Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Unatumia nguvu nyingi sana ktk kumsomesha mtoto, mwisho mtoto anamaliza Shule hana kazi na wewe mzazi huna kitu. Hata akipata kazi fedha anaanza kukurudishia kwa kukulea.

Ila ukianza kuwekeza, hata kama atapata Elimu ya kawaida. Mzazi akipata hela mtoto lazima atapata hela.
acheni kukuta tamaa mapema...have big focus kama tulipuyanga sie na elimu yetu basi unaona dhambi kuwapa elimu bora...tupambane tu mkuu hamna namna...hawa wanatakiwa wawe juu tumia connections zako zote za wana ili madogo watusue...
 
Habari wadau..

January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.

Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.

Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.

Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi ambazo wanasoma msingi zilikuwepo tayari ila wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..

Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za bei nafuu kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
Kwenye paragraph yako ya mwisho, elimu nayo ni asset. Pia curriculum na syllabuses ni zile zile.
 
True.. mtu analipa milioni 3 ama nne kwa mwaka ili mwanae ajue kiingereza tu. Huku sylabus anayofundishwa mwanae wa tusiime ni ile ile ambayo wa elimu bure anafundishwa. Tofauti ni lugha tu.

Tatizo la elimu yetu ni sylabus. Jaribu kuwaza hiyo milion 3 kila mwaka mnunulie kiwanja ndani ya miaka 7 atakuwa na asset kiasi gani huyo mtoto.

Mtoto atakuwa na uhakika wa kupata elimu ya juu ama basic need hata kama mzazi umefariki.
Ushaona asset ni kiwanja pekee?
 
Sehemu tulipowezwa ni hapa..

Mtoto wako, anakuja kuishi Tanzania hiii hiii unahangaika awe mzungu..hahaha.. na anafundishwa matatizo ya kizungu, kwa lugha ya kizungu..akitoka huko ameshakuwa mzungu anakuja kwa watanzania mtaani anaanza moja.. 🙂

Na cha kufurahisha ni sisi wazazi ndio tunakuwa tumewanunulia watoto wetu hiyo delay huku mtaani. Elimu tuliyomnunulia ndio imekuwa kikwazo..

Bora kila mwaka ungekuwa unamnunulia mtoto ng'ombe nne.. anasoma shule ya laki tano kwa Temu.. akija kumaliza shule anakuwa na ng'ombe 68, ukiweka kuzaa na kufa hakosi ng'ombe 100 kwenye kipindi cha miaka 16 ya kusomea elimu.

Na elimu yenyewe ndio imekuwa uchuro uchoro mtupu
Akili yako imeishia kwenye ng'ombe tu?
 
Kuna wazazi wanapata stress ikifika kipindi cha kulipa ada mpaka wanatia huruma.
Kuna mtoto amekaa wiki tatu hajaenda shule tatizo ada.
Mwingine alikuwa analalamika hela imekuwa ngumu plus anadaiwa term ya nyuma hivo mtoto hatapokelewa atleast angekuwa anadaiwa mwaka huu mpya wa masomo wangemvumilia kidogo.
Mimi kwakweli nikija jaaliwa kama nikiona maisha yangu tia maji tia maji wala sitaki stress aende tu kayumba nitajitahidi asikose tution na kumsimamia.
Muda mwingine unakuta mtu anateseka na kumhamisha hawezi anawaza walimwengu watamuonaje.
Pata picha una watoto watatu halafu hela yenyew yamawazo lazima akili ikukae sawa.
tutafute hela wakuu
 
Hawana exposure..na kujiamini.
Kujua lugha hakukufanyi smart... Au kujua kabla ya mwingine hakukufanyi uwe na akili zaidi yake.. mtoto anatakiwa ajue hilo mapema maishani.

Elimu ni kutafsiri maarifa uliyopewa au kupata katika maisha yako ya kila siku. Mtoto anajua kiingereza hajui kufunga kamba za viatu inamsaidia nini!?
Mtoto anajua kiingereza hawezi kwenda sokoni mwenyewe na kurudi itamfaanini!?

Logic and Reasoning ndio muhimu. Kwa level za chini watoto wanatakiwa kuwa curious... Mid ages waweze kuleta connection na theory na uhalisia katika maisha yao.. mtoto awe huru atleast saa 9 saa kumi aende akacheza apumzike kutoka shule ... Ukizidisha hapo unaua curiousity mtoto anakuwa duster ananyonya kila kitu kama kilivyo without Reasoning
Nani alikwambia anapata lugha peke yake?
Kuna mengi mtoto wa international schools wanapata tofauti na lugha.
 
Tatizo watu wengi wanaagalia ufaulubwa darasanj tu wa ma hpa ya chuo nk.

But mtoto aliesoma international schools Na aliesoma Kayumba wanatofauti kubwa sana.

Tofauti kuu ni exposure aisee without exposure katika hii dunia utasota sana tena sana

Pia circle ya marafiki anao kuwa nao maconnection kibao.
 
Akili yako imeishia kwenye ng'ombe tu?

Man mie nashukuru Mungu nimejigundua kuwa wenye uelewa mpana humu JF wa mambo mengi ni wachache na mie nikiwa mmoja wapo ... I THANK GOD nimeweza kuanza kutumia internet at very young age nikiwa 14 in 2004 nilikuwa wote nyumbani mzee katuwekea internet na laptop ya kila mtoto paka pale tulipomaliza form six na kwenda chuo hapo ndio tukaacha huo ujinga wa home ... ila during the time nakumbuka nilikuwa mdogo ila nilikuwa napenda sana kupitia two famous TANZANIA WEBSITE . Moja ilikuwa WWW.MARAFIKI.COM and www.JAMBOFORUM.com kama sijakosea ambayo ndio hii sasa JAMIIFORUM nahisi . So mie ni kijana now wa miaka 30 dot . Lakini nimegundua VIJANA WENGI wa SASA NI ZERO SANA . Nilikuwa mdogo paka sasa ni BIG FAN WA JF . I use to come here at young age kujua whats goin on in my COUNTRY n i was proud kukuta NONDO ZA WATU WAZIMA . I learned a lot paka NIKAJA KUMPENDA mwanamama alijiita FAIZA au watu wengi walikuwa wanamtania bibi paka na mimi nikaamua kuweka SIGNATURE ya “ MJUKUU WA FAIZA “ , to be HONEST am VERY ASHAMED NA JAMII FORUM ya SASA , kila dakika tano huwa lazima nichek whats going on in my country TZ cause mimi niko UGHAIBUNI , ninayokutana nayo na NINAYOYASOMA Kwenye COMMENTS ni ujinga sana . JAMII FORUM YA SASA SI YA ZAMANI , ni NGONO NGONO NGONO , UBISHI UBISHI WA KIJINGA , alafu tunabaki kusema ELIMU BURE INASAIDIA , kweli ??? NAANDIKA KWA UCHUNGU , hapa tu JF ni SEHEMU TOSHA YA KUJUA ELIMU YA TANZANIA INAPELEKA WAPI TAIFA ... sorry kuandika kwa urefu ila NINAUMIA SANA KAMA MTANZANIA .... VIJANA TUJIONGEZE . Tutabaki kuwa END USERS [emoji23][emoji23][emoji23] wazee wataendelea KUTUTAWALA PAKA TUFWEEEEEEZZZZZZ [emoji23]
 
Naona mnahubiri umasikini.
Mimi mwanangu hata mars nitampeleka kusoma.

Kuhusu maisha ni wewe mwenyewe mzazi ndio unaamua mwanao awe nani na umkuze vipi na sio shule ya serikali au shule binafsi yenye ada kubwa.
Kama mzazi unaamini shule fulani ndio zina determine mwanao aje kuwa nani basi uko sahihi kuamini kitu kama hicho hivyo tatizo ni wewe.

Bila kusahau English ni lazima haijarishi upo wapi ilimradi wewe unaishi hapa duniani.
Considering hakuna tatizo kuja lugha zaidi ya moja.
Ninachoona ni wengi English imepita pembeni hivyo wajaribu kutafuta justifications no hard feelings lakini ndio ukweli hivyo siku zote unauma.

Pia ubora wa elimu ni tofauti kati ya private schools na za serikali.
Kuna vitu vingi shule za serikali havina ukilinganisha na shule binafsi.
Labda kama unataka huyo mtoto awe anakariri then aje kuomba ajira au hujui umuhimu wa elimu.
na baada ya hapo hakuna hata kimoja ataweza kitumia sababu ya kukariri.
Hata awe na MBA.


Na asilimia kubwa ya graduates wasio na mbele wala nyuma ni wale wa serikali sababu wazazi wao ni masikini hata humu wamo pia na wale waliopita shule za serikali.
Na ndio sababu kubwa ya kushindwa kuona umuhimu wa elimu ya kueleweka.

yanayotokea huku shule za serikali ni pathetic trust me najua ninachokiandika na situmii emotions.
Kama pesa ipo angalau kidogo peleka mtoto shule ya kueleweka hata kama unauza kachori.

Mengine ni kujifariji na kuwa optimistic juu ya false reality sababu ya emotions hivyo kugeuka fallacy kwani ni personal perspectives and opinions.

Still mfumo wa elimu ni mbovu ila viwango vinatofautiana kutokana na shule.
Serikali yenyewe imeshituka na kuamua kufungua kila mkoa shule moja ya english medium
 
Hivi huu msemo Wa eti watoto wanaosoma shule za academies sijui private school eti wanaishia kujua lugha tu, mi natofautiana na wewe mkuu, Kijana wangu yuko std seven hizo shule, sikifichi anawa challenge hata majamaa waliosoma hizo ma A level za kata na wanamkubali mbaya.
Anawachallenge A level katika ishu zipi
Critical thinking
Creativity
Au current issues.
Kama ni reciting za principle za science basi ni kutokana na kuwa na weledi katika kuzungumza kingereza. Kwani hilo ndio tatizo la wanafunzi wa shule za kawaida.
 
Sehemu tulipowezwa ni hapa..

Mtoto wako, anakuja kuishi Tanzania hiii hiii unahangaika awe mzungu..hahaha.. na anafundishwa matatizo ya kizungu, kwa lugha ya kizungu..akitoka huko ameshakuwa mzungu anakuja kwa watanzania mtaani anaanza moja.. 🙂

Na cha kufurahisha ni sisi wazazi ndio tunakuwa tumewanunulia watoto wetu hiyo delay huku mtaani. Elimu tuliyomnunulia ndio imekuwa kikwazo..

Bora kila mwaka ungekuwa unamnunulia mtoto ng'ombe nne.. anasoma shule ya laki tano kwa Temu.. akija kumaliza shule anakuwa na ng'ombe 68, ukiweka kuzaa na kufa hakosi ng'ombe 100 kwenye kipindi cha miaka 16 ya kusomea elimu.

Na elimu yenyewe ndio imekuwa uchuro uchoro mtupu
Dunia imekua kijiji na lugha kuu ya hiki kijiji ni kingereza, zingine ni ziada, sasa ukitaka kujitenga ni juu yako hakuna aliyelazimishwa, ila watoto watakuja kalaumu wakati wanatafuta kazi au wanafanya Biashara
 
Wengi tu watoto wa Jakaya wenyewe wamesoma Bunge Primary

Na walimu wengi walikuwa wake wa mawaziri pale na mbuyuni na hata olympio ... Bunge x kisutu x olympio x mbuyuni x oysterbay primary school x arusha school zote hizi zilikuwa ndio kwa washua washua kwa enzi zile kayumba .. sio KAYUMBA ya SASA ... wote TUNAGONGANA NAO MITAANI HUKU uchinani ...
 
Na walimu wengi walikuwa wake wa mawaziri pale na mbuyuni na hata olympio ... Bunge x kisutu x olympio x mbuyuni x oysterbay primary school x arusha school zote hizi zilikuwa ndio kwa washua washua kwa enzi zile kayumba .. sio KAYUMBA ya SASA ... wote TUNAGONGANA NAO MITAANI HUKU uchinani ...
Eeh wake wa wanene ndio walikuwa maticha mle 😁😁😁 sasa jamaa anashangaa na kila mkoa shule ya namna hio ipo!
Morogoro kuna Bungo Primary, Sua primary, Solomon Mahlangu nazo ni shule za aina hio!
 
Back
Top Bottom