Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mie huwa nabaki kushangaaaah "hiiiiiiiii"
 
Hakika
 
Ni ishu kama utaonekana una umuhimu mahali uende ukasaidie ulipwe pesa! Ila kwa trend inavyoenda 30yrs ahead hii elimu ya kibongo haitakuwa na maana yeyote.
AAA ya PCM A level . katika 10, 8 watatoboa
 
Hii ndio inaitwa Critical thinking! Walioachana na shule mapema watakuwa mbali sana katika umri ambao watoto wako ndio wanamaliza na mavyeti wanayo ya degree ila kazi hamna! Mzazi umetumia mamillion kibao kusomesha mtu ambaye inabidi uendelee kumlea. Wakati wenzie wana maisha wanaoa 😂😂😂
 
Pita kwa mangi pata 1 kubwa baridi, nakuja kulipa wallah.
 
90% ya wasomi wanafanikiwa?? Ebu tupe definition ya kufanikiwa kwanza!! Maana hao wasomi wa kutegemea mshahara na kununua gari na kujenga kwa mkopo,mshahara ukitoka tarehe 28 baada ya siku 10 ushakata ndio mafanikio hayo?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Oya mkuu FRESHMAN uko pande zipi kesho nikutoe offer moja matata?

Huu ni moja ya uzi bora kabisa wa mwaka huu.

Mimi natumia formula moja: Ni lazima, sio ombi yaani ni lazima wanangu wote level ya primary wasomee shule za kawaida.

Primary ndio level nzuri zaidi ya kujua IQ ya mtoto. Sasa kama umempeleka hizi shule ambazo mwanafunzi wa 1 anakuwa na A na wa mwisho pia ana A kasoro wanazidiana maksi tuu, hapo huwezi kujua uwezo binafsi wa mwanao.

Mtoto akisoma primary za kawaida na akawa hakosi kuwepo kwenye top ten ama five ama three ama akawa anaongoza kabisa basi jua hapo una jembe na unachotakiwa na kumboost kidogo tuu na atafanya maajabu mpaka utashangaa. Sasa huyu hata akienda secondary za kawaida atafanya vzr tuu lkn usiache kumpa guidance.

Kisha sasa wanao ambao watakuwa wazito ndio uelekeze nguvu kubwa kwao. Sio watoto wote wanakuwa wanahitaji nguvu kuuubwa sana, hivyo ni jukumu la mzazi kufanya sorting ya kujua huyu anakaa hapa na huyu anakaa pale.
 
Nimekupenda bure, umeolewa wewe?

Maana wanawake ndio wanazipenda hizi shule za mamilioni vibaya mno ili wauze sura kwa marafiki zao
Ktk maisha yangu nilishasema na hata watu wanajua, watoto wangu watasoma government school, haijalishi sijui nna pesa kiasi gan hat km cha kuweza kuhimili private..

Nyumbani kwetu wazazi wangu wana uwezo mkubwa tyuuh kifedha wa kuweza kutusomesha kwenye shule za magari ya njano, ila walitupitisha ktk shule za kidumu na mifagio huku wakiweka asset za baadae kwetu na wakitiliaa mkazo ktk kupata elimu yetu,

Kwa wakati ule tuliona wazazi ni bakhili na wabinafsi kwa kutuweka shule ambazo hazifanani na uwezo wala status zao km wazazi wa watoto husika, ila leo hii tunajivunia mno tena sana. Na tunashukuru zaidi kwani wazazi walikua wanatengeneza kitu muhimu na bora kwetu.

Now nipo chuo 2nd yr, na faculty yangu n 4yrs, na nasoma kwa pesa zangu, maana sikuomba na wala kuhitaji mkopo, asset ninazomiliki binafsi, kwangu tosha kabisa ku survive maisha yangu yote, na hapa nilipo wala sitegemei ajira hapo baadae labda itokee tyuuh. Ila sio mie kuzunguka na bahasha za kakhi mtaani. Hilo halitakuwepo na halipo.

Nawashukuru sana wazazi kwa msingi huu waliouweka ambao leo tunafaidi matunda yake.
 
Lugha ndio kilakitu mkuu, sikulazimishi lakinin.

Waswahili walisema Samaki mkunje angali mbichi, na shombo lake,
Hapo kwenye Shombo nimechomekea kidogo😛

Madhara ya kuwasomesha watoto awali 'Msondongoma praimari' ni makubwa kuliko faida.

Toto linalemazwa kwa kukaririshwa, linapita kimungumungu hadi Juu,
Matokeo yake na 'Lidigrii' lake lakini hovyo kabisa.
Mahala pa 'Lake' linasema na kuandika 'Rake' bila soni.

Aibu gani hii.
 
Kwahiyo Kiwanja ni bora kuliko Elimu?

Dunia inishushe kituo cha pili jamani.
 

Naomba basi nikuoe.. hela sina za kuonekana tajiri ila njaa sitakulaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…