Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

#falmesimba
Habari wadau..

January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.

Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.

Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.

Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi ambazo wanasoma msingi zilikuwepo tayari ila wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..

Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za bei nafuu kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
[/QUOTE]
 
Anasema kweli mkuu

Maarifa yanapatikana kwa usahihi kama msomaji anasoma kwa native language ya origin ya hayo maarifa

Ukibadili kwenda kwingine kunatokea distortiton

Utasema mbona mimi nilipata 1.7,ni kweli katika kila rule kuna exception,wewe ni mmoja kati ya wanadamu milioni 60 TZ....

Usije dhani ina aaply kwa kila mtu,infact kwenye bell curve pale middle ndio wana suffer zaidi...

Na kumbuka kama baba uliweza kusoma bila kujua kizungu sana,usidhani ita apply kwa wanao,maana law of regression ina take effect
Sio kwa sayansi mkuu.
Mkuu tofautisha uongo, opinions, perspectives na facts.

Sasa nilichoandika sio uongo bali ni facts.
Na haiwezekani kupinga facts bila facts sababu utakuwa unakwenda against reality.

Na tayari umeshindwa kutumia facts kutetea hoja yako.
wewe ulisoma english medium?
 
Nani alikwambia anapata lugha peke yake?
Kuna mengi mtoto wa international schools wanapata tofauti na lugha.
Kuna international school na English medium school. Hizi English medium ni Kayumba za kizungu... International school sio kusoma kwa kizungu.. hata Shule ya Kiswahili inaweza kuwa international vile vile..
 
Dunia imekua kijiji na lugha kuu ya hiki kijiji ni kingereza, zingine ni ziada, sasa ukitaka kujitenga ni juu yako hakuna aliyelazimishwa, ila watoto watakuja kalaumu wakati wanatafuta kazi au wanafanya Biashara
Lugha ya kujifunzia!? Au ya Kuwasiliana!?
 
Yaani wewe unataka mtoto asisome umnunulie ng'ombe achunge akamue maziwa?

Unajua elimu haina replacement?

Na hao ng'ombe akifuga atajifunza lini ku-raise productivity bila kusoma?Machineries atanunulia wapi na kujifunza jinsi ya kuendesha ili,kuzalishia hao ng'ombe?

Kizungu hajui,atajifunza vipi machines za milk processing?Au jinsi ya ku-run milk palour?Zote hizi elimu zake serious zinapatikana kwa kizungu,kizungu hujui,maarifa haya uatayapata wapi wewe ndugu?

Au kama Kingereza chako cha ugoko,maarifa utayasomaje na kuyajua sawia kama lugha yaliyoandikwa hayo maarifa ni Kizungu halafu hukijui?

Kwanini uende shule usome kwa Kingereza?....Ni kwamba maarifa ya dunia natively yamejengwa na wazungu na yameandikwa kwa usahihi kwa lugha hiyo....Maarifa advanced makubwa zaidi huwezi badili kutoka kingereza kuja local language bila kua na athari

Ili uweze kupata maarifa aliyogundua mzugnu huna budi kujua Kingereza kwa ufasaha ili uweze kuyasoma na kuelewa na kuyatumia uweze kufanikiwa,bila hapo tunafeli!

Watanzania wanafeli mitihani shuleni sababu tu hawajui Kingereza vizuri...solution sio kubadili English iwe Kiswahili,ni ghali mno kutoa maarifa kutoka katika native language yake kwenda Kiswahili

Ni ghali na inachukua muda mrefu mno,sio chini ya miaka 100....kwa matokeo ya haraka ni kusoma lugha hiyo hiyo na kuyapata hayo maarifa na kuyatumia kupata maendeleo ndani ya miaka 5 au 10

Oh china imeweza,blah blah..China ina miaka 5000 ya civilization,wao binafsi wana elimu yao binafsi walivumbua na wanaitumia,sisi tuna miaka mingapi vile?50 years

Kwa sasa,dunia hii,hukopi maarifa ya mzungu you are dead,kajidanganyeni machooni huko
So kweli.. maarifa yadunia sio relatively new kama unavyotaka kuamini. Maarifa yalikuwa akiwa kihindi, kichina, Kigiriki, Kilatini .. kiingereza kimeyasambaza tuu.

Huwezi kuniambia maarifa ya kutumia artemisia kwenye kutibu yalikuwa ya kizungu! Wachina wametumia for over 2000 years.. kizungu kimesambaza tuu haya maarifa.

Tusiifocus kutaka kujua kuwasiliana wakati hatuna cha kuwasiliana.. na wazazi chanya hayajengwi na lugha ya kigeni.. hata siku moja.
 
Sehemu tulipowezwa ni hapa..

Mtoto wako, anakuja kuishi Tanzania hiii hiii unahangaika awe mzungu..hahaha.. na anafundishwa matatizo ya kizungu, kwa lugha ya kizungu..akitoka huko ameshakuwa mzungu anakuja kwa watanzania mtaani anaanza moja.. 🙂

Na cha kufurahisha ni sisi wazazi ndio tunakuwa tumewanunulia watoto wetu hiyo delay huku mtaani. Elimu tuliyomnunulia ndio imekuwa kikwazo..

Bora kila mwaka ungekuwa unamnunulia mtoto ng'ombe nne.. anasoma shule ya laki tano kwa Temu.. akija kumaliza shule anakuwa na ng'ombe 68, ukiweka kuzaa na kufa hakosi ng'ombe 100 kwenye kipindi cha miaka 16 ya kusomea elimu.

Na elimu yenyewe ndio imekuwa uchuro uchoro mtupu
Saws mkuu,hivi ngombe mia unawafugia wapi hapo darasarama.
 
Mwambie kabisa wewe ni mwanaume, shida yako unadanganya watu kuwa ni demu halafu baadae kwenye simu wanakuja kugundua kuwa ni mwanaume ndipo unapoleta shida wewe kijana
kumbe na wewe umeshamgundua[emoji2][emoji28]
 
Wakati Mimi ninasoma msingi, english medium za kipato cha kati level za tusiime zilikuwa kibao.. kama st marys kila wilaya, olimpio, esacs, academic, jk nyerere, taps
Ishu sio zilikuwepo, je zilikuwa zishafikia level za kufikisha wanafunzi Hadi chuo kikuu?

English medium nyingi wanafunzi wao wamefika vyuo vikuu na kumaliza kuanzia miaka ya 2010

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
St marys imeanza lini kufikisha watoto chuo kikuu? Vp kuhusu esacs, na olimpio pia?
 
"Kjana wangu yuko std seven hizo shule, sikifichi anawa challenge hata majamaa waliosoma hizo ma A level za kata"
Kumbe jamaa anamsifia kijana wake kuwashinda ma A level lugha ya kigeni, mimi nilijua mpaka Applied Math, Phy, Bio n.k.
Alisikika mwanaJF mmoja akisema huo ni Utopolo Pro Max.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
St marys imeanza lini kufikisha watoto chuo kikuu? Vp kuhusu esacs, na olimpio pia?
St Mary's imeanzishwa mwaka gani na kipindi inaanzishwa kulikuwa na shule ngapi za English medium?

Halafu olimpio ni shule ya serikali sijui umeiweka ya nn hpo?

Naomba unielewe shule za English medium zimeanza kutoa graduate in bulk miaka ya katikati ya 2000 na wengi wao walikuja kuanza kuhitimu chuo kikuu kuanzia miaka ya kuanzia 2010

Now soko la ajira wamelikamata sababu wanajua kiingereza kwenye interview wanatupiga bao sie at kayumba

Je olimpio sio english medium? Mbona unaruka ruka kwenye swali lako? Umeuliza kuhusu english medium ama shule za private tupu?

St marys ni ya muda mrefu pia.. mimi namaliza elimu ya msingi mwaka 2002.. st marys ilishatoa wahitimu wa msingi miaka kazaa kabla mimi sijamaliza... na st marys high school ilikuwa imeshaanzishwa pia. Kuna watu wamesoma st marys kuanzia msingi mpaka high school nawajua na wamehitimu form 6 mwaka 2006. Na walioenda chuo kikuu walihitimu degree zao 2009..

Je mwaka 2009 ni sawa na kusema kuanzia mwaka 2010?

Nimetoa mfano kwenye comments juu ya rafiki yangu ibra ambaye amemaliza msingi mapambano sinza mwaka 2005.. na bado amekimbiza na ameajiriwa nafasi kubwa absa na kuwazidi hao english medium ambazo zilikuwa zimejaa kitambo
 
Usitokwe mfano wa mtu mmoja Kati ya watu elfu moja

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
kwa hyo tumekubaliana vp mtoto asome za kata ama azidi kuchoma mshahara mpaka chuo kikuu ??

but.
TOTO likipiga shule za kata likaenda chuo kwa akili zake hafu linamaliza chuo home kuna M15 zpo benki znamsubili huyu dogo afanye biashara... hapo safi sana hata mbinguni mzazi anaenda na mvinyo kama kawa atagongo huko
 
Ukifanya hivyo Na toto lenyewe litasema baba au mama jembe... ila sasa kosea lipeleke shule za milioni tatu.. limalize shule halafu usilipe mtaji wala nyumba ya urithi.. linasahau ada ulizokuwa unamlipia kila mwaka milioni 3 linaona baba kilaza tu
 
binafsi namtoto m1 mwakani shule. shule za m3 atazisikia kwa waajiliwa wanaoshindana kutumia mishaharaa

katoto kangu kangekua kanamaliza hata leoo ningekapa hiyo pesa m15 ya biashara hafu katafute binti wa aliyesomeshwa maprivate mpka chuo hana mchongo anasubili ajira kisha ampose na kumuoaa ngoma drooo... nasogeza maarifa home
 
Umetisha sana...hii comment yako nime sreen shot na kumtumia mama watoto aisome... maana anapenda sana shule za gharama huku hana hata mia
 
Back
Top Bottom