Kama sio Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Watanzania tulikuwa tunapigwa na kitu kizito sana na DP World

Wewe endelea tu kulisha hao wenzako hayo Matango pori
 
Ni RUSHWA KUBWA. ZA WAAFRIKA WEUSI TU.
 
Aidha ni mjinga au hujauelewa mkataba wa DPW.
Hakuna mtu aliyekataa uwekezaji bandarini.
Wewe ni kati ya watu wanaopenda utumwa. Au ni Mpumbavu.
 
Last week nilikuwa kijijini. Nilishangaa walivyokuwa wanapeana waraka kutoa copy hasa kwa walutheri.
 
Sio wewe tu uliyepoteza Imani,ni wengi tu!Mwananchi wa kawaida anayejua kusoma kiingereza akisoma kichwa cha habari Cha ule mkataba tu,unaona kuwa ni bandari zote ,za bahari,maziwa na nchi kavu zinakodishwa.Halafu mtu mmoja,ama kwa ulevi wa fedha,ama madaraka anasema ni gati chache tu za bandari ya Dar es salaam ndizo zinakodishwa!


Ili uweze kukubali kusaini mkataba wa namna Ile ni lazima uwe umepofushwa na ama rushwa ya fedha ndefu,au ahadi nyingine nzito.Kila nikitafakari sababu ya CCM kukubali na kuukumbatia mkataba ule naona kuwa inawezekana wamepewa fedha nyingi kwa ajili ya uchaguzi ujao,maana kwa ccm kitu pekee chenye maana ni uchaguzi.
 
Aidha ni mjinga au hujauelewa mkataba wa DPW.
Hakuna mtu aliyekataa uwekezaji bandarini.
Wewe ni kati ya watu wanaopenda utumwa. Au ni Mpumbavu.
Wapo wengi sana waliomkataa DPW kwa kigezo cha uarabu wake wakasahau ukubwa na uzoefu alionao dunia nzima.

Mkataba wa DP World nimeelezewa kuanzia kifungu cha kwanza mpaka cha mwisho na mtu aliyeshiriki kuuandika huko Dubai.

Sio suala la kupenda utumwa ni suala la kutaka ufanisi pale TPA usaidie ukuaji wa uchumi kwa maana halisi na sio kila siku kuwafaidisha wapigaji wachache wanaodanganya umma kwa kutoa mamilioni huko makanisan na misikitin na wao wakipata mara kumi zaidi kule bandarini kwa njia ambazo zikizibwa pato litaongezeka zaidi kule hazina.
 
Aliyesaini ule mkataba ni mtaalam wa sheria za kimataifa na amesaini mingi sana iliyozinunua ndege zote za ATCL.

Tatizo letu kila mtu anajua kila kitu na tunabaki kuwa na taifa la wajinga wa miaka yote.
 
Waraka usomwe hadi Oktoba 2025

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…