Kama Rais hataki kufanya kazi na Kassim Majaliwa amuombe ajiuzuru kama Philip Mpango

Haina haja ya kumuomba ni kumsingizia tu kaandika barua ya kujiuzulu mchezo kwisha
Rais hahitaji kumuomba wala kumsingizia barua ya kujiuzulu Waziri Mkuu.

Rais anaweza kuvunja Baraza la Mawaziri akateua Waziri Mkuu mpya tu. Kikatiba.

Nyerere alishafanya hivyo. Mwinyi alishafanya hivyo.

Rais Samia anagojea tu baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba akishinda atapanga Baraza la Mawaziri jipya, na sitashangaa ikiwa Majaliwa hatakuwemo katika baraza hilo.

Sasa mnataka amuondoe Majaliwa kwenye uwaziri mkuu miezi 9 kabla ya uchaguzi na kuanza kujieleza kwa nini kafanya hivyo, wakati anaweza kumuondoa baada ya uchaguzi na kusema Majaliwa kashakuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 sasa Samia anajenga timu mpya baada ya uchaguzi?

Kwa wanaotaka Majaliwa aendelee kuwa Waziri Mkuu au angeteuliwa kuwa mgombea mwenza, kwani Majaliwa ana hatimiliki ya hivyo vyeo?

Si mnajua kuwa rais ana haki ya kupanga timu yake?

Kuhusu manung'uniko ya Watanganyika, si mnaikubali hii katiba inayoorodhesha mambo ya Muungano? Kila siku mkiambiwa mabadiliko ya katiba mnafikiri ni mchezo?

tpaul
 
Mkuu nadhani ni hizo Kanuni mlizotunga wenyewe!
Mkuu kuna hiki kigezo ndiyo nadhani kimefanya Kassim asifikiriwe!
Dini-Rais akiwa Mkristo,VP anapaswa awe Muislam! Rais akiwa Mkristo,VP anapaswa awe Muislam.
Sambamba na hilo kuna hili la uwiano wa pande za Muungano.
President akitoka Zanzibar,VP anapaswa atoke Tanganyika.
Rais akitoka Tanganyika,VP anapaswa atoke Visiwani.
Mama hastahili Lawama zo zote tena za kutoka kwa Mwana CCM tena kindakinda.
1.Mkapa-Dk.Omar/Shein
2.JMK-G.Bilal
3.JPM-SSH
4.SSH-Dr.Mpango
Na sasa SSH anaenda na Dr.Nchimbi
Na kwa kuwa huko kuna fomu moja bila kujali sifa komaa tu Mkuu.
 
To be
Honestly angempa majaliwa nafasi ya mgombea mwenza uhakika wa majaliwa kushinda ni mkubwa,wta mm ningejiandikisha kwa sababu ya majaliwa
 
Hakuna vigezo vyovyote, ni connection tu.

Baba yake alitumia vigezo gani zaidi ya kuhifadhi juzuu mbili tatu kichwani na elim dunia kidogo ya kuzugia, kisha kapewa uraisi bila kuwa na ndugu hata mmoja huko Zanzibar.
Inaonesha hakuna unachokijua kuhusu uraia wa Zanzibar, ndo maana kuna kitambulisho cha uraia wa Tanzania na kitambulisho cha mzanzibar mkazi. Sàsa wewe njoo na chogo lako uone kama utapewa kitambulisho cha mzanzibar mkazi.
 
Mkuu nakubali kuwa katiba ya chama chetu imesiginwa na pia katiba ya nchi imesiginwa. Katika uteuzi wa Kassim Majaliwa kama mgombea mwenza, bila kufuata utaratibu huko pia simo. Mimi nilipenda Majaliwa ateuliwe kuwa mgombea mwenza kwa kufuata utaratibu.

Kitendo cha rais kumteua mamluki kuwa mgombea mwenza kimekumiza sana chama chetu. Rais anajua kabia kuwa Nchimbi ni team Lowassa, na yeye (Nchimbi) na Sofia Simba waliasi maamuzi ya chama waziwazi kwa kumuunga mkono Lowassa, ambaye hatimaye alitimkia UKAWA.

Simba ameishafukuzwa uanachama lakini Nchimbi ameachwa hadi amekuja kuteuliwa kuwa mgombea mwenza na hatimaye VP. Kama Nchimbi naye angefukuzwa uanachama kama Simba alivyofukuzwa, leo hii asingepata nafasi ya kuteuliwa.
 
Hizo hisia zako ni chochoko na fitna tupu.
Kuchagua mgombea mwenza hakuna uhusiano wowote na waziri mkuu.Nionavyo Kassim Majaliwa anaweza kuweka rekodi ya kuwa waziri mkuu kwa kipindi kirefu kuliko waziri yoyote aliyetangulia kwenye cheo hicho.
 
Mtenda jamala hulipwa jamala, Samia naye atatendewa kama Job Ndugai na Mpango (kulazimishwa kujiuzulu).
Mimi nadhani adhabu yake itakuwa kubwa zaidi ya hizi adhabu alizowapa Mpango na Majaliwa. Magufuli alionywa hakusikia, likamkuta la kumkuta. Ngoja naye aendelee kuwatesa watu, Mungu anamuona.
 
Reactions: G4N
Huyo inasubiriwa natural death. Yaani mama siku anavunja bunge ili tuende kwenye uchaguzi na yeye itakua ndio byebye.
 
Namuomba mungu ccm ipasuke vipande viwili. Wanamapinduzi wa kweli tuanzishe chama kingine tuweze kugombea uchaguzi mkuu. Kama hilo haliwezekani tuhamie chama kimoja kidogo. Ukweli tumezidiwa ujanja na hila.
 
Mmeanza kulumbana wenyewe kwa wenyewe naona sasa akili zimeanza kurudi ule ujinga wenu unapotea taratibu.
Mkuu nawe ni shahidi nadhani ulishuhudia kilichotokea kule Dodoma. Wewe unaona ni sawa? Wanachama wengi tumekasirishwa sana ila tunaogopa tu kusema hadharani.
 
Mkuu wewe ndiye unahubiri ubaguzi, ni vema ungemshauri atafute suluhisho la wabara kutopewa nafasi visiwani
Kumbe hata wewe unakubali kuwa mtanganyika hawezi kuteuliwa kuwa RAS katika mkoa wa nchi ya Zanzibar? Huo ubaguzi bado huuoni mkuu? Unataka wapemba waendelee kuchukua nafasi za watanganyika hadi lini? Mama Samia anakiuka sana utaratibu.

Nakwambia huyu mama ni mbaya hata kuliko Magufuli. Watu hamjui tu. Je, yule mpemba wa baraza la mitihani (NECTA) alifikaje hapa Tanganyika? Kule kwao kuna baraza la mitihani (ZEC) pia. Kwanini hawakumpa nafasi kule wamekuja kumtupa hapa Tanganyika? Ili iweje?
 
Seen
 
Ukweli kabisa watanganyika ni wapumbavu sana. Zanzibar hakuna upumbavu kama huo. Eti mtu atoke chamwino akawe mkuu wa wilaya pemba!
Sasa toa solution siyo kulalamika tuu
ulishaambiwa zanzibar ina serikali yake, sasa mtanganyika unataka ukafanye nini huko kwenye nchi ya watu?
 
Kumbe raisi Hana makosa. Wewe ndiye mwenye makosa, kwanini uwe kada wa ccm kindakindaki wakati unajua ubaya wake.
 
Haina haja ya kumuomba ni kumsingizia tu kaandika barua ya kujiuzulu mchezo kwisha
hivi akikanusha na kusema ukweli kuwa hakuandika barua kama wanavyofanya kina lissu kusema ukweli daima na uhalisia itakuaje, watamshughulikia?
 
kuna kero za muungani ambazo kwa sasa zimetatuliwa sana moja walo ni uteuzi wa wazanzibari kwenye vyeo vya muungano
Wewe kiazi kweli. Bila shaka utakuwa mdebwedo wewe, hivyo unatetea ubwete wa vyeo mnavyopewa hapa Tanganyika. Kama uteuzi unaondoa kero za muungano mbona watanganyika hawateuliwi kushika nafasi katika nchi ya Zanzibar kama nyie mnavyogawiwa vyeo kwenye nchi yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…