Kama Rais Samia ameshindwa kazi basi ajiuzulu maana hali inazidi kuwa mbaya

Wanadai vifurushi ni ofa za biashara wakitaka wataviondoa
Hawana uwezo wa kuviondoa maana biashara yao itakufa. Ni muda muafaka sasa bunge lilete mwongozo wa kikanuni juu ya mabando maana ndio biashara ya mtandao wa simu hapa Tanzania.
 
Mkulima aliyefaidika na jasho lake mwaka huu ni wa kupaswa kushukuru ukame uliosababisha hali ya mavuno kuwa chini sana. Hivyo aliyebahatika kuvuna kidogo kakutana na soko zuri. Uzalishaji ukiwa mdogo bei inakuwa kubwa, we huoni mafuta yalivyopaa bei kisa mzalishaji mkuu hakuweza kuweka bidhaa zake sokoni?
 
Amepewa Muda acha waliompa muda wapime KAZI yake wakiridhika nayo aendelee kuupiga Mwingi!!
 
Hakuna awamu iliyofanya mabaya ya kutisha kama awamu ya tano.
Hapana kwa kweli vitu vilikua bei nafuu tambi tulinunua 1200 sasa 2000, mche wa sabuni tulinunua 2000,sasa 3500 mpaka 4000 jamaa, mchele tulinunua 1200 sasa 3500,mafuta ya petrol ilikua 2100 litre sasa habari tunayo
Kiukweli hatuna jinsi ila utawala ule ulikua nafuu mara 1000 kwanza sisi wenye biashara zinahusu umeme oooh umeme kukatika mnaweza kaa mwezi umeme haujakatika na ukikatika mapema tu huu hapa maji yalitiririka muda wote utawala ule nimeumiss kwangu maisha yalikua nafuu labda kwenu wanasiasa ndo yalikua magumu.
 
Mazuri yake ni mengi kwangu kuliko mabaya
 
Nafikili itakua nzuri kuomba uraia MOJA ya nchi za ughaibuni, hapendi kabisa tulia bongo , ila maisha ndivyo yalivyo , Kuna vitu

Mfanono, kusafili safili, kuchangia kila arus, kushona nguo mpya kila kwenye tukio n.k inakua ni hulka ya mtu, Sasa mtu akibatika akawanazo pesa, kapata nafasi flani hivi , kisu kinakua kimepita kwenye mfupa
 
Maisha ya watanzania yamekuwa magumu kuliko hata enzi za utumwa
 
Sijaelewa unaongelea nini hapa.
 
Anapokua nje anakua huru kimkakati,kama ana ndoto ya urais ya 2025/2030!

Akiendelea kubaki HUMU wanga wengi Sana wanamsagia kunguni!

Sukuma gang,msoga gang na wengineo ambao hawakufurahishwa yeye kushika hatamu!!

Acha aende akafanye yake huko ughaibuni!!
 
Nimekuelewa mkuu, bati anajisumbua bure na Urais , Kama anasoma nyakati, alitakiwa Sasa FANYA Mambo muhim ili kuacha kumbukumbu nzuri pale atakapo hayupo Madarakani,

Mfano ukiangalia miradi mingi anamalizia au kuendeleza ya mwenda zake,

Kuna Jambo linaweza mpa legacy kubwa mbele anapoenda kutokua Madarakani nalo ni katiba mpya basi, hii inatosha Sana, ila hii ya kufukuzana na Urais anapoteza mda tu
 
Unaaminije anapoteza Muda!?

Ki ccm ccm na kibongo bongo huyu mama Anaweza peta akawa tena !

Sema kama wale jamaa 0101 ndio pekee wanaweza mwambia Bas kaa pembeni awamu yenu na hayati imeisha Acha next stage ifanikishwe na Mwingine co z tunamwelekeo mpya wa Mabadiliko!!

Ni Hao jamaa pekee tu!!

Mi Nadhani waliomharibu kichwa na mama kuingia kwenye vita kwa kutangaza mapema nia ni wahuni FULANI HIVI wanaotaka achoke mapema kisiasa
kwa kuhujumiwa Ili akose mvuto kabisa kadri muda unavoenda na kweli wamefanikiwa Sana!

Hadi Sasa anajitutumua lakini haonekani kama anafanya kitu cha maana!shaka anajitahidi lakini sioni anaemwelewa KABISA!!

Hasa pale alipowaondoa mawaziri wa mwendazake!WATU walitaka moto ule uendelee kuwaka ule wa tumbua mafisadi,leo wamepeleka MAHAKAMANI mafisadi walitaka hayo!sasa hawaoni!

Wanasikia tu mara kodi hailipwi mara CAG karipoti UPIGAJI ule mara Huu!Halafu HAMNA kinachofanyika !!

Kazi ipo ngoja Tuone!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…