Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

ndio maana mpaka sasa Tanzania, shule za serikali za advance zinaongoza kwa ufaulu!, kule hakuna changa la macho ni "if u know you know, if u dont know na english yako basi huna maajabu'.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mnahubiri umasikini.
Mimi mwanangu hata mars nitampeleka kusoma.

Kuhusu maisha ni wewe mwenyewe mzazi ndio unaamua mwanao awe nani na umkuze vipi na sio shule ya serikali au shule binafsi yenye ada kubwa.
Kama mzazi unaamini shule fulani ndio zina determine mwanao aje kuwa nani basi uko sahihi kuamini kitu kama hicho hivyo tatizo ni wewe.

Bila kusahau English ni lazima haijarishi upo wapi ilimradi wewe unaishi hapa duniani.
Considering hakuna tatizo kuja lugha zaidi ya moja.
Ninachoona ni wengi English imepita pembeni hivyo wajaribu kutafuta justifications no hard feelings lakini ndio ukweli hivyo siku zote unauma.

Pia ubora wa elimu ni tofauti kati ya private schools na za serikali.
Kuna vitu vingi shule za serikali havina ukilinganisha na shule binafsi.
Labda kama unataka huyo mtoto awe anakariri then aje kuomba ajira au hujui umuhimu wa elimu.
na baada ya hapo hakuna hata kimoja ataweza kitumia sababu ya kukariri.
Hata awe na MBA.


Na asilimia kubwa ya graduates wasio na mbele wala nyuma ni wale wa serikali sababu wazazi wao ni masikini hata humu wamo pia na wale waliopita shule za serikali.
Na ndio sababu kubwa ya kushindwa kuona umuhimu wa elimu ya kueleweka.

yanayotokea huku shule za serikali ni pathetic trust me najua ninachokiandika na situmii emotions.
Kama pesa ipo angalau kidogo peleka mtoto shule ya kueleweka hata kama unauza kachori.

Mengine ni kujifariji na kuwa optimistic juu ya false reality sababu ya emotions hivyo kugeuka fallacy kwani ni personal perspectives and opinions.

Still mfumo wa elimu ni mbovu ila viwango vinatofautiana kutokana na shule.
 
ndio maana mpaka sasa Tanzania, shule za serikali za advance zinaongoza kwa ufaulu!, kule hakuna changa la macho ni "if u know you know, if u dont know na english yako basi huna maajabu'.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hii haiwezekani mkuu.

Huwezi kuelewa physics na masomo yote ya science kama huelewi lugha iliyotumika labda kama unakariri tu then upate A.


English itabaki kuwa muhimu tu.
 
Kumbe ni mwendo wa kukariri tu.
English ni muhimu tu hakuna excuses za kueleweka.

Wengi wanaumia ndani kwa ndani angalia tu utaona wanavyocomment.
 
Ongeza round ya kwnza imeisha... Mtoto wa miaka sita anaweza kupanga hoja kwa ujasiri hadi naogopa kitu ambacho me wa kayumba hata nikiwa high school nlikuwa siwez halafu leo eti nimpeleke kata... Kweli ntakopa kikoba mwanangu asome inglish midiyam

Nakuunga mkono 'akanana'.

Endelea kugida tu.
Weita nitamaliza shoo mimi bili ya huyu muungwana-anaejitambua.
Hao wengine enderea kuwaruka😉
 
Kumbe ni mwendo wa kukariri tu.
English ni muhimu tu hakuna excuses za kueleweka.

Wengi wanaumia ndani kwa ndani ndio angalia tu utaona wanavyocomment.
english haina umuhimu wowote kwenye sayansi labda kwenye history huko, lakini sayansi ni Ujiniazi wako tu mkuu. Wewe endelea kubishana na sisi tu.
 
english haina umuhimu wowote kwenye sayansi labda kwenye history huko, lakini sayansi ni Ujiniazi wako tu mkuu. Wewe endelea kubishana na sisi tu.
Mimi najua nachokiandika sababu nakishuhudia mwenyewe na wala sibishani.

Physics na masomo ya science yote ni tatizo kwenye shule za kata sababu ya lugha hawaelewi hivyo wanakariri tu au wanaita kumeza.
Hivyo wanakesha kutwa kucha usiku na mchana wakikariri kanuni nk then wanasahau baada ya muda mchache tu.

Ila kama unaelewa lugha unasoma mara moja tu na kuelewa wala hakuna kigumu na hakuna kusahau sababu umeelewa.

Na huwezi ukasema English haina umuhimu wakati hayo masomo ya science yote yanatumia English.

English ni essential kivyovyote vile na haikwepeki kama kweli unaju umuhimu na maana ya elimu.
 
Acha uongo mkuu, nimesoma shule za kataa mkuu, nimesoma na hao english medium advance na university, kwa kifupi hawajai kunimakata kwenye anga zangu katika masomo. Narudia tena hawajawahi, huwa nawakalisha chini na kuwapiga kitabu.
 
Acha uongo mkuu, nimesoma shule za kataa mkuu, nimesoma na hao english medium advance na university, kwa kifupi hawajai kunimakata kwenye anga zangu katika masomo. Narudia tena hawajawahi, huwa nawakalisha chini na kuwapiga kitabu.
1)Ungekuwa English mediam ungeweza kuwa smart zaidi.
Tunapolinganisha vitu/watu wawili tuweke constant mambo mengine.
2)Hugo jamaa wa sayansi hajui kuwa English inayohitajika kwenye Sayansi ndi kidogo tu. Mtu akifaulu akiingia A level Hugo anayo English ya kuelewa sayansi. Asipoelewa shida ni ubongo . Concepts hazihitaji kiingereza kingi kama cha Kelvin Jackson Twisa mzee wa Vitasa Night.
 
Sidhani
 
H hahahahaaaaaa hesabu hata iwe kwa lugha ya kiswahili kama akili hazichaji huwezi kufauru.
 
ung'ele upande wa sayansi ,sio kigezo Sana.sayansi inahitaji IQ kubwa,uwezo wa kumeza na ku memorize vitu,kinyume na hapo hutoboi kilahisi hata Kama umezaliwa UK.
 
Kama unafikir elimu ni garama jaribu ujinga.
Mi mtu anaemsomesha mwanae kwa hela nyingi kwangu huyo ndio mpambanaji. Unachotakiwa umuandae mwanao kuajiriwa popote dunian sio lazima iwe hapa. Unatakiwa ujiulize kwanini wewe uliyezaliwa nyumba ya kawaida baadae unajenga gorofa kuna nini kipya hapo? Kwanini ucjenge nyumba ya milion 40 tu safi mpaka unatumia milion mia 3 mpaka 6 kujenga makaz yako. Mi nashaur kama unaweza wekeza kwenye elim elim elim na elim isiwe hii ya bure mzee. Mtu asikudanganye elimu ni huku mwanzo kule juu unamalizia ulichokianzisha. Mi nakumbuka niliwasomesha wadogo zangu nikiwa na banda. Matokeo nimeyaona na hata nikiona mtu anamaisha mabaya ciz anasomesha mi cmlaumu. Mjengee mwanao kujiamin. Ukiangalia utawala wa nchi yetu wa sasa ni matokeo ya kutokujiamin zile shule za kajamba nani walizopitia. Muda wote anahic wazugu au wenye hela wanataka kutuangamiz. Fear of unknown. Elim elim elim.
 
hichi kilimo cha matikiti online
 
Tatizo muda wa kumsimamia mwanao
 
Kayumba ya sasa hari ni mbaya sana...sio tuliyosoma sisi..pili wale walimu na matution tuliyoyasoma hayapo tena walimu wa sasa wito huo pia hawana kabisa.

Wito uko huko private school kwakuwa wanalipwa maslahi mazuri,yaani madogo kayumba wanatoka weupe pyeeeee.

Mie nafikiri tuwape elimu bora kwa kadri inavyoeezekena hata ikibidi kwa mabeberu...ila tupambane sana kutafuta maisha na hela pia tuwekeze mnooo mfano wanangu wanataka kuwa madaktari...napambana ili nifungue duka la dawa ili kije kuwa kijiwe chao kipindi cha likizo...

Mwingine anataka kuwa rubani..skimaliza form4 tu namtia kwenye zile course zao..

Sasa lugha ya malikia ni muhimu sana na pia confidence so najaribu kuwapa mwanga na maarifa..Kayumba huu mwanga haupo...

Alafu hatausaki tu shule kuna za private nyingi sana bei nafuu alafu za seminary..mie nalipa 1.6M kwa mwaka..boarding...alafu huwezi natupiaga 5K kila mwezi madogo wako w2..so hatuna stress za wadada wa kazi,sie tukiamka ni kusaka mshiko tu..na kuwekeza kwa ajiri ya madogo...

Kuna mwana anasema dunia kuna dini 2 tu umasikini nau tajari sasa kazi kwetu kuchagua dini gani na kuitumikia.?
 
Hilo halina mjadala mkuu, ila personally siwezi ku toil kwenda kuspend mahela Tusiime wakati kuna shule za serikali nzuri tu ambazo ukimpeleka mtoto ana excel bila shida. Kikubwa ni mtoto awe kichwa tu! Kokote atatoboa.
humu unajua % kubwa wote mlipasua kwa msuri sana...mlikuwa kichwa zipo shule nzuti na affordable embu siku tembelea kayumba check darasani...msikilize mwalimu...anavyofundisha pia ns mszingira ya shule na vyoo nk...
 
Wanajifariji tu hawa!
 
Kwahiyo huko Kayumba schools ndio wanafundishwa reasoning?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…