Ktk maisha yangu nilishasema na hata watu wanajua, watoto wangu watasoma government school, haijalishi sijui nna pesa kiasi gan hat km cha kuweza kuhimili private..
Nyumbani kwetu wazazi wangu wana uwezo mkubwa tyuuh kifedha wa kuweza kutusomesha kwenye shule za magari ya njano, ila walitupitisha ktk shule za kidumu na mifagio huku wakiweka asset za baadae kwetu na wakitiliaa mkazo ktk kupata elimu yetu,
Kwa wakati ule tuliona wazazi ni bakhili na wabinafsi kwa kutuweka shule ambazo hazifanani na uwezo wala status zao km wazazi wa watoto husika, ila leo hii tunajivunia mno tena sana. Na tunashukuru zaidi kwani wazazi walikua wanatengeneza kitu muhimu na bora kwetu.
Now nipo chuo 2nd yr, na faculty yangu n 4yrs, na nasoma kwa pesa zangu, maana sikuomba na wala kuhitaji mkopo, asset ninazomiliki binafsi, kwangu tosha kabisa ku survive maisha yangu yote, na hapa nilipo wala sitegemei ajira hapo baadae labda itokee tyuuh. Ila sio mie kuzunguka na bahasha za kakhi mtaani. Hilo halitakuwepo na halipo.
Nawashukuru sana wazazi kwa msingi huu waliouweka ambao leo tunafaidi matunda yake.