Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Hili nalo neno
 
Duuuh ni balaa
 
Hii story ndefu na inavutia.. Ila inawiana vipi na nilichokiandika?
 
Hakuna cha kung'amua hapo. Ni story na methali za kale za Europeans. Hata wenye imani yao hawaamini huo upuuzi.
 
Waislam walisha ambiwa kwenye kitabu chao kuwa; hapa Duniani wapo kwenye chumba cha mtihani kwa hii miaka michache tu ya kuishi hapa. Kwa hiyo kila mtu ajitahidi awezavyo; kwa wale watakaofaulu ndio watakula mema ya milele...
Cheza karata yako vizuri; Kuna unaona wamefaulu hapa duniani kumbe kwenye mtihani hawajafanya vizuri.
Tenda haki/tenda mema/swali/ na mtegemee sana Mungu huku ukimuomba msamaha kila mara!!!
 
Hapa unadogosha sifa ya Mungu ya kujua yote bila kujua. Yaani Mungu hajui kila kitu ndiyo maana anakupa mtihani ili akupime.

Hivyo Mungu hajui utafia wapi, utaumwa lini, utakula nini kesho, utamuoa au utaolewa na nani, utapata hela, etc. ndiyo maana anakupa mtihani ili akupime
 
Swala la Spiritual world ni la kiimani sio la kisayansi au kimantiki, sasa swala yupo au hayupo inategemea na imani,
Uwezi kuthibitisha kisayansi kwamba Mungu yupo.
Maana Mungu Ni Roho yohana 4:24
Hivyo ambao wamekuwa maskini ktk ulimwengu wa Roho wote wanaamini Mungu hayupo ila ambao ni matajiri wa ulimwengu wa roho wanajua Mungu yupo.
Swala la kwanini mabaya yanawapata watu ni kwasabb mambo yote yanaonekana yapo chini ya utawala wa mwanadamu. Mwanzo 1:26-28.
Hivyo mabaya na mazuri yanaamuriwa na utashi wa mwanadamu.....
 
Umezaliwa na Ukimwi na Ukafa na Ukimwi katika age ya 20, haiondoi Ukweli kuwa Mungu ni Mungu.

Umezaliwa Mlemavu Bado Mungu ni Mungu.
Tunapozaliwa, hatima ya Maisha yetu ya kiroho yapo Mikononi mwa Familia, ila tunapokua Watu wakubwa hatima yetu ya kiroho ipo ndani yetu.

Watu wengi wamezaliwa na Mapungufu Kwa ajiri ya Mungu tu kujitwalia Utukufu..
Kuna Marais wengi wa Nchi wanauza kahawa mtaani.
Kuna Viongozi wengi wakubwa wamekufa kabla ya Wakati.
Kuna Matajiri wa kesho waliokufa wakiwa na Miaka 12 tu.

Huwezi kumtafakari Mungu Kwa namna ya kibinadamu na ukamuelewa, Kwa sababu Pale ambapo Akili Yako haikubaliani na chochote ndipo Mungu Huwa anaonekana.

Ukiwa mtiifu Kwa Mungu ukatembea kwenye kanuni zake utakula mema ya Nchi.

Mungu ndiye aliyekuumba, ila Biblia inasema alimchukia Essau Toka akiwa Tumboni...!
Mungu kaongea na Mussa kuhusu kwenda Misri kuwaokoa Wana wa Israel, wakakubaliana vizuri, Mussa akiwa njiani kwenda Misri, yeye Mke na Mtoto ghafla Mungu anatokea na anataka kumuua Tena Mussa, bila Mussa kujua, bahati yake Mkewe alikua mtoto wa Mchungaji na alielewa ghafla Kuna uwepo wa Mungu, na akaelewa kile Mungu anataka kufanya, na akachukua hatua na Mungu akahairisha kumuua Mussa.

Kama hufanyi kitu Kwa ajiri ya Mungu na yeye hafanyi kitu Kwa ajiri Yako.....!
 
Hiki ndicho huwa nakiamini pia. Hakuna tofauti na wanyama wengine. Wao pia wana mapitio yao, magumu yao na mwisho wao bado ni kufa tu
100%

Na wao wakifa hakuna lingine zaidi ya kuwa chakula cha wadudu huko chini, hakuna cha kwenda mbinguni wala jehanamu 😎
 

Mungu ametupa utashi wa kutenda ili aweze kutuhukumu...
Usije kuona chui ukamfuata eti kwa sababu Mungu atakulinda; Amesha kupa utashi na maarifa
Na alifanya hivyo kwa maksudi ili kiwe kigezo cha waliofaulu kupata raha za milele
Mungu anakusanya malipo ya kila mtu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…