtu atupilie mbali uzoefu, historia, falsafa na maadili ili tuanze kwenye “blank slate” ambayo haipo katika uhalisia wa binadamu.
Kama unadai tusijadili Mungu hadi upate definition "pure," basi hata hutaki mjadala, na unataka kusitisha mjadala kwa sababu hoja zako ni dhaifu sana.
Na hiyo si hekima.Hiyo ni episte
mic evasion.
Mkuu mimi sijui, Hivyo ninapokutana na mtu anayekiri anajua lazima nimuhoji ili nijue.Aisee, hongereni kwa kusimama upande wa 'sijui',,huo ni msingi mzuri wa kutokujifunza kabisa. Kwa sababu kila ukikutana na jambo gumu, suluhu ni kujifunika blanketi la 'sina majibu' na kulala kwa raha.
Unajua, akili ya kufikiri bila mipaka ni nzuri sana, mpaka inapoanza kuzunguka bila dira kama mlevi. Wanaopenda lojiki na mantiki wanaelewa kuwa hata kutokuwa na jibu ni sehemu ya mchakato wa kupata jibu,,lakini siyo kibali cha kubweteka.
Kusema hujui ni ujasiri, sawa. Lakini kama kila siku unasimama kwenye mstari wa 'sijui' bila kutafuta kuelewa, basi wewe hauna tofauti na msafiri aliyekataa ramani kwa madai ya kupenda msitu.
Mtu wa kweli hupenda ukweli, hata kama ni mgumu. Lakini kudai hamtaki mipaka ya fikra huku mnakimbia mantiki, mnakuwa hamna tofauti na dereva dereva anayetaka uhuru wa barabara bila sheria, halafu alalamike gari likipinduka.