Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Sikatai. Hata mimi nimesoma huko mwanzo mwisho. Na kutokana na background yetu kama famikia, naweza kusema nimetoboa kiasi.

Ila sasa, usitumie hii kumfanya mwanao awe mnyonge baadae. Yes, anaweza kufuata nyayo zako na akatoboa hata kwa Kayumba. Lakini what if he doesn't?

Private sio uhakika wa kutoboa. Lakn walau kuna ziada inapatikana ya kutumia hata asipotoboa.
Ukiwa mji wa kielimu.. ni kumjengea mtoto tabia.. anasoma shule ya kawaida.. anatumia muda wake vizuri. Anaratiba ya library, ana tembelea maeneo kujifunza kwa vitendo ndio kumjengea mtoto uwezo. Sio kulipa hela nyingi apewe taarifa na kuaminishwa vitu.

Apate vitabu, mtembeze aonane na Mainjinia, tofauti tofauti.. aone processes mbalimbali anazojifunza kwa nadharia.. hivyo ndio kumpa mtoto elimu..
 
Kufaulu ni kipimo cha kwamba knowledge iliyokusudiwa ameipata

Wenye kazi nzuri wengi walifaulu. Mzazi anajua watu kibao ambao walifaulu kisha wakapata kazi nzuri.

Kuanzia kwa Benno Ndulu, Kimei,nk
Ishi na mentality hio hio mkuu, miaka 30 ijayo ndio utaelewa kwamba kupata AAAA inaweza isiwe ishu ya maana vile vile.
 
Hiyo ni sawa na yule mtu aliyemuuliza mlevi wa pombe, kiasi anachokunywa kwa siku,mwezi na hadi mwaka, gharama yake ilikuwa ni sawa na bei ya kununulia Benzi, lakini muulizaji alipoulizwa wewe ni mlevi?akajibu hapana, akaulizwa una benzi ngapi? Akajibu hana hata moja. So kwa kutomsomesha mtoto kwenye hizo shule hakumaanishi kuwa utaserve hela na kumnunulia huyo mtoto any asset, kama uwezo upo, hata wa kuteseka msomeshe mtoto, vinginevyo waweza kosa mwana na maji ya moto
True.. mtu analipa milioni 3 ama nne kwa mwaka ili mwanae ajue kiingereza tu... huku sylabus anayofundishwa mwanae wa tusiime ni ile ile ambayo wa elimu bure anafundishwa. Tofauti ni lugha tu.

Tatizo la elimu yetu ni sylabus.. jaribu kuwaza hiyo milion 3 kila mwaka mnunulie kiwanja ndani ya miaka 7 atakuwa na asset kiasi gani huyo mtoto.

Mtoto atakuwa na uhakika wa kupata elimu ya juu ama basic need hata kama mzazi umefariki...
 
Hivi huu msemo Wa eti watoto wanaosoma shule za academics sijui private school eti wanaishia kujua lughatu,mi natofafautiama na we we mkuu,Kijana wangu yuko std seven hizo shule,sikifichi anawa challenge hata majamaa waliosoma hizo ma A level za kata.na wanamkubali mbaya.
Hakikisha awachallenge kimaisha pia, sio amalize degree na ma AAA yake uanze kumlisha ugali akiwa 30yrs hapo kwako.😁😁😁 sababu hana pa kupeleka cheti apate chochote kitu.
 
Ubungo vijijini sema

Ubungo mjini mwisho river side

Kama TFDA na maabara iliyofungwa mashine ya kupimwa corona nchi nzima ipo kijijini sawa .. sina la kubishana na wewe...ila hujue mtu yeyote anaesafiri nje ya nchi zama hizi lazima aje kata yangu ya makuburi... university of dar es salaam biggest hostel.. mabibo hostel zipo kata yangu ya makuburi
 
Kwanini kupata AAA sio ishu
Ni ishu kama utaonekana una umuhimu mahali uende ukasaidie ulipwe pesa! Ila kwa trend inavyoenda 30yrs ahead hii elimu ya kibongo haitakuwa na maana yeyote.
 
Shule ya Kayumba wanayosoma watoto wa viongozi haiwezi kuwa ya kipimbi mzee [emoji16][emoji16][emoji16]!
Huwezi fananisha Bunge Primary na shule ya kata uliosoma wewe.
But both are government schools.
Noma hiv unaanzaje kumpeleka mtt wako shule ina walimu 10 wanafunzi 600+ walimu wenyewe wanamtumia mtoto wako ndo awauzie biashara zao za kababu na barafu shuleni
 
Noma hiv unaanzaje kumpeleka mtt wako shule ina walimu 10 wanafunzi 600+ walimu wenyewe wanamtumia mtoto wako ndo awauzie biashara zao za kababu na barafu shuleni
Hata hao waliopeleka watoto wao huko wangekuwa na uwezo kama wako wasingekubali hali hio!
 
Ishi na mentality hio hio mkuu, miaka 30 ijayo ndio utaelewa kwamba kupata AAAA inaweza isiwe ishu ya maana vile vile.

Ishi na mentality hio hio mkuu, miaka 30 ijayo ndio utaelewa kwamba kupata AAAA inaweza isiwe ishu ya maana vile vile.
Ishi na mentality hio hio mkuu, miaka 30 ijayo ndio utaelewa kwamba kupata AAAA inaweza isiwe ishu ya maana vile vile.
Akifaulu hata kubeba box kunakuwa Na wepesi akienda Ulaya,US.
Wanaoponda kufaulu in real sense wanahaha watoto wao wakifeli.
 
Mimi wakwangu watasoma kayumba kama nilivyosoma mimi hadi nikafika Chuo.. kama ni mwenye akili atafanikiwa pia, kama ni wa kusuasua ataishia atakapoweza ndipo hatua zingine zitachukuliwa[emoji3525]
Safi kabisa.
 
Ni ishu kama utaonekana una umuhimu mahali uende ukasaidie ulipwe pesa! Ila kwa trend inavyoenda 30yrs ahead hii elimu ya kibongo haitakuwa na maana yeyote.
Nimependa umetambua umuhimu wa AAA nilitegemea ulete hoja sijui maarifa sijui nini sasa mtoto mmoja ana maarifa na CCC na mwengine ana maarifa na AAA wapili si mzuri zaidi.
 
Sehemu.tulipowezwa ni hapa..

Mtoto wako, anakuja kuishi Tanzania hiii hiii unahangaika awe mzungu..hahaha.. na anafundishwa matatizo ya kizungu, kwa lugha ya kizungu..akitoka huko ameshakuwa mzungu anakuja kwa watz mtaani anaanza moja.. 🙂

Na cha kufurahisha ni sisi wazazi ndio tunakuwa tumewanunulia watoto wetu hiyo delay huku mtaani. Elimu tuliyomnunulia ndio imekuwa kikwazo..

Bora kila mwaka ungekuwa unamnunulia mtoto ng'ombe nne ..anasoma shule ya laki tano kwa Temu.. akija kumaliza shule anakuwa na ng'ombe 68 ukiweka kuzaa na kufa hakosi ng'ombe 100 kwenye kipindi cha miaka 16 ya kusomea elimu.

Na elimu yenyewe ndio imekuwa uchuro uchoro mtupu
Ubarikiwe sana, [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Unatumia nguvu nyingi sana ktk kumsomesha mtoto, mwisho mtoto anamaliza Shule hana kazi na wewe mzazi huna kitu. Hata akipata kazi fedha anaanza kukurudishia kwa kukulea.

Ila ukianza kuwekeza, hata kama atapata Elimu ya kawaida. Mzazi akipata hela mtoto lazima atapata hela.
 
Hawana exposure..na kujiamini.
Kujua lugha hakukufanyi smart... Au kujua kabla ya mwingine hakukufanyi uwe na akili zaidi yake.. mtoto anatakiwa ajue hilo mapema maishani.

Elimu ni kutafsiri maarifa uliyopewa au kupata katika maisha yako ya kila siku. Mtoto anajua kiingereza hajui kufunga kamba za viatu inamsaidia nini!?
Mtoto anajua kiingereza hawezi kwenda sokoni mwenyewe na kurudi itamfaanini!?

Logic and Reasoning ndio muhimu. Kwa level za chini watoto wanatakiwa kuwa curious... Mid ages waweze kuleta connection na theory na uhalisia katika maisha yao.. mtoto awe huru atleast saa 9 saa kumi aende akacheza apumzike kutoka shule ... Ukizidisha hapo unaua curiousity mtoto anakuwa duster ananyonya kila kitu kama kilivyo without Reasoning
Ahsanteeeeeeeeh.
 
Back
Top Bottom