Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Somo linalomshinda ni kiswahili tu ndo nataka nimpige tuition.
Hivi kumbe na Kiswahili ni kipengele kwa Mtoto wa Kibongo, itakua mwanao alizaliwa Uganda au Australia au wazazi huwa hamuongei kiswazi nyumbani na pengine hata mtaani kiswahili ni kipengele.
 
Bu
True.. mtu analipa milioni 3 ama nne kwa mwaka ili mwanae ajue kiingereza tu... huku sylabus anayofundishwa mwanae wa tusiime ni ile ile ambayo wa elimu bure anafundishwa. Tofauti ni lugha tu.

Tatizo la elimu yetu ni sylabus.. jaribu kuwaza hiyo milion 3 kila mwaka mnunulie kiwanja ndani ya miaka 7 atakuwa na asset kiasi gani huyo mtoto.

Mtoto atakuwa na uhakika wa kupata elimu ya juu ama basic need hata kama mzazi umefariki...
Huo upumbavu binafsi nilishakiri humu sitakaa nifanye 😁😁😁! Hio hela bora umwekezee mtoto tu akija kukua mtu mzima apate pa kushika. Ni fedhea sana kulipa mamilioni kisha mtoto aje kuzunguka na kibahasha kama mwendawazimu 😂😂😂
 
Bu

Huo upumbavu binafsi nilishakiri humu sitakaa nifanye [emoji16][emoji16][emoji16]! Hio hela bora umwekezee mtoto tu akija kukua mtu mzima apate pa kushika. Ni fedhea sana kulipa mamilioni kisha mtoto aje kuzunguka na kibahasha kama mwendawazimu [emoji23][emoji23][emoji23]
Bro una watoto? If yes, wangapi?
 
Aah sawa mkuu,ila kama kauwezo kapo pambana mkuu mpeleke private mkuu atapata ka elimu katakako muwezesha hapo mbeleni akawa na kauwezo ka kuji express him/her self mbele ya wasomi Wa mataifa mengine kwa ujasiri.

Hivi unajua kwa nini Baba yetu mpendwa aka RAIA no one alituaibisha alipoulizwa kaswali kadogo na mwandishi Wa habari akiwa na museveni,ye akajibu tu simple eti do you rove corruption.
Mimi sijasoma huko Academy lakini siwezi kushindwa kujieleza mbele ya mtu yeyote.

Tunahadaika kirahisi sana.. watoto wengi wa Academy wanajua kiingereza kidogo na kiswahili kidogo.. huo ndio ubaya..

Mawazo yao mengi yanaathiriwa. Na mazingira ambayo ni ya kiswahili.. anajifunza nadharia kwa kizungu.. halafu aje awe mbunifu wa kuzitumia nadharia hizo kwa kiswahili kuvumbua haiwezekani.

Watoto walipaswa wasome kila somo kwa kiswahili.. mwalimu angekuwa na uwezo wa kuwa extra na kuaccomodate knowledge mpya kirahisi.. na elimu ingekuwa relevant. na wapate waalimu wa kingereza ikibidi kutoka Uingereza wawafundishe lugha ya kiingereza.

Nadharia content yake haibadilishwi na lugha. Ukifunza hesabu kwa kichina, kiarabu au kiingereza inabakia kubwa hesabu tuu... Mpe mtoto ujasiri wa kujifunza katika lugha ambayo anauhuru nayo.. hizo nyingine ni lugha tu za kuwasilisha anachokijua.
 
Hivi kumbe na Kiswahili ni kipengele kwa Mtoto wa Kibongo, itakua mwanao alizaliwa Uganda au Australia au wazazi huwa hamuongei kiswazi nyumbani na pengine hata mtaani kiswahili ni kipengele.
Changamoto hasomi shule ya kutwa muda mchache sana wako mtaani,ila issue ya corona ikasaidia akakaa kitaa muda mrefu.

Pia madogo wakiwalikizo hawajichanganyi sana vijiweni wako home tu wanajifanya wazungu eti wanaangalia Nickelodeon.

Jkiwasemesha kiswazi wanajibu kidhungu tu.
 
Shule za kayumba ni za kipimbi mi sina kitu ila nikiwa hai na nguvu zangu sitakubali mwanangu apitie niliyo yapitia Eee Mungu nisaidie
Shule ya Kayumba wanayosoma watoto wa viongozi haiwezi kuwa ya kipimbi mzee 😁😁😁!
Huwezi fananisha Bunge Primary na shule ya kata uliosoma wewe.
But both are government schools.
 
Ukimsomesha mwanao kayumba mtaani unachekwa,kuna mother mtaani kapanga chumba kimoja halafu anamsomesha mwanae efemu akademia anachukuliwa na gari.......Ni maamuzi tu tuwaache mambo yakiwa magumu watawarudisha KAYUMBA.
Huo ndio utopolo Pro Max! Yani ukishindwa ma Ada huko sindio fedhea kubwa zaidi.
 
Nina mmoja kwa sasa ila naplan niongeze wengine wa 4
Ok. Binafsi naona elimu ni msingi wa maendeleo ya wanangu. Na elimu hapa ni zaidi ya kufaulu darasani.

Kuna vitu vingi vya ziada shule binafsi (sio zote) zinatoa ambazo hupati shule za serikali.

Mfano, hata kujiamini na kujieleza tu kunaweza kuwa ni mlango wa mafanikio katika baadhi ya maeneo. Au kuwa na mtazamo fulani juu ya maisha na exoosure.

Hiki kitu kwa shule za serikali ni bidhaa adimu. Hapa kata yetu, mwaka huu tu drs la kwanza wameandikishwa wanafunzi elfu 1. Nilikua naongea na ndugu ambaye ni mwakimu hapo, walimu wako overhwelmed. Unakuta stress zote anamalizia kwa watoto.

Kwa kweli kwa kadri hali yangu ya fedha itakavyoruhusu, nawapeleka shule binafsi wanangu.

Hii hainizuii kuplan pia future nzuri kwa ajili yao. Nafikiri, tupambane kiuchumi tuwakwamue watoto.
 
Mimi sijasoma huko Academy lakini siwezi kushindwa kujieleza mbele ya mtu yeyote.

Tunahadaika kirahisi sana.. watoto wengi wa Academy wanajua kiingereza kidogo na kiswahili kidogo.. huo ndio ubaya..

Mawazo yao mengi yanaathiriwa. Na mazingira ambayo ni ya kiswahili.. anajifunza nadharia kwa kizungu.. halafu aje awe mbunifu wa kuzitumia nadharia hizo kwa kiswahili kuvumbua haiwezekani.

Watoto walipaswa wasome kila somo kwa kiswahili.. mwalimu angekuwa na uwezo wa kuwa extra na kuaccomodate knowledge mpya kirahisi.. na elimu ingekuwa relevant. na wapate waalimu wa kingereza ikibidi kutoka Uingereza wawafundishe lugha ya kiingereza.

Nadharia content yake haibadilishwi na lugha. Ukifunza hesabu kwa kichina, kiarabu au kiingereza inabakia kubwa hesabu tuu... Mpe mtoto ujasiri wa kujifunza katika lugha ambayo anauhuru nayo.. hizo nyingine ni lugha tu za kuwasilisha anachokijua.
Mkuu ungejua kuwa Dunia inakuwa na pia inazeeka,dunia ya sasa hivi ni nyingine yani ni kama kakijiji Fulani.

Ni uwezo tu hatuna ila kila mzazi anatamani hata mtoto wake a some Tanganyika au braeburn,yaani asisome ungese wa NECTA.
Yaani akifika la tatu akifaulu anarushwa la tano mambo ya Cambridge full.

Mtoto Ana miaka 21 tayari ni pilot.
Lakini ndo hivyo uwezo hatuna basis za bure zinatuhusu.
So unajua zetu wabongo mwenye vxr l/cruiser anamuheshimu mwenue vitz ila mtembea kwa miguu anamdharau mwemnye vitz,eti naue atasema ana Gari.
Ndimi comedian wako chiburabhanu.
 
Back
Top Bottom